Video: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alihutubia Bunge la Kenya na mustakabari wa uhusiano wetu

Video: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alihutubia Bunge la Kenya na mustakabari wa uhusiano wetu

Sijui tutaambia nini wakenya. Kikwete ukienda Kenya utaficha wapi sura yako?
 
Kikwete ni Raisi wetu mstaafu tunampenda na alifanya yake mengi tu mazuri, pamoja na yote kunaupumbavu mwingi tu jamaa alishiriki kufanya na mwingine kuhusika moja kwa moja.

Moja ya upumbavu wake ni hiyo speech, alijuaje kwamba utawala utakao mfuatia utakuwa na misimamo kama yake licha ya kukili kuwa hapo awali kabla yake uhusiano baina ya hizi nchi mbili haukuwa mzuri kama kipindi chake? Pengine wakati huo alikuwa bado anamatumaini ya kumrithisha mtu wake hatimaye baadae mkeka ukachanika.

Kwa upande mwingine inawezekana alikuwa akiwapaka wakenya mafuta kwa mgongo wa chupa maana huyu jamaa ni ana masterly ya ku twist maneno. Ikumbukwe kuwa jamaa ni mswahili original maana haimake sense kwamba Kenya pekee ndio waonekane kama ndio wateja pekee wa mali ghafi za Tanzania.

Mwisho kabisa, sera za kikwete zilikuwa sahihi kuwashobokea wakenya maana Tanzania tulikuwa wazalishaji haswa na bidhaa ghafi huku tukitegemea industrial products kutoka Kenya, Sera ya viwanda ya Magufuri inashabihiana na ya late Kambarage Nyerere ambayo haina utegemezi mkubwa Kenya. No wonder enzi za Kambarage na Mzee Jomo hazina utofauti na hii enzi ya Dr. na Uhuruto.
Sera za ujamaa pure zilifeli.
 
Alisema anayeweza kuharibu uhusiano na Kenya ni mpumbavu, kisha akasema wapumbavu Tanzania ni wachache kwahiyo hilo haliwezi kutokea. Tena akawahakikishia kabisa. Sasa hivi wakimuuliza sijui atajibu kitu gani!
aliyeanza ni nani?
 
Tatizo mtu mwenyewe alituletea yeye, nani wakulaumiwa?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio Kikwete aliyemleta Magufulin ni Mungu ndiye alimleta baada ya kusikiliza maombi ya chadema.

Chadema waliomba Mungu kuwa wanataka Raisi mkali sio anayecheka Cheka kama Kikwete pia Mungu alijibu maombi ya chadema walioomba Mungu kuwa awape Raisi ambaye hasafiri nje ya nchi kama Kikwete akamleta Magufuli

Chadema msimdukumizie Kikwete huyo Magufuli ndie mlimtaka
 
Alisema anayeweza kuharibu uhusiano na Kenya ni mpumbavu, kisha akasema wapumbavu Tanzania ni wachache kwahiyo hilo haliwezi kutokea. Tena akawahakikishia kabisa. Sasa hivi wakimuuliza sijui atajibu kitu gani!

Uhusiano na Kenya haujaharibika, bali umeteteleka kidogo tu na mazungumzo ya chini kwa chini yanaendelea.

Balozi wa Kenya TZ bado yupo, hajafukuzwa halikadhalika balozi wa TZ nchini Kenya naye anaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Ni hivi punde machungwa ya TZ yatatinga Nairobi bila shida na blue band itatinga Dar es salaam.

Alamsiki!
 
Nukuu alichosema Rais mstaafu, kwamba huu uhusiano kwenda ndivyo sivyo labda tupate nani... wa namna gani... na wa namna hiyo wapo wachacha sana Tanzania...


Cc: mahondaw
Tuisikiize tena hii clip ya kwenye Thread hii ni MAONO tosha aliyokuwa ametuletea JK
 
Kabisa hasa ukiangalia series ya mambo yanavyoendelea kwenye mpaka wetu na Kenya utajuwa tu MPUMBAVU aliyetabiriwa ni nani
Kwanini mnakuwa wapumbavu sana?

Hivi Kenya wamechukua hayo maamuzi sababu tuna uhusiano mbaya? Upi? Je Uganda nao wana uhusiano mbaya na Kenya?
 
Back
Top Bottom