VIDEO: Rais Ruto apigwa na kiatu akihutubia Wananchi wa Kehancha

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mtu mmoja amemrushia kiatu Rais wa Kenya William Ruto wakati akizungumza na wananchi wa Kehancha, Kitongoji cha Migori ambapo leo alikuwa anazindua mradi wa nyumba 298 zenye nafuu kwa wananchi.

Kiatu hicho kilimkosa Rais Ruto ambaye aliendelea kuzungumza na wananchi wa eneo hilo bila kujali kilichotokea.
 
Weka sasa hiyo vid
 
Tangu Wakenya wapigane Mwaka 2007, raia wake wameshindwa kabisa kuwa waoga Kwa Viongozi wao

Tofauti na hapa nyumbani, ambapo raia anaweza kutekwa Mchana kweupe na wasiojulikana na raia wote kubaki kimya bila hata kuchukua hatua 🙌
 
Katika tukio la kushtua lililotokea Jumapili, Rais William Ruto alinusurika kwa fedheha kupigwa na kitu kilichorushwa—kinachoaminika kuwa kiatu—wakati akihutubia umati wa watu katika Mji wa Kehancha, Kaunti ya Migori.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya Kiongozi wa Taifa kuzindua mradi wa nyumba nafuu 298, ambao ni sehemu ya mpango mkubwa wa serikali yake wa kuwapatia Wakenya nyumba za gharama nafuu kote nchini. Rais Ruto alipokuwa akizungumza na wananchi na kusisitiza dhamira ya serikali yake kwa maendeleo, mtu ambaye hajafahamika alirusha kitu hicho kuelekea kwake.
 
Tangu Wakenya wapigane Mwaka 2007, raia wake wameshindwa kabisa kuwa waoga Kwa Viongozi wao

Tofauti na hapa nyumbani, ambapo raia anaweza kutekwa Mchana kweupe na wasiojulikana na raia wote kubaki kimya bila hata kuchukua hatua 🙌
waTanganyika ni mambumbumbu. Mwenge unaozungushwa kila maeneo kila mwaka umeondoa fahamu za watu
 
Mtu mmoja amemrushia kiatu Rais wa Kenya William Ruto wakati akizungumza na wananchi wa Kehancha, Kitongoji cha Migori ambapo leo alikuwa anazindua mradi wa nyumba 298 zenye nafuu kwa wananchi.

Kiatu hicho kilimkosa Rais Ruto ambaye aliendelea kuzungumza na wananchi wa eneo hilo bila kujali kilichotokea.
View attachment 3324644
huku kwetu baso kidogo maana wanachoongea kinakera
 
Wakenya wanafundishwa elimu ya uraia ko hawanaga kuogopa.... Umewahi kusikia chawa wa Ruto? Huko hata wafuasi wa Ruto wanampinga akikengeuka!..

Nyerere aliambiwa anaongoza maiti zinazotembea😃😃😂
 
Back
Top Bottom