Video | Serikali ya Djibouti yavunja mkataba na DP World kuhusu uendeshaji wa bandari ya Doraleh

Hivi hii serikali yetu wanatutakia nini sisi waTanganyika lakini, mnataka hadi damu imwagike ndio muelewe huo mkataba haufai?
 
Hiyo stori ni ya siku nyingi na Djibouti ameshashindwa kwenye mahakama ya kimataifa.
Sawa mkuu, ila habari inafunua madhaifu ya dpw. Ndiyo maana wanasema kesi zisikilizwe S.A. Kama Djibouti wameonja machungu ya dpw na wanatamani kujiondoa sisi tutie maji kichwani kusubiri zamu ya kunyolewa.
 
Inaumiza sana
Generational Trauma!
Kuna wale wenye hisia za kuupinga, tena kwa nguvu zote.
Kuna wale wanaoupinga kwasababu ya madoa yaliyomo kwenye 'sijui niuite nini tena'....Mkataba, MOU, IGA,.
Kuna wale wanaoupinga kwasababu za Uwekezaji tulioufanya Watanzania, Kuna wanaoupinga kwa Sababu ya Uzanzibari na Utanganyika, Kuna wale wanaoupinga kwa sababu ya Historia ya DPW, vilevile Kuna wale wanaoupinga kwasababu kwa sababu wanajua fika kuwa huo mkataba pamoja na Mabilioni ya Dola zinazo zungumziwa kuwekezwa, hazitawafikia kamwe.

Generational Trauma ni athari za kisaikolojia ambazo mateso kinachowapata watu kinawapata vizazi na vizazi vilivyofuata katika Jamii...

Kwa mfano, mateso ya pamoja yaliyoshuhudiwa na waathirika wa mauaji, ukatili, ubakaji, na mateso mengine n.k na baadhi ya makabila ya Watanganyika/Wafrika weusi wakati wa utumwa. Uliofanywa na Waarabu na Wazungu!

Upo uwezekano mkubwa kuwa tuna experience hivi Viwewe sasa hivi.

Inauma kwa kweli.
 
Uwepo wa DP World kule Somaliland au Puntland/Bosaso kinyume na maadhimio ya bunge la Somalia ni uharamia. Hutaki unaacha.
Watajijuwa, siku hizi kigezo chetu cha uchumi ni Somalia? Huko hata USA katoka mbio.

Hizo bandari zote za Somalia ni za watu binafsi., sasa hata sijuwi unataka kusema nini?

Tupe mfano wa mabawana zetu Waingereza.

Sikuelewi.
 
Yamepita mengi, ila hili halitapita hivi hivi
 
Unganisha tu dots dp world watu wa Dubai walikuwa wanamsapoti Eritrea wakati 90-95% ya Ethiopia cargo inapita hapo bandarini inayoendeshwa na kampuni ya Dubai na hapo hapo Eritrea na Ethiopia hawako vizuri tegemea tu hayo yatokee.
 
Ule Muungano wa Kisomali uliamuliwa kwa mtutu wa Bunduki.

Sio kama sisi tunaotaka muungano uamuliwe Facebook na Twitter Tiktok nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…