Video | Serikali ya Djibouti yavunja mkataba na DP World kuhusu uendeshaji wa bandari ya Doraleh

Video | Serikali ya Djibouti yavunja mkataba na DP World kuhusu uendeshaji wa bandari ya Doraleh

Kwanza shukuru mungu leo unaongea na binadamu mwenye akili nyingi sana kuliko binadamu wa kawaida ....kwa hiyo leo tembea kifua mbale pia msimulie mkeo
Kwakweli Samia anastahili pongezi kuyaongoza mijitu yenye akili kwenye korodani.
 
Kuna Dar Port kuna ile Conteiner terminal pale Vigwaza kuna Isaka Dry port zote ajira hizo kumbuka volume ya mizigo ikiongezeka na makampuni ya usafirishaji yataongezeka zote ajira hizo na kuna indirect nyingi sana.

Mimi ni mdau ndio maana nakuambia.
Kama kitu ni kibovu ukakifanya kiwe mediocre haimaanishi huwezi kukifanya kikawa superb Dar ilipo strategically ina natural advantages; kwahio potential yake sio sababu ya DP World au hata Aliens kutokea Mars; ni utendaji wa kizalendo na mikataba yenye busara na akili;

Hakuna sababu ya kuwapa watu exclusivity na monopoly hatushindwi kuwapangisha hata mataifa tofauti kwa kazi tofauti (wagombanie wenyewe kwa wenyewe hapo tutakuwa na negotiation power) ila ukianza negotiation at a weaker position au kuona kwamba unapewa msaada / Hisani matokeo yake tutaendelea kula makombo na kuwafunga mpaka vitukuu kwa mikataba ya ajabu ajabu...
 
Muhtsari
  • Serikali ya Djibouti yavunja Mkataba wa Bandari ya Doraleh na DP World
  • Sababu za kuvunja Mkataba ni kutokuwepo kwa maslahi kwa Taifa la Djibouti na rushwa iliyotolewa na mkuu wa bandari
  • Serikali ya Djibouti yaishtaki DP World kwa madai ya ukiukwaji wa Mkataba

Serikali ya Djibouti imeamua kuvunja mkataba wa uendeshaji wa bandari ya Doraleh iliyokuwa inasimamiwa na kampuni ya DP World kutoka Falme za Kiarabu. Hatua hii imefuatia uchunguzi uliofanywa na serikali hiyo uliobaini kuwa mkataba huo ulikuwa na masharti yasiyo na tija kwa taifa la Djibouti na ulikuwa umeingiwa kwa njia ya rushwa na aliyekuwa mkuu wa bandari.

Serikali ya Djibouti imesema kuwa imefungua kesi dhidi ya DP World kudai fidia na kurejesha mali zake zilizokuwa chini ya usimamizi wa kampuni hiyo. Serikali pia imesema kuwa itatafuta mshirika mpya wa kuendesha bandari hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi hiyo na ukanda mzima.

Pia soma |
Watawala wa Africa ni wachache sana wenye macho ya kuona, walio wengi wana macho tu ya uumbwaji. Ukiangalia Tz tunachopishana upande mmoja unaelezea mapungufu ya mkataba, an wakati huo huo mtawala anazungumzia ufanisi badala ya kujibu hoja zinazotolewa juu ya mkata husika., neno UPOTOSHAJI, UCHOCHEZI ndiyo nguzo yao.
 
H
Hatuwezi kwasababu serikali ya CCM ni takataka. Chukulia mfano wa Biswalo Maganga, rais analalamika jamaa katuibia mabilioni hapohapo anampa teuzi. Kwa staili hiyo unafikili tutatokaje
CCM ndio mzizi wa fitina.
 
Tuwape kwanza ATLC inayolitafuna taifa lakini nasema hatuwezi.
Ndege karibia dunia nzima zina-run at a loss Huwezi linganisha hii bandari (commanding height of the economy) na shirika la ndege; Kwahio hata Quatar Airways n.k. zipo heavily subsidized ingawa faida yake kwa nchi inaweza ikawa indirectly ila directly sidhani hata kama wana-break even....

Kwahio hili la ndege hata tungewaleta Budget Airlines all over the world waka-compete; By the way nikirudi katika mfano huo huo nilioutoa kwenye Ndege kwanini tusiwalete hawa wanaoweza from all over the world waka-compete (ikibidi kwa tender za miaka mitatu mitatu to be renewed accordingly) Mpaka pale tutakapoweza...
 
Ndege karibia dunia nzima zina-run at a loss Huwezi linganisha hii bandari
Rwanda shirika lao la ndege wamewakabidhi Qatar na Dry port yao wamewapa wawekezaji wa DPWORLD sio wajinga wanatafuta solution ya matatizo yao tofauti na sisi tumekalia siasa.
 
Rwanda shirika lao la ndege wamewakabidhi Qatar na Dry port yao wamewapa wawekezaji wa DPWORLD sio wajinga wanatafuta solution ya matatizo yao tofauti na sisi tumekalia siasa.
Rwanda ana nini ? Hivi Rwanda ana hata theluthi ya natural advantages kama sisi ?

Aisee ni sawasawa useme yule kipofu anatumia fimbo kwanini na mimi nisitumie fimbo wakati wewe unaona ? Ukweli disadvantage kubwa tuliyonayo ni between our ears.....
 
Rwanda ana akili.
Rwanda anachofanya ni the best kwake kutokana na disadvantage alizonazo; Sisi na vitu tulivyonavyo tungekuwa hatujilinganisha na Rwanda tungekuwa tunawaza ni vipi tunaweza kuzalisha umeme na kulisha nchi za Africa au ni vipi kuliko hip Dry Port yao kupewa DP World tusipewe sisi...

Hio ndio inaitwa Aiming for the Moon even if you Miss you will hit the Stars (Lakini kizazi cha walamba asali wa sasa they settle for mediocrity) wamegeuka kuwa madalali (even that they seem to do it wrong, wangewachukua wauza magari au mitumba Kariakoo huenda tungepata a better deal...

Nina uhakika Tanesco ndio inafuata kuuzwa wakati huenda Ingeweza ikawa Cash Cow ya Nchi....

 
Back
Top Bottom