Video: Tuacheni utani, Kabendera anatia huruma

Video: Tuacheni utani, Kabendera anatia huruma

Kwani anashitakiwa kwa kutakatisha fedha ama kuandika makala dhidi ya Magu? Halafu Magu ana mamlaka ya kusamehe watu ambao kesi zao bado zinaendelea mahakamani?
Wangapi wamesamehewa na kesi zao zilikuwa zinaendelea mahakamani ? Waliandika barua na pesa wakarudisha. Eric pia aliandika barua.
Hujui kuwa maandishi yake ndo yaliwafanya wazee wa kazi wamchunguze na kukuta kumbe analipwa mamilioni ya dola na hayalipii kodi.
Kila jambo hutokea kwa sababu.
 
Kwani Kabendera alipanda nini na anavuna nini?

Alipanda umbea na chuki kwenye gazeti la nje kwa kificho akapata pesa akala na nduguze na familia yake, sasa anavuna matunda ya usariti, nyie ambao hamjatumia pesa ya dhambi mnalialia tu. Kama alijua ukosoaji wake ni halali kwa nini hakuliandikia gazeti la Tanzania daima tungepata na kodi maana watu wangelinunua machapisho yote.
 
Wewe ukweli unaujua?

Kwani Pascal Mayalla analaumiwa kwa lipi?
kuna uzi uliletwa humu kwamba ndugu pasco ndiye aliye mchongea Erick, kuna vijana wameushikilia ule uzi kama marejeo yao bila hata kujishughulisha kuutafuta ukweli

Je kosa la pasco ni kuitafsiri makala na kuileta humu?

wabongo bhana!!

mimi nijuavyo Erick angekamatwa tu kutokana na lugha aliyokua anatumia kwenye makala zake.
 
Huyu jamaa tukiacha unafiki alimtukana sana Magufuli, mbaya alikuwa anatumia gazeti na maadui zetu wazungu... Tena aombe sana Mungu bado yupo hai, anajua Jamal Khashogy alicho fanyiwa baada ya kuichafua nchi yake na kukimbilia Marekani?



Sent using Jamii Forums mobile app
Uzuri n kwamba imefikia mahali hamuwezi kujificha tena, mmeamua kuweka wazi kwamba mateso anayoyapitia/wanayoyapitia wengi ni maagizo ya magufuli
 
Kutoka kwenye hekalu Mbweni mpaka kwenye Cell Segerea.Na Magu alimpania hatoki humo. Kila Magu akitaka kumsamehe anakumbuka "John Magufuli is bulldozing the opposition and wrecking the economy "
The dinosaur of Dodoma.

Hivi hapo kuna tusi? Hayo ni maneno ya kawaida tu kumuelezea mwanasiasa. Tatizo ni hicho kikosi cha kumhami rais! Wengi wao ni hoodlums wasiojua kuwa uongozi wa kisiasa hauwezi kutenganishwa na ukosoaji ambao huambtana na sifa za aina hiyo.
 
Alipanda umbea na chuki kwenye gazeti la nje kwa kificho akapata pesa akala na nduguze na familia yake, .
Wakati Mwingine ukisoma kinachoandikwa humu JF unapata mashaka kama wote tuliomo humu tuna akili timamu na tunaishi Tanzania.

Alipanda chuki na Umbea kwa nani na kwa nini unadhani alifanya kwa kificho? Wewe ulitaka fedha alizolipwa ale na ukoo wenu?
 
Jamaa kagoma kumsamehe...hata waliomchongea wanasaidia kumwombea msamaha ila ngoma bado mbichi.

Wao kila Jpili wanaomba msamaha, ila kuwasamehe wenzao hilo suala halipo.
 
Back
Top Bottom