Amani iwe nanyi .
Rais Magufuli ambaye Tanzania na dunia kwa ujumla imemjua na kumwogopa kama rais mwenye kasi zaidi ametoboa siri ya mafanikio yake.
Rais Magufuli amesema katika safari yake ya mafanikio kisiasa tangu kuanza mpaka leo ,wote waliojaribu kumkwamisha walikwama wao! Hali hiyo ilidhihiri kwenye wizara zote alizopita na hadi Sasa ni rais wa Tanzania.
Akiwa rais wa awamu ya tano wafuatao walijaribu kumkwamisha wakaishia kukwama wao kwa aibu kubwa.
1. Mange Kimambi.
Huyu alishambulia sana mwanzo wa utawala wa rais Magufuli . Alitoa matusi ya kila aina na mwishoni akaitisha maandamano nchi nzima aliyopanga yafanyike siku ya muungano, yaani April 26!
Matokeo yake aliishia kuandamana mwenyewe akielekea kwenye ubalozi huko Marekani, huku watanzania wakimpuuza na kuendelea kuchapa kazi.
Tangu siku hiyo Mange Kimambi akafutika na akamwacha rais Magufuli akiendelea kupeta kwa kuwaletea maendeleo watanzania
2. Tundu Lisu
Huyu nae amefutika tarehe 28/10/2020 baada ya kujaribu kwa miaka 3 mfululizo kukamisha juhudi za rais Magufuli.
Amezunguka duniani kote akimtukana rais Magufuli na Tanzania kwa ujumla lakini katikati ya matusi yake bank ya dunia ikatangaza Tanzania imeingia uchumi wa kati !!
3. Godbless Lema .
Huyu alikuwa mbunge wa Arusha akalipwa na mabeberu kumchafua rais Magufuli hadi akafikia hatua ya kuitangazia dunia kwamba ana ndoto ameoteshwa kuhusu rais Magufuli!!
Godbless Lema amefutika tarehe 10/12/2020 baada ya kutangazwa kuwa mkimbizi wa Canada!!
Lema licha ya kuwa mbunge kwa miaka kumi lakini sasa anaenda kuishi kambini kama wale wakimbizi wa Burundi wanavyoishi kule Kigoma!
4. Freeman Mbowe.
Huyu amefutika kwa aibu kubwa. Chadema ilikuwa na wabunge zaidi ya 100 bungeni ,leo hii ina mbunge mmoja tu!
5. Bernard Membe
Alijiaminisha ni kachero mbobezi mzee wa kazi na bata na akaahidi atamkwamisha na kumgaragaza vibaya rais Magufuli kwenye uchaguzi mkuu wa October 28 mwaka huu, matokeo yake amegaragzwa yeye kwa kukataliwa na hata watu wa Lindi na hatainuka tena!