VIDEO: Tundu Lissu, aliyepigwa risasi akipinga ukabila na u-Mobutu, na yeye aiga kuongea vilugha majukwaani

UKABILA ni nini?

Mtu kuzungumza lugha ya kabila lake ni ukabila?

Ama kuzungumza lugha ya kabila lolote lile ni ukabila?

Naomba kufahamishwa kuhusu masuala hayo!
 
Mleta mada hapo Tundu Lissu yupo jukwaani??? Alafu umewai fika vijijini singida??? Unadhani wanajua kiswahili??? Basi umepotea sana!!!

Hapo Tundu Lissu watu wanamsalimia kwa kilugha chao unataka awajibu kiingereza??? Unataka awajibu kiswahili??
Hata Nyerere aling'atuka mpaka hilo neno likaingia kwenye Kiswahili kwa hiyo lisingekuwa kosa kuzungumza Kisukuma na Wasukuma wa Chato kule Chato lakini kuzungumza Kisukuma na Wasukuma wateule maeneo nje ya Usukuma ndo watu wanahoji. Ugogoni wamejaa.

Uzaramo wamejaa na nchi nzimà wako, hata miradi mingi inapelekwa Usukumani, Burigi, Chato International Airport, Chato Traffic Lights, Geita Port etc, etc.
 
Kama kuzungumza maneno ya kabila lako jukwaani ni "ukabila" basi sidhani kama kuna kiongozi wa Tanzania atapona katika hili.

Sababu hata Mwl. J.K. Nyerere aliyewahi kukemea ukabila naye wakati mwingine alikuwa akizungumza kizanaki katika hotuba zake. Alipokuwa akienda kwao je ilikuwaje?

Nini maana ya ukabila?
 
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano...
Kuongea kilugha si ukabila, wapo watanzania wengi sana wasiokijua kiswahili, hao hatuwezi kuwaita wabaguzi au wanaukabila. Unapofanya kampeni tumia lugha zote za mawasiliano uzijuazo kulingana na eneo na kama hauijui weka mkalimani, sheria haizuii.
 
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano.

Alisema Rais huyu anafanya mambo yaliyokataliwa na waasisi wa nchi hii ya kujali kabila lake kwanza.

Na tumeshuhudia Rais huyu wa sasa akipanda majukwaani na kuweka mbele Kisukuma bila kuzingatia misingi ya kuendeleza Utaifa mmoja, unaoongea lugha ya Taifa moja, lugha ya Kiswahili.

Tundu Lissu, kati ya watu wote, na yeye eti ameangukia mtego huo wa kuongea cha kwao majukwaani. Anatuangusha.

Mwalimu Nyerere anaviringika kaburini.

Kwahiyo tumeshaaminishwa kwamba ni crime kwa mwanadamu kuongea lugha ya ancestors wake?

Yaani....
 
Kuongea kilugha si ukabila, wapo watanzania wengi sana wasiokijua kiswahili, hao hatuwezi kuwaita wabaguzi au wanaukabila. Unapofanya kampeni tumia lugha zote za mawasiliano uzijuazo kulingana na eneo na kama hauijui weka mkalimani, sheria haizuii.
Kuna watu wanachanganya mambo kati ya kuongea kwa kabila (kilugha) na ukabila.

Ukabila ni ule utumikao kama kigezo ama sifa katika maamuzi au masuala mbalimbali ya kijamii na kitaifa kwa ujumla.

1. Unakwenda katika maofisi ama taasisi mbalimbali unakuta watu wa kabila moja tu. Kama wewe ni kabila jingine kazi hupati hata kama umekidhi vigezo vyote vya kielimu na nafasi za kazi zipo.

2. Mnampa mtu uongozi sababu tu ni kabila lenu bila kujali kuwa ana uwezo wa kuwaongoza. Akitokea kiongozi hata awe na uwezo kiasi gani mnamnyima uongozi sababu tu si kabila lenu.

3. Mnaoana kikabila. Mtu akitaka kuoa/kuolewa lazima wazazi waulize kabila la huyo mwenza, la sivyo hakuna ndoa.

4. Mnapanda mabasi la kikabila! Aliwahi kusema Nyerere.

Na kadhalika!
 
Lakini kwa Tundu Lissu naweza kumpa benefit of doubt kidogo

..... Tena alikuwa akijishtujia Kama ulivyosema ikimaanisha anajua Ni wrong na kaifanya tu one time
Tundu Lissu, kati ya watu wote, ndio hatakiwi kupewa udhuru.

Ametaka kuuawa akipinga mambo haya, leo anamuigaje vitabia tabia Magufuli ???

Amefanya kidogo, kidogo mara ngapi, hotuba tatu tofauti ni kidogo?

Hizo ndio zinaitwa mbiu za mgambo, warning signs, kwamba na yeye tutegemee akiwa Rais atuletee baadhi ya tabia za JPM. Amekengeuka, aache mara moja!
 
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano.

Alisema Rais huyu anafanya mambo yaliyokataliwa na waasisi wa nchi hii ya kujali kabila lake kwanza.

Na tumeshuhudia Rais huyu wa sasa akipanda majukwaani na kuweka mbele Kisukuma bila kuzingatia misingi ya kuendeleza Utaifa mmoja, unaoongea lugha ya Taifa moja, lugha ya Kiswahili.

Tundu Lissu, kati ya watu wote, na yeye eti ameangukia mtego huo wa kuongea cha kwao majukwaani. Anatuangusha.

Mwalimu Nyerere anaviringika kaburini.

Out of context
 
Tindikali sasa wewe ndio umewasha moto kwa wananchi juu ya nani anahusika na jaribio la mauaji ya Lissu, kumbe?!!! Lazima haki itendeke.
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano.

Alisema Rais huyu anafanya mambo yaliyokataliwa na waasisi wa nchi hii ya kujali kabila lake kwanza.

Na tumeshuhudia Rais huyu wa sasa akipanda majukwaani na kuweka mbele Kisukuma bila kuzingatia misingi ya kuendeleza Utaifa mmoja, unaoongea lugha ya Taifa moja, lugha ya Kiswahili.

Tundu Lissu, kati ya watu wote, na yeye eti ameangukia mtego huo wa kuongea cha kwao majukwaani. Anatuangusha.

Mwalimu Nyerere anaviringika kaburini.

Hapa ndio umeonesha vizuri nani aliehusika kumshambulia Tundu Lissu, hukumu yake ipo, na Mungu ndie hakimu wa kweli.
Kama unataka ufanye jambo zuri lolote hapa Tanzania basi jua huwezi kuwa wewe wa kwanza lazima alianza Magufuli na yeye ndio atamalizia ukweli ni kwamba siku zinavyo zidi kwenda Tundulisu ataendelea kutoka kwenye Ramani mdogo mdogo
Mleta mada hapo Tundu Lissu yupo jukwaani? Alafu umewai fika vijijini singida? Unadhani wanajua kiswahili? Basi umepotea sana!!!

Hapo Tundu Lissu watu wanamsalimia kwa kilugha chao unataka awajibu kiingereza? Unataka awajibu kiswahili?

CCM mmekosa hoja kabisa. Magufuli hasemwi tu kuongea kisukuma bali kwa nepotism yake anayoionesha wazi tena mchana kweupe kwa kuwapendelea watu wake!!!

Kama Tundu Lissu angekuwa Singida Mjini alafu anaongea kinyaturu hapo ungekuwa na hoja ila kwa huko vijijini hapo huna hoja yeyote!!

Lissu kuongea kilugha kijijini tena kwao hilo sio tatizo lolote ndugu!!
Kiukweli CCM kwa sasa mmezidiwa
Kumbuka juzi tu hapa kasema Tanzania kuna corona watu wengi wanapoza maisha kimyakimya, chakushangaza alikuwa anakumbatiana na watu bila woga hawa watu hawa zakuambia changanya na za kwako.
Siku ya kifo cha ccm miti yote uteleza
Umemtaja aliyemshambulia Mh. Lissu kama hizo ndiyo miongoni mwa sababu za shambulio like la kigaidi basi msiwasingizie watu wasiojulikana.Bebeni lawama zenu wenyewe.

Ikungi kuna Wazee wa Kinyaturu, wengine hawafahamu kiswahili,je unamlinganishaje na Ukabila wa Jiwe? Hawana ulinganifu wowote. Acha Rais Mtarajiwa asalimie Wazazi wake apendavyo, tunamfahamu kuwa hana tabia za Ukabila.Ukienda Kijijini kwenu unaongea English/ Kiswahili?
Kumbe ndio nyie mliomfanyia unyama ule!? Basi sawa!
 
Hongereni Mataga kwa kufuatilia kila anakopita Lissu,mpaka uchaguzi upite mtakuwa mmenyooka kisawasawa!
 
Kuongea kilugha si ukabila, wapo watanzania wengi sana wasiokijua kiswahili, hao hatuwezi kuwaita wabaguzi au wanaukabila.

Jakaya Kikwete hakuongea Kikwere. KAMWE!

Wala Mkapa. Wala Mwinyi. Wala Nyerere.

JPM ndio katuletea vilugha majukwaani. Tundu Lissu kamuiga JPM.
Tabia hizi za Lissu na JPM zipingwe na zikemewe.
 
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano.

Alisema Rais huyu anafanya mambo yaliyokataliwa na waasisi wa nchi hii ya kujali kabila lake kwanza.

Na tumeshuhudia Rais huyu wa sasa akipanda majukwaani na kuweka mbele Kisukuma bila kuzingatia misingi ya kuendeleza Utaifa mmoja, unaoongea lugha ya Taifa moja, lugha ya Kiswahili.

Tundu Lissu, kati ya watu wote, na yeye eti ameangukia mtego huo wa kuongea cha kwao majukwaani. Anatuangusha.

Mwalimu Nyerere anaviringika kaburini.

Delete ccm Oct 28
 
Kama unataka ufanye jambo zuri lolote hapa Tanzania basi jua huwezi kuwa wewe wa kwanza lazima alianza Magufuli na yeye ndio atamalizia ukweli ni kwamba siku zinavyo zidi kwenda Tundulisu ataendelea kutoka kwenye Ramani mdogo mdogo
Ni kweli mkuu, mh. Ndiye rais wa kwanza TiZiii! Ndiye aliyeomba uhuru wetu toka kwa mkoloni, ndiye mzee wa ruksa, ndiye mzee wa ‘ukweli na uwazi’, na ndiye mzee wa Msoga! Ndiye kila kitu, kila kitu kilianzia kwake!!😂😂😂! Wewe ni #kangilugolamtotowayesu!
 
Muda huu alitakiwa awe anazungumza lugha ya wafu.
Ila kama anaweza kuongea lugha yoyote ya walio hai basi tumshukuru Mungu.
 
Jambo nyeti la mwisho alilofanya Tundu Lissu kabla ya kupigwa risasi, na ambalo wachunguzi wengi wa kisiasa wamesema lilichangia kupangwa mashambulizi ya kigaidi dhidi yake, ni kutoa hotuba ile ya "Mtoto wa Dada," ambamo alishutumu vikali na kulaani kwa nguvu ukabila na undugu uliokuwa unaota mizizi ghafla kuanzia utawala wa awamu ya tano.

Alisema Rais huyu anafanya mambo yaliyokataliwa na waasisi wa nchi hii ya kujali kabila lake kwanza.

Na tumeshuhudia Rais huyu wa sasa akipanda majukwaani na kuweka mbele Kisukuma bila kuzingatia misingi ya kuendeleza Utaifa mmoja, unaoongea lugha ya Taifa moja, lugha ya Kiswahili.

Tundu Lissu, kati ya watu wote, na yeye eti ameangukia mtego huo wa kuongea cha kwao majukwaani. Anatuangusha.

Mwalimu Nyerere anaviringika kaburini.

JPM katili sana, ndiye aliyebariki shambulio la Lissu kuchapwa zile mvua za risasi. Muda ukifika tutaweka wazi kila kitu.
 
Jakaya Kikwete hakuongea Kikwere. KAMWE!

Wala Mkapa. Wala Mwinyi. Wala Nyerere.

JPM ndio katuletea vilugha majukwaani. Tundu Lissu kamuiga JPM.
Tabia hizi za Lissu na JPM zipingwe na zikemewe.

..kweli.

..pamoja na kuchombeza kilugha, TL alitakiwa atafsiri ktk lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

..nayasema hayo kwa kuzingatia kwamba wako watu[wageni wake] waliomsindikiza kama Salum Mwalimu, Susan Kiwanga, etc ambao hawazungumzi Kinyaturu.

..pia tukio zima lilikuwa linafuatiliwa kila pembe za Tanzania hivyo ni vizuri wafuatiliaje waelewe kila lililozungumzwa.
 
Jakaya Kikwete hakuongea Kikwere. KAMWE!

Wala Mkapa. Wala Mwinyi. Wala Nyerere.

JPM ndio katuletea vilugha majukwaani. Tundu Lissu kamuiga JPM.
Tabia hizi za Lissu na JPM zipingwe na zikemewe.
Nyerere kwenye hotuba: Mazi ga nyanza....Wakerewe.
 
Back
Top Bottom