Video: Vurugu zazuka Kinondoni baada ya raia kugoma mwenzao kuchukuliwa na Polisi wakihofia Polisi huyo kuwa mtekaji

Napata faraja kuona watu wameanza kufunguka akili.

Utaratibu wa Ukamataji uko wazi tangu hapo Mwanzo hakuna Raia anagoma kukanatwa na polisi.

Hawa wasiojulikana siku zote wanajiita asikari polisi.

Utoke Ukonga ukakamate mtu Kinondoni?
 
Sielewi CCM na Serikali strategy yao ni nini? Walitegemea baada ya watu kutekwa hivyo ingekuaje? Huyu jamaa angelazimisha naye angepigwa mawe hadi afe alafu ungesikia mapovu ya RC na IGP!!

Ni vizuri hatua zichukuliwe, kwani hao TISS kazi yao ni nini? Wanashindwaje kukamata hao watekaji wa Soka, Nondo, Sativa na mamia ya watoto wanaotekwa hovyo nchini!! Mbona hizi kelele zingeisha?

Hii nchi inatia sana hasira
 
KWa utaratibu ninaoujua mimi, mwanajeshi akina mtaani kwetu hata kama ni likizo ni lazima aende kwenye uongozi wa serikali za mtaa akaripoti na nafhani kuna fomu wanaijaza kisha wanatuma kazini kwao.
Polisi anakuja aeneo ambalo kuna uongozi tayari ambao ni Mjumbe wa nyumba kumi, Serikali ya mtaa, Serikali ya kitongoji, Diwani na wajumbe wengine wote, anawaruka bila kutoa taarifa ya uwepo wake kwa hawa wenye mamlaka kwa ngazi hizi za chini na kwenda moja kwa moja kumkamata mtu anayesadikiwa ni mtuhumiwa kweli?
Kwanini hawa watu waliopo serikalini hawapendi kufata sheria kama wanavyotaka sisi tufanye?
Ina maana hizi serikali za mitaa na vijiji viongozi wake ndio hawaheshimiki kiasi hiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…