Video: Vurugu zazuka Kinondoni baada ya raia kugoma mwenzao kuchukuliwa na Polisi wakihofia Polisi huyo kuwa mtekaji

Yaani ni hatari sana.
 
Ila mwisho wa siku wamembeba. Jamaa alikuwa anafurahia assist ya wananchi ilihali anajua kweli alizingua na ana kesi ya kujibu.

na
Ndivyo inavyotakiwa....tunapokataa matukio ya kutekana sio kwamba tunatetea uharifu.

Waharifu wataendelea kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa yao.
Hii ya kutekana ilitaka kuchukuliwa kama Loop Hole ya waharifu wa kwenye system.

Wanakulilua risasi wanaenda kulipoti kwamba ulitaka kupindua nchi. Imeisha hiyo
 
Hapo askari kapewa pesa ili aende kumkaamata jamaa bila kufuata utaratibu ndiyo maana yanawakuta mambo .

Watu wa aina hii ni kwenda nao kiulalo ulalo tu hakuna namna.
 
Hahaha nimewapenda jaman watu wa kinondoni hadi nawamejiridhisha ila hilo lijamaa linaonekana limepiga tukio kwa mtu kabisa haha
 
Sasa nasema, hawa wananchi ni wapole sana, tena wastaaarabu sana. Huyo "askari" alitakiwa ashughulikiwe ipasavyo, hadi somo lieleweke

Jamani, vipi, mbona bado tunakubali uzembe na upumbavu? Mtu mmoja anawasumbua umati mkubwa namna hii? Bado kuna tabia za nyumbu miongoni mwa jamii
 
Nchi imefika Patamu sana!
 

Haki inataka wajibu. Hakuna one way street kwenye haki. Eti kuamlisha tu halafu kila mtu akusikilize...ni kujidanganya?

Lakini pia tumefikaje hapa? Mbona hatukuwa na matatizo ya aina hii? Mbona waliyoyasababisha hawawajibiki wala kuwajibishwa?

Kila siku nikiona haya, au yale ya wanaisiasa wa upinzani, namkumbuka RTD IGP Harun Mahundi. Alimaliza pale na ikawa ndio kamaliza.

Jeshi letu hili bado tunalihitaji sana na kwa mustakabali mwema wa nchi yetu, lazima lijifunze kukaa karibu na wananchi na kufanya nao kazi kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Kujidanganya kila kitu tunakiweza bila kushirikiana ni kujitafutia majanga. We all need each other
 
Wananchi baada ya kuona tukio hilo, walimzingira Polisi huyo na kuanza kumuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kwanini hajavaa nguo za kiaskari, kwanini hana gari la Polisi, kama yeye ni Polisi kutoka Ukonga kwanini anakuja Kinondoni kukamata
 
Niliwahi kutuma post humu kuwa Black Mamba ana sumu kali sana lakini hapendi kuitumia isipokuwa uhai wake unapokuwa mashakani, tuwe makini jamani black mamba ( wananchi) ameanza kuitumia sumu yake kulinda uhai wake.
 
Wananchi baada ya kuona tukio hilo, walimzingira Polisi huyo na kuanza kumuuliza maswali mbalimbali ikiwemo kwanini hajavaa nguo za kiaskari, kwanini hana gari la Polisi, kama yeye ni Polisi kutoka Ukonga kwanini anakuja Kinondoni kukamata
Wazembe kabisa. Akili za Watanzania bado zimekaa kinyumbu nyumbu sana. Tukichukua hatua madhubuti sisi wenyewe Wananchi, hakuna mtu wa kutushinda. Hata waje na vifaru lakini mwishowe watashindwa tu.
 
Maneno ya Mzee Warioba watu wengine wanayachukulia poa tu lakini yana uzito mkubwa sana.

Tunajiona tuko special sana kwamba hii erosion of trust and national unity haiwezi kutuharibia nchi, we are not that special.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…