Coach Slamah Hamad
JF-Expert Member
- Nov 12, 2014
- 3,740
- 4,938
Ana hoja kubwa. Pia uthubutu mkubwa sana.
Lakini….
Kusema hotuba ya Rais ilikua ni Mipasho tu hakuna content inaondoa ustaarabu katika hoja yake, tukosoane kwa staha.
Kuhusu Bandari kasema Ukweli ila kauweka general sana kiasi ikiwa anasikilizwa yeye kwanza ili kufanya maamuzi basi atawapoteza wengi. Uwekezaji bandarini sio Tatizo, tatizo ni masharti na makubaliano ya huo uwekezaji.
Elimu ya Katiba ya sasa ni muhimu pia sio mbaya japo timing kwa upande wa serikali ni mbovu.
Watanzania waliokua na umri wa miaka 10 Mwaka 2014 wakati wa mchakato wa Katiba Mpya na ukusanyaji maoni hawakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi wala kupiga kura. Leo hii watu hao wanamiaka 19 umri sahihi wa kuifahamu kiundani Katiba ya sasa na pia ndio umri sahihi wa kufanya maamuzi na kupiga kura.
Na hapo kwenye Katiba, tuwe wakweli, hii iliyopo sasa inavunjwa na kukanyagwa kila kukicha ni kipi cha maana kimewahi kufanyika?
Somo la Katiba ya nchi halipo mashuleni wala kwenye jamii zetu, asilimia karibu 50 ya watanzania hawaelewi haki na hawatambui wajibu wao.
Tatizo ni kwamba elimu waliyosema wataitoa kwa wananchi kwa miaka 3 inawezekana isitolewe na watu wakapiga pesa za project na uchaguzi ukapita na tukaendelea pale pale tulipokua.
Kwanini vyama vya upinzani navyo visiungane na hii kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu Katiba ya sasa, Haki na Wajibu wao kwao binafsi na Taifa ili kuwapigania kwa vitendo watanzania?
Kwenye hizo kamati zao za maridhiano kwanini wasiridhiane kushirikiana kuelimisha ummah kuhusu Katiba na hilo fungu la project waligawane pamoja?
Maana Kama wote nia ni moja hata Muda wa kusambaza hiyo elimu utapungua to a half maana nguvu kazi itakua kubwa na watamaliza mapema zaidi.
Baada ya hapo wamuachie mtanzania kuamua baada ya kuelimishwa na pande zote, Serikali na Vyama vya Upinzani.
Ama lazima tuwe tofauti kwa kila jambo?