Video ya kuogofya: Jambazi alivyopigwa risasi shingoni wakati alipovamia benki.

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
CCTV Crime News

Your browser is not able to display this video.


Mwisho wa Video ya pili utamuona namna alivyoingia benki kama mlemavu vile.

Your browser is not able to display this video.

................

Hii ilikuwa San Mateo, huko Maranhao, Brazil na huyu ndiye mhusika lakini alikufa.
Jina ni: Nilton César Silva Aguiar.


....
Hapa aliingia Benki kama mlemavu


.....
Hili hapa pigo la kwanza, askari alipigwa risasi ya kifua, bahati nzuri askari alikua amevalia bulletproof ya kuzuia risasi, hivyo haikumpiga


....
Pigo la pili, askari alirudisha mapigo na kumpiga jambazi sehemu ya kifua.


................
Baada ya jambazi kupigwa ya kifua akainama kisha akapigwa nyingine ya shingo


........
Jambazi kipindi anapiga alikua akimsogelea askari, ndipo askari akainama chini ya meza ili afanye counter kumzungukia kwa nyuma, lakini jambazi lilisogea hadi usawa wa meza na likampiga askari risasi ya uti wa mgongo ili kumpa-paralysis. Ambapo hata hivyo haikumpata ila ilimchubua mkono wa kushoto.



Jambazi alifia mlangoni kwa kuvuja damu shingoni. Baada ya jambazi kudondoka utawaona wahudumu wa benk wakikimbilia ndani na mlinzi akirudi ulingoni. Kwa hivyo Hakufa wala kujeruhika mtu, ispokua mlinzi ilimchuna mkono wa kushoto.
....
Jambazi alifanikiwa kukwepa hatua za usalama za benki kwa kutumia sahani ya chuma kwenye mguu wake kama mlemavu wa mguu wa kushoto ili kuweza kuingia ndani na bunduki bila kulazimika kupitia mlango mkuu wa ukaguzi.
 
Kama muvi aisee

Uhalifu umelipa hapo
 
Response ya Mlinzi ilikua very fast,
kilichomsaidia ni kuwa at the right place with right tools and Right Mind, najaribu kuimagine hawa walinzi Bongo Darisalaam unamkuta kabeba kirungu, filimbi na smartphone kubwa anaangalia tiktok tungetoboa kweli ?
 
Kama movie vile.Hivi kwanini inapotumika neno jambazi inatamkwa "li" au "hayo"
Mfano; Jambazi hilo sugu alikamatwa....
Au
Majambazi hayo yalitokomea....

Kwanini sio jambazi huyo au hao? 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…