Sema askari alikuwa na bastola, angekuwa na mjegejo ilikuwa ni kumimina tu.
Hio risasi shingoni ilipasua artery, jamaa damu inaruka kama bomba.
Ni jambo la kusikitisha sana mtu anapokufa akiwa katika harakati za kufanya dhambi, na hajapata hata nafasi ya kutubu ili afe katika Bwana.
Ufunuo 14:13 inasema:
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Ukifa, matendo yale uliyokuwa nayo kabla ya kufa, ambayo haukuyatubia, utaenda nayo, meaning, ndio utaenda kuhukumiwa nayo. Imagine mfano, hapo ameishi miaka mingi yenye opportunity ya kumrudia Mungu, hajatumia opportunity hizo, akaja kufa kibudu tuhivyo.
tumeshuhudia pia watu wengi wakifa guest house wakati wakifanya uzinzi, wengine wanauana wakigombea mwanamke, wengine wanakufa na ajali wakitokea kwa hawara, wengine wanakufa wakitoka kwa mganga wa kienyeji, wengine wametumia utajiri wa ndagu na shetani anakuja kuwavuna kabla hata hawajaacha uchawi wakarudi kwa Mungu. hao wote ni moja kwa moja motoni, sawasawa na wewe unayejifanya mkaidi, hujui utakufa lini ndugu, maisha hayo uliyo nayo ni opportunity Mungu amekupa ili pengine ubadilishe maisha yako, tengeneza na Mungu wako, nafasi hizo inaweza isiwepo.
msiwasikilize mapadre na wachungaji wanaowaaminisha kwamba hata msipookoka, mkifa wataziombea maiti zenu zikasamehewa huko huko mliko,
ndio maana huwa mnaombea wafu, mnaombea wazazi wenu waliokufa, mnafikiri watasamehewa, Noo, wameenda na matendo yao kwenda kuhukumiwa huko, baada ya kifo ni hukumu, hakuna kutubu au kusamehewa tena. wengi wanang'ang'ania hadi dini zenye mapokeo ya kishetani wakiogopa kuwa wakiondoka huko wasije kukosa mtu wa kuwaombea wakifa ili wasamehewe, ingelikuwa hivyo ndio ukweli,
Biblia isingesema mtu ataenda na matendo yake, na kutubu kusingehubiriwa kwasababu kuna haja gani kutubu wakati ukifa kungekuwa na nafasi ya ndugu zako kukuombea ukasamehewa baada ya kufa? hivi mnanielewa kweli katika hili? mapokeo ya dini yamekuja kuwajaza shingo ngumu na upofu ili msiokoke kabisa, kwa kigezo kwamba mkifa wao ndio wameshikilia uzima wenu wa milele, wawataombea msamehewe mikiwa maiti: kweli? hata Yesu alipoeleza mfano wa tajiri na lazaro, alisema kama hawatawasikiliza waliko hukohuko duniani....basi tena.
msidanganywe, shetani wa dini zenu ni mwongo sana, msibahatishe maisha, msifanye betting kwenye maisha yenu, msije enda motoni siku ile mkaona haya tunayaongea yalikuwa ni ya kweli kweli, tengenezeni mambo yenu na Mungu, ili muwe tayari. Mungu asawaidie.