Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Believe me, wewe hapo ulipo tuchukulie nikupe ndawa ya kuwaona wangaa,huwezi waonona wakiyeyuka tena maana hapo inakuwa ni live,
Tuanze na wewe, umewahi kutumia dawa ya kuwaona hao wanga??

Na kama uliwahi kuitumia uliajuaje kwamba ni ya ukweli na sio kilevi cha kukufanya uone kile akili inachotaka kuona??
 
Hiyo video imerekodiwa na simu wakati jamaa ana kagua matukio (video preview) ya picha kwenye camera alizofunga hapo ndipo atakutana na hilo tukio.

Kwa kifupi hizo ni video mbili kwa nyakati tofauti mfano "mtu anaangalia mpira kwenye TV halafu anachukua simu na kurekodi kipande cha tukio la mpira kama sehemu ya kumbukumbu ama kubishana na wenzake, hapo lazima kutakuwepo na sauti zingine nje ya sauti halisi ya TV, hata kama mtu akitukana itasikika tu na haitamaanisha hilo tukio sio la kweli eti kisa kuna sauti zisizohusika na tukio ama kucheza kwa picha hakutomaanisha hilo tukio sio la kweli maana atakuwa ameshika simu kwa mikono.

Hilo tukio ni la kweli na nijuavyo mimi Tekinolojia huwa haisemi uongo.
Ogopa sana tekinolojia popote pale ilipo na wewe ukawepo.
 
Hakuna kitu kama hicho. Ni uongo wa wazi na ujinga.

Hapo wauza CCTV Camera wametengeneza tukio wapige hela.

Kwanza Hakuna uchawi wala ulogi, ni ujinga tu wa watu.
 
Nimeiona hii video ya tukio lililotplea tarehe 4 ikimuonesha mchawi akiwanga, pia anaonekana live anapotea

teknolojia ya ku edit nayo imekuwa sana siwezi kuamini moja kwa moja
Editing, tena imefanywa na layman tu.

Angalia hapo mahala mchawi anapotokea, kuna kama layer hivi inaziba na inacheza cheza then ndio anatokea. Halafu kuna effect kabisa ya kutokea japo wakati anaondoka wametoa tu frame bila kurudia ile effect.

Pili hio monitor bei yake mbaya sidhani kama kuna mtu anatumia kwa ajili ya display ya camera, hiyo ni monitor ya mtu anae edit video.
 
Kwakweli mimi nawahitaji sana wachawi na uchawi wao!

Niliwahi kwenda mpaka Pemba kule ndani ndani ili nipate walau hata uchawi wa kiislamu, lakini hakuna nilichopata.
Nikamtafuta mshana jr, badala anipe mwongozo wa kuupata huo uchawi, akawa ananiletea stori za kusema "mara ooh uchawi ni utumwa, mara hivi, mara vile"
Kwa ufupi akawa analeta uswahili.
Mpaka sasa nimeamua kutulia tu kama namba moja.
Nimepoteza matumaini ya kupata uchawi.
Nb, mimi ni mtu wa kigoma.
Khaaak...[emoji23]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Editing, tena imefanywa na layman tu.

Angalia hapo mahala mchawi anapotokea, kuna kama layer hivi inaziba na inacheza cheza then ndio anatokea. Halafu kuna effect kabisa ya kutokea japo wakati anaondoka wametoa tu frame bila kurudia ile effect.

Pili hio monitor bei yake mbaya sidhani kama kuna mtu anatumia kwa ajili ya display ya camera, hiyo ni monitor ya mtu anae edit video.
Kama Chief umenena ni nani wa kukubishia mkuu!
 
Nimeiona hii video ya tukio lililotplea tarehe 4 ikimuonesha mchawi akiwanga, pia anaonekana live anapotea

teknolojia ya ku edit nayo imekuwa sana siwezi kuamini moja kwa moja

Najua uchawi upo maana nimewahi kukaa mitaa ambayo ikifika usiku kuna fujo zao zinafanya wengi walale kw wasiwasi ikiwemo kukimbia juu ya dari, mchanga kumwagwa kwenye bati, n,k. nilikosa ujasiri niliacha kodi.

uchawi upo lakin hii video ni kweli au?

Mshana Jr

hadi sasa nimewaza vitu kadhaa ila bado havina uzito

- kamera kucheza cheza - cctv hua haitikisiki lakini katika hii video inatikisika ni kwasababu imerekodiwa kwenye kioo cha computer kwa kutumia simu.

- muda ni saa 11 jioni lakini kuna giza - muda huo wa kwenye cctv unaweza ukawa haujasetiwa kuendana na muda halisi, huenda hakupatikana mtaalam anaejua kuseti muda, licha ya hivyo bado haizuii cctv kurekodi video, huenda muda halisi ni usiku wa manane na hata taa tumezoa kuwasha usiku na sio jioni.

View attachment 2009151
Mshanaaaa Jr
 
Familia iliyorekodi tukio IPO na imenithibitishia tukio hilo kuwa lipo kweli na hiyo kumbukumbu IPO kwenye Camera zao. Ni Tabata Kisukuru
 
Wangapi wenu washaona cctv camera inayotoa sauti yani inarecord audio na video????

Halafu huyu mchawi mbona kavaa nguo nyeupe wakati tunajua fika anatakiwa awe uchi au ajifunike na matambala meusi na mekundu!!!
 
Kwakweli mimi nawahitaji sana wachawi na uchawi wao!

Niliwahi kwenda mpaka Pemba kule ndani ndani ili nipate walau hata uchawi wa kiislamu, lakini hakuna nilichopata.
Nikamtafuta mshana jr, badala anipe mwongozo wa kuupata huo uchawi, akawa ananiletea stori za kusema "mara ooh uchawi ni utumwa, mara hivi, mara vile"
Kwa ufupi akawa analeta uswahili.
Mpaka sasa nimeamua kutulia tu kama namba moja.
Nimepoteza matumaini ya kupata uchawi.
Nb, mimi ni mtu wa kigoma.
Kwenye Uislamu uchawi hauruhusiwi jpo kua wapo waislamu wanofanya ayo mambo ila jirekebishe kuita uchawi wa kiislamu
 
Wangapi wenu washaona cctv camera inayotoa sauti yani inarecord audio na video????

Halafu huyu mchawi mbona kavaa nguo nyeupe wakati tunajua fika anatakiwa awe uchi au ajifunike na matambala meusi na mekundu!!!
Alitakiwa aseme mwanga na si mchawi tofauti yao ya haraka mmoja hufanya shughuli zake akiwa na nguo na mwingine hufanya akiwa mtupu

Sent from my SM-N920P using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom