Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Ile ilikuwa live kabisa na ilinaswa kwenye security camera... Kusema ile ni edition sidhani.. Ninachoweza kusema ni kwamba lile halikutokea hapa kwetu na pengine sio tukio jipya
 
Nikamtafuta mshana jr, badala anipe mwongozo wa kuupata huo uchawi, akawa ananiletea stori za kusema "mara ooh uchawi ni utumwa, mara hivi, mara vile".

Kwa ufupi akawa analeta uswahili.
 
Baada ya maelezo haya,naomba Jaji wa JF anayesikiliza hii aufunge rasmi.
 
Mwingine huyu
Your browser is not able to display this video.
 
@Scars
Bufa
 
@Scars
Bufa
 

Mkuu bora wewe, mimi niliomba jina tu sikupewa hadi leo na niliahidi kutoa 500,000 TSH kwa yeyote atayenipa jina tu.

Mtu alianzisha uzi kwamba kuna diwani huko huko Kigoma alifariki kisha akafufuka na mitanganyika sababu mingi ni mizwazwa ikaamini ile story kama ilivyo kama kwenye uzi huu tu. Sababu diwani ni ofisi ya umma na info zao zipo wazi mimi nikaomba jina tu la huyo diwani huwezi amini nilipigwa chenga hadi leo sijapata hilo jina. Sababu wewe ni mkigoma labda umewahi kusikia huu mkasa.

 
Huu ni ujinga!... labda nirudie tena kama hujasikia vizuri HUU NI UJINGA!

Hakuna siku utaona mchawi au jini au malaika katika umbile lake halisi halafu ukaweza kumchukua sauti picha wala video

Niliona clip fulani tena eti farasi mweupe anakimbia angani halafu watu shazi wanashuhudia na kelele nyingiiii kama kweli vile. Ni ujinga mtupu kuamini maigizo kama yalivyo maigizo ya kina Jet Li
 
kwa taarifa nilizozipata inasemekana kuwa ni kweli na hilo tukio lilichukuliwa kupitia mfumo wa cctv na limetokea kwa tajiri mmoja huko kigoma...na kuhusu hizo sauti ni kwamba hiyo video imechukuliwa kwa simu ikiwa imeelekezwa kwenye display ya computer.
 
Hii inaweza kuwa sahihi zaidi wanaosema ni editing labda hawajaiangalia vizuri
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu, kigoma kwenyewe kila mtu anasema "nasikia kuna mtu alikuwa hivi au vile"
Kuna mambo yako hivi au vile, cha ajabu huyo anayeongea, unakuta nayeye alisikia tu.

Kuna eneo fulani pale kijijini kwetu, ilikuwa inasemekana huwa inapita treni nyakati za usiku wa saa saba mpaka saa tisa.
Na wakawa wanasema hiyo treni huwa inatoa misukule burundi na kongo.
kijijini kwetu hakuna reli ya kupitisha treni, nikajisemea, "mimi nitaenda hilo eneo kuiangalia hiyo treni yenye misukule"
Kwakweli nilifululiza kama wiki hivi eneo lile nyakati za usiku wa manane na sikuiona hiyo treni.
 
Hakuna cctv inayoweza "kukamata" picha za "ulimwengu wa roho" Vitu vya ulimwengu wa roho VIPO KABISA lakini macho ya nyama (macho ya kawaida) hayawezi kuviona.

Kwa maana hiyo, cctv ambayo inachukua picha za vitu vinavyoonekana kwa macho ya nyama haiwezi kukamata picha ya vitu vya ulimwengu wa roho.

Kwani wewe umeshawahi kuona kwa macho yako wachawi wakiwanga? Lakini si wapo?
 
Mimi nimeshawahi kuona kwa macho yangu hayahaya ya nyama.

 
Usisingizid tabia zako za kuhonga wanawake na kunywa pombe useme uchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…