Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Video ya mchawi/mwanga aliyekamatwa akiwanga ina ukweli?

Hiyo sinema siyo ya kweli kwa mantiki hii hapa.

a) kwenye sekunde ya 00.06.38 kuna effect ya fade in imechelewa kuapply, yaani huyo 'sijui' mchawi anaonekana ameshatua badala ya kutua kwa mfumo wa kutoka juu na hiyo bombadier yake.

Na kwenye kuruka pia alitakiwa aonekane anapotea kwa kupaa not kutoweka.

Hiyo ni man made video, ukitaka kuona real video za wachawi kule YouTube zipo nyingi tu.
 
Kwakweli mimi nawahitaji sana wachawi na uchawi wao!

Niliwahi kwenda mpaka Pemba kule ndani ndani ili nipate walau hata uchawi wa kiislamu, lakini hakuna nilichopata.
Nikamtafuta mshana jr, badala anipe mwongozo wa kuupata huo uchawi, akawa ananiletea stori za kusema "mara ooh uchawi ni utumwa, mara hivi, mara vile"
Kwa ufupi akawa analeta uswahili.
Mpaka sasa nimeamua kutulia tu kama namba moja.
Nimepoteza matumaini ya kupata uchawi.
Nb, mimi ni mtu wa kigoma.
Hapo kwa mshana sasa
 
Ni bongo movie hii[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Very true
Tulikatazwa tukiwa wadogo kuamini na mpaka sasa sijawahi kuona kama una nguvu yoyote kwangu
Sisi wengine tumerogwa tangu hatujazaliwa hadi leo still tunarogwa na mambo yanaenda atujaathirika.
Mimi nguvu yeyeto ya kiumbe ikinijia usiku huwa na sensi kuna mchawi nilimkosa ngumi akawahi yeyeyuka wapumbavu Sana hawa takataka.
 
Nimeifatilia kwa umakini Sana hii video,lakini sioni uhalisia wake kwa kutumia vigezo vifuatavyo:-

1. Uchawi una kanuni na mashariti mengi sana,moja yawo ya mashariti ya uchawi ni kuwanga huku ukiwa uchi/ nusu uchi hii ikiwa ni Dhana ya kwamba uchawi hufanyika katika ulimwengu ambao unahitaji nguvu ya ziada kuuona au kuwaona wachawi,sasa Kama huyo kwenye video ni mchawi ,alivaa nguo za nini Wakati wachawi hawaonekani kwa macho ya nyama,alikuwa anamwogopa nani?, Hivyo naweza hitimisha kuwa hii video sio sahihi kwa kuzingatia vigezo vya uchawi, unless Uwe uchawi wa Pwani na ughaibuni,lakini in most cases uchawi hufanywa kwa watu( wahusika) kuwa watupu.

2.Nimeshindwa kutambua ikiwa Wakati huyo mtu anafanya huo uchawi kulikuwa na mtu anamrecodi pembeni au Ni uwezo wa CCTV-Camera kuona yaliyo sirini,na Kama Ni uwezo wa CCTV-Camera kwanini Kuna Wakati anapotea huyo mchawi na CCTV-Camera inashindwa kutuonesha namna anavyopotea Wakati zoezi zima linaonesha huyo mchawi anafanya uchawi wake pasina kuonekana ila CCTV imeweza kumnasa,Basi ilipaswa hiyo CCTV ituoneshe na namna anavyopotea!!

Haya ni maigizo !!!
Huyu mchawi mstaarabu hataki kuwa uchi
 
Naona huyu ndio yule anaechoma magodoro na kugeuka chui
Kweli uchawi upo ila mimi siuamini
Mimi nilikuwa kama wewe, nikawa siamini kabisa,nilikuwa vizuri kiasi kiuchumi, nilivohamia kwangu ndani ya miezi miwili tu nikajipambanua zaidi kumbe sijui binadamu anawaza nini, siku moja nimeamka wakati tupo kwenye ziara ya jumuiya asubuhi na viongozi wenzangu ndo wananishtua mbona kichwani huna nywele (pande mbili za kichwa zilikuwa zimenyolewa haswa maana nilikuwa na nywele ndefu) nilidharau tu, nikaenda nikanyoa nywele zote zimeanza tu kuota nikanyolewa tena baada ya hapo maisha yangu yakawa ni historia maana hata nguo za kuvaa zilinishia. Sikuwahi kuwa na hata akiba ya elf tano ndani.,nilipitia mapito ijapo nilikuwa napata miamala kupitia send waves lakini sikufanya cha maana hata kidogo, aiseee usiombe
 
Sisi wengine tumerogwa tangu hatujazaliwa hadi leo still tunarogwa na mambo yanaenda atujaathirika.
Mimi nguvu yeyeto ya kiumbe ikinijia usiku huwa na sensi kuna mchawi nilimkosa ngumi akawahi yeyeyuka wapumbavu Sana hawa takataka.

Duu pole sana
Kila mmoja wetu amejaribiwa kwa namna moja au nyingine
Nakumbuka nyumbani siku moja ndugu yangu alijikwaa mlangoni kuja kuangalia wamezika chupa yenye matakataka na manyoa na vitu kibao

Ila father aliifukua na kwenda kuitupa jalalani akasema wapumbavu hao wanajisumbua tu msiamini haya mambo

Ila kama wanakujaribu kila wakati ni mtihani
 
Mimi nilikuwa kama wewe, nikawa siamini kabisa,nilikuwa vizuri kiasi kiuchumi, nilivohamia kwangu ndani ya miezi miwili tu nikajipambanua zaidi kumbe sijui binadamu anawaza nini, siku moja nimeamka wakati tupo kwenye ziara ya jumuiya asubuhi na viongozi wenzangu ndo wananishtua mbona kichwani huna nywele (pande mbili za kichwa zilikuwa zimenyolewa haswa maana nilikuwa na nywele ndefu) nilidharau tu, nikaenda nikanyoa nywele zote zimeanza tu kuota nikanyolewa tena baada ya hapo maisha yangu yakawa ni historia maana hata nguo za kuvaa zilinishia. Sikuwahi kuwa na hata akiba ya elf tano ndani.,nilipitia mapito ijapo nilikuwa napata miamala kupitia send waves lakini sikufanya cha maana hata kidogo, aiseee usiombe
True,pia kama maisha huwa kuna kupanda na kushuka, wakati mwingine unaona kabisa kama Mungu kakuacha na wakati mwingine unaona kama Mungu kakupendelea hasa pale mambo yako yanapokwenda safi.
 
Kwakweli mimi nawahitaji sana wachawi na uchawi wao!

Niliwahi kwenda mpaka Pemba kule ndani ndani ili nipate walau hata uchawi wa kiislamu, lakini hakuna nilichopata.
Nikamtafuta mshana jr, badala anipe mwongozo wa kuupata huo uchawi, akawa ananiletea stori za kusema "mara ooh uchawi ni utumwa, mara hivi, mara vile"
Kwa ufupi akawa analeta uswahili.
Mpaka sasa nimeamua kutulia tu kama namba moja.
Nimepoteza matumaini ya kupata uchawi.
Nb, mimi ni mtu wa kigoma.
We mrundi acha ujinga hamna uchawi wa kiislam

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Nimeiona hii video ya tukio lililotplea tarehe 4 ikimuonesha mchawi akiwanga, pia anaonekana live anapotea

Teknolojia ya ku edit nayo imekuwa sana siwezi kuamini moja kwa moja

Najua uchawi upo maana nimewahi kukaa mitaa ambayo ikifika usiku kuna fujo zao zinafanya wengi walale kw wasiwasi ikiwemo kukimbia juu ya dari, mchanga kumwagwa kwenye bati, n,k. nilikosa ujasiri niliacha kodi.

uchawi upo lakin hii video ni kweli au?

Mshana Jr

hadi sasa nimewaza vitu kadhaa ila bado havina uzito

- Kamera kucheza cheza - cctv huwa haitikisiki lakini katika hii video inatikisika ni kwasababu imerekodiwa kwenye kioo cha computer kwa kutumia simu.

- muda ni saa 11 jioni lakini kuna giza - muda huo wa kwenye cctv unaweza ukawa haujasetiwa kuendana na muda halisi, huenda hakupatikana mtaalam anaejua kuseti muda, licha ya hivyo bado haizuii cctv kurekodi video, huenda muda halisi ni usiku wa manane na hata taa tumezoa kuwasha usiku na sio jioni.

View attachment 2009151
hakuna mchawi huwa anaonekana ukimpiga picha, huo ni uongo wa mchana. mchawi anakuja kiroho wewe upige picha kimwili au cctv camera hizo sio za kiroho ndio zimpige mchawi? mtadanganywa hadi lini, hapo kuna mganga wa kienyeji anatafuta biashara watu wamfuate tu hakuna lolote.
 
Mimi nilikuwa kama wewe, nikawa siamini kabisa,nilikuwa vizuri kiasi kiuchumi, nilivohamia kwangu ndani ya miezi miwili tu nikajipambanua zaidi kumbe sijui binadamu anawaza nini, siku moja nimeamka wakati tupo kwenye ziara ya jumuiya asubuhi na viongozi wenzangu ndo wananishtua mbona kichwani huna nywele (pande mbili za kichwa zilikuwa zimenyolewa haswa maana nilikuwa na nywele ndefu) nilidharau tu, nikaenda nikanyoa nywele zote zimeanza tu kuota nikanyolewa tena baada ya hapo maisha yangu yakawa ni historia maana hata nguo za kuvaa zilinishia. Sikuwahi kuwa na hata akiba ya elf tano ndani.,nilipitia mapito ijapo nilikuwa napata miamala kupitia send waves lakini sikufanya cha maana hata kidogo, aiseee usiombe

Pole sana aisee najua haya mambo yapo ila mimi yamenipitia mbali sana namshukuru Mungu
Tukijua huyo ana mambo ya ushirikina tulikuwa tunawapiga mawe na kuwaita majina ya kila aina tulipokuwa wadogo na bahati hawakuwa wanatudhuru sujui kwa sababu ya utoto

Vipi uliponaje baada ya hapo?
 
Na ni Islamic sio Kwa kuswal kule

Sent using Jamii Forums mobile app
mbona una chuki na Uislamu ww
Ivi unafikiri ukiwa na chuki zako na uislamu unadhani kwamba Uislamu hautoendelea?
Yni heshimu dini za watu uspende kukurupuka
As a Muslim sipendi kuona Dini yangu ikichafuliwa na watu wajinga wajinga tuu
 
Back
Top Bottom