Video ya Paul Makonda msibani kwa baba yake GSM yazua gumzo jijini Dar

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ila jamani nyie ! usiombee watu wakupuuze aiseee! yaani Makonda ameshiriki msiba utadhani kaingia Dar jana kutoka Kolomije , yaani watu hata kumpa salamu hakuna kabisa! hii si sawa kabisa, Ama kweli Cheo ni kama koti la kuazima .

Nadhani sasai ile karatasi ya kuitwa Mahakamani amekwishakabidhiwa

======

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ni miongoni mwa watu maarufu walioshiriki katika mazishi ya baba mzazi wa mmiliki wa Kampuni ya GSM, Ghalib.

Makonda alijitokeza katika Msikiti wa Maamur Upanga, jana Machi Mosi, 2022 ambapo ndipo mwili wa baba wa GSM uliposwaliwa.

Marehemu alizikwa jana hiyohiyo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Kusambaa kwa video hiyo kumesababisha gumzo mitandaoni ambapo watu wengi wametoa maoni hasa kwa kuwa Makonda anaonekana akiwa kama raia wa kawaida bila kuwa na walinzi wala msafara kama ilivyokuwa zamani!

Your browser is not able to display this video.


Source: Global TV
 
Ila jamani nyie ! usiombee watu wakupuuze aiseee !! yaani Makonda ameshiriki msiba utadhani kaingia Dar jana kutoka Kolomije , yaani watu hata kumpa salamu hakuna kabisa ! hii si sawa kabisa , Ama kweli Cheo ni kama koti la kuazima...

Tatizo wabongo wengi tumezoea kuwapa watu heshima kwa vyeo, muonekano, hali ya maisha mfano tajiri, elimu nk.
Kwahiyo mtu akiwa hana hivyo vitu au hali tunamchukulia kawaida sana. Hili ni tatizo!
 
Kenge we! Yaani mnataka kuingiza siasa kila sehemu? Idiot
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…