Video ya Rais wa Sudan Kusini akitokwa na haja ndogo yazua maswali kuhusu afya za viongozi

Video ya Rais wa Sudan Kusini akitokwa na haja ndogo yazua maswali kuhusu afya za viongozi

Katika tukio lisilo la kawaida, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mwenye miaka 71 ameonekana akitokwa na haja ndogo wakati wa hafla ya Kitaifa na wimbo wa Taifa ukipigwa. Kitendo hicho kinaibua maswali kuhusu hali za kiafya za viongozi wengi duniani kuendelea kukaa madarakani hata baada ya umri wao kuwa mkubwa na wengine wakiwa na afya zisizoridhisha.

Mwaka huu 2022, pia mgombea wa Urais nchini Nigeria Bola Ahmed Adekunle Tinubu mwenye miaka 70 alionekana akiwa na mfuko maalumu wa kuhifadhia mkojo wakati wa mchakato wa kuanza kampeni hali iliyopelekea wananchi kuhoji kuhusu afya yake na majukumu anayotaka kugombea.

... sasa huyu ndio ka-demonstrate lively and vividly; sio Lowassa alisingiziwa na wabaya wake!
 
Nimeshindwa kuangalia video mara mbili. Ni fedheha kubwa sana, alipojiangalia sasa. Nami najiuliza hilo swali aliondokaje?
Ama walinzi walimzingira, kama kumficha?
... kwa jinsi ubongo wake ulivyokosa connection na viungo vingine including vya haja, the first sign aliyohisi ni joto kuongezeka miguuni ghafla ndio akawa anajitazama kuna nini. Hakujua lile joto limetoka mwilini mwake mwenyewe.
 
Hio video ilitakiwa kudhibitiwa haraka iwezekanavyo kutoka kwenye eneo la tukio ili kumtunzia mhusika heshima yake.
Na yeyote ambaye alithubutu kuisambaza video hyo alitakiwa kuchukuliwa hatua Kali za kisheria ili iwe funzo kwa wengine.

Ila hii fedheha nayo Ni mojawapo ya madhara ya tamaa za Madaraka na mamlaka.
 
Kuna watu wanapenda ku ng'ang'ania madaraka

Unakuta umri ushaenda ila yeye yumo, afya ni mgogoro yeye yumo

Hatu huyu wakwetu SAA 100 mwaka 2025 apumzike tu, kwani mpaka kufikia Januari 27 mwaka 2025 atakuwa na miaka 65 ukiongeza na miaka 5 ya awamu ya pili anayo ing'ang'ania kuwa atagombea atatoka akiwa na miaka 70

Na pia kama sasa nchi ni ngumu kwake ndo ataiweza kweli katika umri wa miaka 65 hadi 70 (umri wa ubibi)
Umri sio hoja sana kama katiba inaruhusu, na hii sio hapa Tanzania tu hata kwenye nchi zilizoendelea wapo viongozi wenye umri wa zaidi ya miaka 70, hoja ni afya njema.
 
Katika tukio lisilo la kawaida, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mwenye miaka 71 ameonekana akitokwa na haja ndogo wakati wa hafla ya Kitaifa na wimbo wa Taifa ukipigwa. Kitendo hicho kinaibua maswali kuhusu hali za kiafya za viongozi wengi duniani kuendelea kukaa madarakani hata baada ya umri wao kuwa mkubwa na wengine wakiwa na afya zisizoridhisha.

Mwaka huu 2022, pia mgombea wa Urais nchini Nigeria Bola Ahmed Adekunle Tinubu mwenye miaka 70 alionekana akiwa na mfuko maalumu wa kuhifadhia mkojo wakati wa mchakato wa kuanza kampeni hali iliyopelekea wananchi kuhoji kuhusu afya yake na majukumu anayotaka kugombea.

Siyo mambo ya vipapai kweli??? Maana hata yeye kashangaa
 
... kwa jinsi ubongo wake ulivyokosa connection na viungo vingine including vya haja, the first sign aliyohisi ni joto kuongezeka miguuni ghafla ndio akawa anajitazama kuna nini. Hakujua lile joto limetoka mwilini mwake mwenyewe.
Alihisi kamwagiwa maji ya moto....
Hivi si wanavaaga ....kifuani wamesahau.......wamvalishe pia
 
Back
Top Bottom