Video ya Rais wa Sudan Kusini akitokwa na haja ndogo yazua maswali kuhusu afya za viongozi

Video ya Rais wa Sudan Kusini akitokwa na haja ndogo yazua maswali kuhusu afya za viongozi

Mimi ni muisilamu wa Jumuiyya ya Ahmadiyya, Jumuiya ya Ahmadiyya imeanzishwa kwa amri ya Mungu na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) mwaka 1889, Yeye alizaliwa katika kijiji cha Qadian huko India mwaka 1835. Huyo ndiye nabii Isa wa mfano aliyesubiriwa kuja kutoka miongoni mwa waisilamu kuja kufundisha ule Uisilamu alioufundisha kipenzi chetu Mtukufu mtume Muhammad (saw), Hadhrat Ahmad (as) ni nabii mfuasi wa mtukufu mtume Muhammad (saw), kaja kuwaunganisha waisilamu chini bendera ya " laa illa illallah muhammad rasullah" isitoshe kaja kuwafanya watu wa dini zingine waingie kwenye Uisilamu.
Huo unabii amepewa na nani? na ushahidi kuwa hiyo jumuiyya imeanziwa kwa amri ya allah uko wapi?.
 
Yaani sijui tunabishania nini, anyway haya.

Wewe unasema hali ya huyo Rais kitokwa na mkojo hadharani kwamba kadhalilika, mimi nasema hivi; kudhalilika kunategemea na mazingira, huyo Rais ni mgonjwa na ugonjwa huo ni maarufu sana hivyo jambo likimtokea mgonjwa kwa Sababu ya huo ugonjwa hapo hakuna udhalilifu kwasababu ni Ugonjwa ndio umesababisha jambo hilo, udhalilifu unakuja katika mazingira yasiyokuwa ya Ugonjwa mfano nikakupa kwamba kama huyo Raisi angekuwa kanywa pombe na mkojo ukamtoka kwa bahati mbaya au kwa kusudi au akajiharishia hapo ndipo lugha ya udhalilifu inaingia, chukua mfano huu; kama badala ya kujikojolea aangeanguka kifafa na kutokwa povu mdomoni je hapo ungesema kadhalilika??

Usichanganye kati ya kudhalilika kwa kutokwa na haja (uchafu) hadharani kwa sababu ya kujitakia na hali hiyo itokee kwa bahati mbaya kutokana na ugonjwa ambao kila mtu anaweza kuupata.
 
Kwa wanaojua presidential directives za mamlaka kama hapa Tz, Ni Nini kinapaswa kifanyike hapo baada ya AIBU hio ? Atabadirishwa Nguo na kuendelea ama zoezi lilokua linaendelea litakomea hapo? Kivyovyote vile hawezi kuachwa hivyo
Yule minister wa kwetu alipewa huduma gani?
 
Katika tukio lisilo la kawaida, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mwenye miaka 71 ameonekana akitokwa na haja ndogo wakati wa hafla ya Kitaifa na wimbo wa Taifa ukipigwa. Kitendo hicho kinaibua maswali kuhusu hali za kiafya za viongozi wengi duniani kuendelea kukaa madarakani hata baada ya umri wao kuwa mkubwa na wengine wakiwa na afya zisizoridhisha.

Mwaka huu 2022, pia mgombea wa Urais nchini Nigeria Bola Ahmed Adekunle Tinubu mwenye miaka 70 alionekana akiwa na mfuko maalumu wa kuhifadhia mkojo wakati wa mchakato wa kuanza kampeni hali iliyopelekea wananchi kuhoji kuhusu afya yake na majukumu anayotaka kugombea.

Kisukari!!
 
Daah tezi dume noma. Mtoto wa mjini aliliwahi lisimletee madhara
Mtoto wa mjini mshamba tu
Mtu kama ruto ndiyo mtoto mjini sasa
Mumpe mda mje kuangalia mzee wa fursa hata akija kuwapiga nyie mnabarikia mnaona poa tu
Mtoto wenu wa mjini kwa sasa anayofanya kwa asilimia kubwa amejifunza kwa msukuma sasa mtoto wa mjini gani wote viazi tu
 
Angevaa suti ya rangi nyeusi, kidogo ingesaidia kuficha hiyo aibu.
Hiyo rangi ya suti aliyovaa, si rafiki kama wanajua kibofu kishafanya yake.
Viongozi wa kung'ang'ania madarakani, kila uchaguzi wapo. Utasema hakuna wengine wenye sifa za kuongoza nchi...
Suti nyeusi ingesaidia nini?...kojo linatiririka mpaka linatengeneza bwawa hapo chini unafikiri mchezo...usifananishe na ile kitu ya kila mwezi aisee...
Magonjwa yapo muhimu ni kukubali yaishe...hatusemi kwa ubaya ila watu waache ving'ang'anizi...angalia sasa..
 
Hawakumtengenezea sponji flani ya kunyonya mkoja hapo kwa chini?
 
Katika tukio lisilo la kawaida, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mwenye miaka 71 ameonekana akitokwa na haja ndogo wakati wa hafla ya Kitaifa na wimbo wa Taifa ukipigwa. Kitendo hicho kinaibua maswali kuhusu hali za kiafya za viongozi wengi duniani kuendelea kukaa madarakani hata baada ya umri wao kuwa mkubwa na wengine wakiwa na afya zisizoridhisha.

Mwaka huu 2022, pia mgombea wa Urais nchini Nigeria Bola Ahmed Adekunle Tinubu mwenye miaka 70 alionekana akiwa na mfuko maalumu wa kuhifadhia mkojo wakati wa mchakato wa kuanza kampeni hali iliyopelekea wananchi kuhoji kuhusu afya yake na majukumu anayotaka kugombea.

Watu wazima hao pengine ana tezi dume.
 
Back
Top Bottom