Mimi ni muisilamu wa Jumuiyya ya Ahmadiyya, Jumuiya ya Ahmadiyya imeanzishwa kwa amri ya Mungu na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) mwaka 1889, Yeye alizaliwa katika kijiji cha Qadian huko India mwaka 1835. Huyo ndiye nabii Isa wa mfano aliyesubiriwa kuja kutoka miongoni mwa waisilamu kuja kufundisha ule Uisilamu alioufundisha kipenzi chetu Mtukufu mtume Muhammad (saw), Hadhrat Ahmad (as) ni nabii mfuasi wa mtukufu mtume Muhammad (saw), kaja kuwaunganisha waisilamu chini bendera ya " laa illa illallah muhammad rasullah" isitoshe kaja kuwafanya watu wa dini zingine waingie kwenye Uisilamu.