Video: Yadaiwa Samaki Mtu (Nguva) aonekana ufukweni

Video: Yadaiwa Samaki Mtu (Nguva) aonekana ufukweni

Wataalam wa Nchi gani unawazungumzia kaka? Usikute ni hawa wabongo!! Ndege kubwa ilitua uwanja mdogo wa Arusha WATAALAM wetu wakasema ili ndege iweze kuruka tena lazima uwanja ujengwe kuongeza urefu vinginevyo itabakia hapo milele, wakaja wenye ndege yao ndege ikaruka nusu uwanja.
Walishahuri isafirishwe vipande vipande 🤣🤣🤣
 
Wakuu!

Mwanzoni niliziona Kama hadithi tuu za kizamani lakini baada ya kuiona video hii mtazamo wangu umeanza kubadilika.

Ingawaje bado sijapata uhakika wa moja Kwa moja kuhusu video hii kama imeghushiwa au laa.

View attachment 2179190
Nenda Makumbusho ya taifa posta ukajionee, yupo pale nguva wamemuhifadhi......
 
Mkuu; kama wewe mleta uzi huna uhakika na tukio hili ss wasomaji wako tuweje au tukueleweje?
Hii clip NI FAKE kwa hoja zifuatazo:
1. Mtoa mada yy mwenyewe hana uhakika na Tukio hilo.
2. Clip haioneshi Ufukwe unaodaiwa kutokea tukio hilo wala uwepo wa bahari ambamo ndio makazi ya kiumbe huyo.
3. Kwa hulka ya kibinadamu esp. Afrika , hapo Ufukweni pangelifurika watu waliokuja kushuhudia Tukio hilo. Lakini clip inaonesha watu 2-3 tena mandhari ya giza-giza.
4. Clip ni Fupi mno kitu ambacho kinawanyima watazamaji /wasomaji nafasi ya kudadisi kama ni Ukweli
# Nadhani tukubaliane Mkuu Robert Hariel, clip hii au Bango hili ulitegemea/ulilenga libandikwe na kusomwa sherehe ya tar.01/04/2022 😂

😀😀😀

Mkuu Mimi Kwa kweli kwenye mambo ya Teknolojia ya Photoshop sio Mtabe,
Hilo niwe muwazi,
Na Kama nikisema ni editing au sio editing nitakuwa naongopa tuu ndio maana nimeileta humu ili Wale Wataalamu WA ishu hizo watasema.

Najua kuna Wafuata mkumbo ambao watasema Editing pasipo na Facts zozote na Hilo ndilo Mimi linanishinda,

Maelezo yako mengine upo sahihi, hata Mimi ndio maana nashangaa Kama wewe.

Ila ninashindwa kufika hitimisho Kwa sababu ya Falsafa yangu kuwa; Duniani lolote linawezekana"
 
Kuna mwaka niliwahi soma makala kuhusu samaki nguza Ktk gazeti la mwananchi , nikagundua wengi mitaani tunapigana kamba.

😀😀😀

Ila uhakika ni kuwa hakuna kitu binadamu anachoweza kukisema au kukifikiri alafu kisiwepo, au hakijawahi kuwapo, au hakitakuja kuwapo
 
Bonge la wigi
Yaani hata hao wananunua mawigi kumbe
Utakuta na simu janja anayo
 
😀😀😀

Mkuu Mimi Kwa kweli kwenye mambo ya Teknolojia ya Photoshop sio Mtabe,
Hilo niwe muwazi,
Na Kama nikisema ni editing au sio editing nitakuwa naongopa tuu ndio maana nimeileta humu ili Wale Wataalamu WA ishu hizo watasema.

Najua kuna Wafuata mkumbo ambao watasema Editing pasipo na Facts zozote na Hilo ndilo Mimi linanishinda,

Maelezo yako mengine upo sahihi, hata Mimi ndio maana nashangaa Kama wewe.

Ila ninashindwa kufika hitimisho Kwa sababu ya Falsafa yangu kuwa; Duniani lolote linawezekana"
Ila kiukweli ni kwamba mnyama aitwaye Nguva yupo na anaishi baharini.
Zipo taarifa/maelezo sahihi na picha za mnyama huyo ila sura yake hafanani kabisa na binadamu. 🙏
 
Back
Top Bottom