Video: Yadaiwa Samaki Mtu (Nguva) aonekana ufukweni

Video: Yadaiwa Samaki Mtu (Nguva) aonekana ufukweni

Nina maswali matatu:
.Kwa nn Mweusi
.Tunamlaje sasa
.Namba yake ya simu,Halafu Tukiamua kumla tunamla kama samaki au Mtu.
 
Siku ukiona habari kama hii Aljazeer, CNN, Sky, RT ianzishie na wewe habari.
Nilishawahi kumuona nguva akitangazwa kuonekana maeneo flani visiwani akiwa amejiegesha juu ya mwamba. Habari iliripotiwa BBC miaka ya 2000 kama nakumbuka vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hizo ni hadithi ngano za zamani ambazo ni illusions zizizo.za kweli, hivyo watunhutengeneza picha za kijanja janja kama hizi ili kuoanisha na imani potofu walizokuwa nazo watu. Hakuna kitu cha namna hiyo hakijawahi kutokea na hakitatokea
 
Niliiona fb kwa urefu wa kama 3 ama 4 hivi.

Sidhani kama ni video ya kweli.
Kwanza angalia hao wanaochukua hiyo video wenyewe(mashuhuda), wanafanania na wavuvi??
Kwa rangi za hao watu wanaonekana ni weusi na hata huyo samaki mtu ni mweusi nachelea kusema ni waafriaka na ni video kutoka Africa na lugha waliyokua wanaongea hapo lafudhi yao si watu toka nje ya Africa nadhani ni west Africa hiyo.

Na huo mlio anaoutua huyo mwamba hapo chini ni kama wa ngurue, sauti inatokea wapi ilhali bado kafumba mdomo? Au hao samaki mtu sauti zao hutolea wapi??

Na hizo nywele si za kusokota kabisa jaman, ko huko chini ya maji kuna wasusi, vipi hiyo rangi yake haidhuriwi na maji kwa kukaa majini muda mrefu??

Na hilo dimbwi la damu hapo, alipigwa na hao wavaa modo ama niaje?, Mleta mda vipi kavuliwa au kakutwa tu ufukweni, au kapotea njia ???
 
Video zenye utata miaka yote zinakua low quality na fupi. Hata videos za UFO,aliens na hao nguva. Dunia inavitu very interesting sana angalia NAT GEO World utajua.

Viumbe kama hao wangekuapo kweli tungepata uhakika was kitu kinachoeleweka sio Kila siku video Kama hizo,watu wamemzunguka na video imekua fupi hivo kwanini asingechukua Kila kitu,kwanini watu hawaongei?Kwanini mtu mmoja tu ndio ana Simu?
Ungekuta walishamchukua mmoja kumhifadhi kule Germany zoological society kama yule mjusi wetu wa kusini
 
Ukiangalia kwa makini kipande cha kiunoni mpaka chini kiko very sharp tofauti na sehemu nyingine Za video hivyo kwa asilimia 99 hii video ni fake
 
Tuliza mteru bro hii clip imeditiwa tena kishamba sana, mathalani ukitazama kwa makini utagundua nguva kavaa wigi na hicho kiwiliwili chake cha juu hata hakiendani na cha chini
 
Tuliza mteru bro hii clip imeditiwa tena kishamba sana, mathalani ukitazama kwa makini utagundua nguva kavaa wigi na hicho kiwiliwili chake cha juu hata hakiendani na cha chini
Kabisa
 
Nguva wa mchongo huyo.

Wapo samaki wanaitwa nguva ila sio kama inavyovumishwa kwamba nusu mtu nusu samaki,nguva ni samaki kuanzia kichwa mpaka mkia hana mikono wala nywele.
 
Wakuu!

Mwanzoni niliziona Kama hadithi tuu za kizamani lakini baada ya kuiona video hii mtazamo wangu umeanza kubadilika.

Ingawaje bado sijapata uhakika wa moja Kwa moja kuhusu video hii kama imeghushiwa au laa.

View attachment 2179190
Mkuu; kama wewe mleta uzi huna uhakika na tukio hili ss wasomaji wako tuweje au tukueleweje?
Hii clip NI FAKE kwa hoja zifuatazo:
1. Mtoa mada yy mwenyewe hana uhakika na Tukio hilo.
2. Clip haioneshi Ufukwe unaodaiwa kutokea tukio hilo wala uwepo wa bahari ambamo ndio makazi ya kiumbe huyo.
3. Kwa hulka ya kibinadamu esp. Afrika , hapo Ufukweni pangelifurika watu waliokuja kushuhudia Tukio hilo. Lakini clip inaonesha watu 2-3 tena mandhari ya giza-giza.
4. Clip ni Fupi mno kitu ambacho kinawanyima watazamaji /wasomaji nafasi ya kudadisi kama ni Ukweli
# Nadhani tukubaliane Mkuu Robert Hariel, clip hii au Bango hili ulitegemea/ulilenga libandikwe na kusomwa sherehe ya tar.01/04/2022 😂
 
Wataalamu WA IT watujuze hiyo Video ina-editing au ni tukio la kweli
Wataalam wa Nchi gani unawazungumzia kaka? Usikute ni hawa wabongo!! Ndege kubwa ilitua uwanja mdogo wa Arusha WATAALAM wetu wakasema ili ndege iweze kuruka tena lazima uwanja ujengwe kuongeza urefu vinginevyo itabakia hapo milele, wakaja wenye ndege yao ndege ikaruka nusu uwanja.
 
Back
Top Bottom