Video: Zitto Kabwe akiunga mkono faragha za watu hata kama ni ushoga ulipigwa marufuku kisheria

Video: Zitto Kabwe akiunga mkono faragha za watu hata kama ni ushoga ulipigwa marufuku kisheria

Tunajifunza kwa waliotangulia kuhalalisha hiyo faragha.
Walianza na faragha
Ikafuata kutambulika kisheria na kijamii.
Sasa wanawafundisha watoto wasio na hatia mashuleni utamu wa faragha.
Je hadi hapo kuna faragha?
Sio yote ya kuiga, mengine tuyaache yaende
Ndo utumie nguvu kuwaepusha watoto wako na hilo balaa.
Kwa dunia ya sasa utapinga haya mambo lakini hutakuwa na nguvu ya kuzuia hata iweje.

Serikali yenyewe imeshindwa thats why unaona mashoga wakitamba bila wasiwasi na sheria walizoziweka wanashindwa kuzisimamia.

Pambana kulea watoto wako katika njia sahihi ili kuwaepusha
 
Nilikuwa nakuona wa maana kumbe ni mpuuzi fulani hivi,

..kazi na dawa.

..you can not be serious all the time.

..mazoezi ni muhimu sio kumuachia unakuwa na makalio na tumbo kama la mwanamke.🤣
 
..kazi na dawa.

..you can not be serious all the time.

..mazoezi ni muhimu sio kumuachia unakuwa na makalio na tumbo kama la mwanamke.🤣
Hapana sio vizuri,tumseme sana kwa mambo mengine,

Lakini kwa umbile alilopewa na mwenyezi Mungu jana namna ya kufanya, hata afanye mazoezi,

Sijawahi ina mtu a nafanya mazoezi ya kupunguza makalio.

Hapo kubali umeteleza
 
Ndo utumie nguvu kuwaepusha watoto wako na hilo balaa.
Kwa dunia ya sasa utapinga haya mambo lakini hutakuwa na nguvu ya kuzuia hata iweje.

Serikali yenyewe imeshindwa thats why unaona mashoga wakitamba bila wasiwasi na sheria walizoziweka wanashindwa kuzisimamia.

Pambana kulea watoto wako katika njia sahihi ili kuwaepusha
Kuna malezi ya kifamilia ambayo wanawajibika walezi.
Pia kuna malezi ya kijamii ambapo inawajibika jamii nzima.
Sio rahisi kulea watoto na kuwaongoza kwenye maadili mema kwenye jamii iliyoharibika.
 
Kuna malezi ya kifamilia ambayo wanawajibika walezi.
Pia kuna malezi ya kijamii ambapo inawajibika jamii nzima.
Sio rahisi kulea watoto na kuwaongoza kwenye maadili mema kwenye jamii iliyoharibika.
Upo sahihi lakini jamii imeshaharibika na inaendelea kuharibika jinsi miaka inavyosogea.

Tumeanza lini kuongelelea haya mambo na hujaona yakipungua kama sio kuongezeka na kupewa promo kila siku?

Jamii unayoizungumzia ikiongozwa na serikali yake ni ya kinafiki, zaidi ya kupiga kelele kwenye mitandao hawafanyi lolote kwenye uhalisia.

NI wewe mzazi jukumu lako kumuongoza mtoto wako aishi kwenye aina gani ya jamii inayomzunguka.
Unaweza usifanikiwe sana lakini kwa malezi yako wewe jinsi utakavyomuongoza inaweza kusaidia.
 
Mnaishi nao,tunaishi nao,mkiandaa
Shuguli wanakuja mnawaalika

Ova
 
Kuna mambo mengine hata ukisema unapinga hayapunguzi wala kuongeza kitu kwa maana mambo yenyewe yanafanyika gizani, huwezi hata kuthibitisha.

Mabinti wengine wanadai ni marafiki sana, kila mara wapo wote, wanalala chumba kimoja, hujui kama ni urafiki tu au ndio wanafanyiana huo uchafu, na huna uwezo wa kuthibitisha.

Tukazane kuwalea watoto wetu katika maadili tunayoyaamini japo hatuna uhakika wa 100% kuwa hawawezi kuja kuyageuka maadili yetu.

Lakini kwa upande mwingine, si aheri shoga kuliko wanaoteka watu, wanaowaua, wanaopora mali za watu, halafu bado tunawashangilia kwa sababu wamepanda punda au lorry. Shoga anafanya huo uchafu kwenye mwili wake, lakini haya majitu tunayoyashangilia yalikuwa yanaumiza na kupoteza nafsi za watu wasio na hatia.

Bila shaka itakuwa rahisi kwa shoga kuionja ahera kuliko watekaji, wauaji na wadhulumu mali za watu kwa kutumia madaraka yao. Yamelaanika majitu hayo na vizazi vyao.

Hata haya mafisadi ya kwenye report ya CAG, yanaumiza jamii kubwa ya watu kuliko mashoga. Kila.mmoja akiulizwa ameumizwa na nini na kwa kiasi gani na mashoga, ni wachache sana watakaopatikama, na zaidi watakuwa wanafamilia wa hao mashoga, na zaidi watakuwa wameuamia kisaikolojia kuliko ule uhalisia wa moja kwa moja.
 
Zitto kanifanya nicheke sana yani kumbe kuna namna ya kujibu hili swali ambayo haitakuwa na makali sana.

Yani kuna ujibuji wake wa hili swali ambapo haitaonesha kuwa unapinga ushoga bila

Lakini viongozi wetu kwanini kwenye ishu ya kupinga ushoga wanakuwa na kauli za kusita (indirect) lakini kwenye kukemea madada poa wanaenda straight?

Natamani hili swali aulizwe Chalamila siku moja
Ni kujitoa ufahamu kuwa eti tunachukia ushoga wakati tumeshindwa kuwachukia wevi wa pesa ya umma, tumeshindwa kuwachukia wauaji na waporaji, tumeshindwa kuwachukia wevi wa kura, tumeshindwa kuwachukia wanaouza rasilimali za nchi kwa manufaa yao.

Yaani ushoga usioyagusa moja kwa moja maisha yetu utuumize kuliko uchafu wa kila aina tunaofanyiwa na watawala, na tunaendelea kuwashangilia na kuwapamba.

Kama kweli tunachukia uovu, tunze kwanza na hili shetani lililokuwa linasimamia utekaji na mauaji ya wakosoaji wa serikali.ya awamu ya 5. Tuje na hawa waliouza bandari na mamlaka ya nchi yetu, tumalizie na haya mafisadi yaliyotajwa na CAG. Vinginevyo, kusema tunachukia ushoga ambao haugusi maisha yetu moja kwa moja, ni 'UNAFIKII'.
 
Yuko sahihi 💯%.
Nakumbuka wakati fulani, M. Bandio (Diaspora wetu yupo Marekani) alirusha live kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kikao cha watanzania wanaoishi Marekani.

Kilichonistua, baadhi ya wanaume kwenye Kikao hicho walijitambulisha Tena kwa lugha ya kiswahili kuwa bado "hawajaolewa"....Niliwaza sana, Baadaye nikahisi labda walitafsiri neno " married" moja kwa moja kwenda kiswahili!!!

Kadri siku zinavyosonga naona nilichokiwaza katika tafsiri kinaweza kuwa si kweli.
 
Kwahiyo anaheshimu faragha hata kama ni kinyume cha maumbile.
Aulizwe kama mtu atakuwa faragha na binti yake au mwanae au akiwa faragha na mnyama iwe mbuzi au bata mzinga anaendelea kuheshimu maadam wako faragha?
 
Wakiwa faragha wewe utajuaje wamesuguana?
Unadhani faragha ya wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake inamaanisha nini? Kama sio kufirana na kusagana? Ni Haramu. Period
 
Back
Top Bottom