Inasikitisha sana yale yalotokea kipindi mv bukoba inazama leo hii ndo yale yale yaloikuta ndege yetu na kusababisha vifo visivotarajiwa sina uzoefu na ndege ila siku ya tukio sikuwa mbali na eneo husika baada ya ndege kupata ajali eneo la mbele la ndege liliingia ndani ya maji na kubakiza mkia na eneo la kati vikiwa havijafikwa na maji kilikuwa ni kitendo cha kuvutwa ile ndege na kusogezwa eneo lina kina kidogo ndo mlango ukafunguliwa yakafanywa yale yale ya mv bukoba, akatokea kijana wa hovyo asie na maarifa akafungua mlango wa ndege na kusababisha abiria walokuwa ndani ya ndege na rubani wetu maskini wamejifunga mikanda ili kungoja taratibu za uokoaji, kijana wa hovyo alafungua mlango na kuingiza maji kwenye ndege ndicho kilichofanya abiria hao 19 kufariki Dunia ni jambo baya mno