Vifo vingi vya Marais wa Kiafrika vinatia mashaka

Vifo vingi vya Marais wa Kiafrika vinatia mashaka

Toka miaka ya 1980 Idriss Deby alihusika mwenyewe kupigana. Alimsaidia kupindua nchi Hissene Habre kisha naye akampindua 1990. Alikuwa rais anayepigana mwenyewe mstari wa mbele na waasi au maadui wake. Alikuwa rais mpiganaji na hatari sana.

Mtoto wake Mahamat Kaka mwenye miaka 37 naye anafuata ya baba'ke. Sasa ndiye anayeongoza Tchad kupitia Baraza la Mpito la Kijeshi. Hayo pia ni mapinduzi maana alipaswa kuongoza spika wa bunge. Nchi hiyo iko vitani tangu ipate uhuru huku utajiri wa mafuta yakifaidi makampuni ya nje na wachache wenye mamlaka, si wananchi wa Tchad.

Mataifa ya magharibi, hasa Ufaransa, yalimpenda sana Deby kwa kuwaachia wachote rasilimali za nchi bila bughudha yoyote na pia kumkubali kwa uwezo wake wa kupigana na ugaidi katika nchi tano za Sahel. Sasa naye kupigwa kwenye uwanja wa vita
Hivi raisi anaendaje vitani jamani? Is this possible .Tena front kabisa??
 
Hajauawa na walinzi wake bali waasi wa FACT akiwa vitani kaskazini mwa Tchad kwenye milima ya Tibesti jangwani. Hata mtoto wake Mahamat Kaka naye alikuwa vitani sambamba na baba yake, na ndiye kampindua spika na kuchukua nchi kinyume na katiba. Kwahiyo aliyepinduliwa ni spika, si hayati Deby!
Kauawa na wanaomlinda

Yale ni Mapinduzi ya kijeshi ndio sababu baada ya Mauaji Jeshi lime chukua nchi badala ya Spika kama katiba yao inavyoelekeza
 
Lakini kaingia mwanawe Mahmat Idris Deby
kwanza kafa peke yake au kuna wanajeshi wamekufa pia kwenye hayo mapigano.....kama kafa peke yake ....wanajeshi wake ndo watakua wamemuua
Vyombo havijaripoti kuhusu wengine. Kuna jambo linafichwa
 
Na wanajeshi wake kadhaa pia waliuawa pamoja naye. Serikali ilisema watano lakini inaelekea ni zaidi ya hao. Yeye Deby alijitapa kwamba kaua waasi 300 labda hakuwa mkweli.

Alipoambiwa kashinda urais kwa 80% alisema hayupo ikulu, angekuja kusherehekea ushindi baada kuwafyeka waasi, sasa kafyekwa yeye!!!
kwanza kafa peke yake au kuna wanajeshi wamekufa pia kwenye hayo mapigano.....kama kafa peke yake ....wanajeshi wake ndo watakua wamemuua
 
Nilivyoona unajiita Detective J nikajua umepitia masuala ya usalama. Kumbe ni mropokaji tu. Rais mpaka anakwenda battle front bila tathimini ya kiusalama?
Hiyo tathimini ya usalama ndo inazuia mtu asife.aliyekwanbia kifo kinazuiwa hivyo ni nani.Ukitoa cheo chake cha kisiasa huyo ni binadamu kama binadamu wengine na ilikua lazima afe kama wanavyokufa wengine hiyo ya kwenda uko ni sababu tu ya kifo chake na ilikua lazima aende ili akafe.
 
Angalia Laurent Kabila alivyouawa, mlinzi wake Rashid Kasereka, ambaye baadaye alipigwa risasi na Col Eddy Kapendi. Ni kama mchezo wa kuigiza . Maana inasemekana Rashid alikuwa anasubiriwa na mtu nje ya Ikulu huku ngazi ya kuruka ukuta nje ikiwa imeandaliwa. Mpaka leo hii nani alipanga njama za kumuua Kabila ni ndoto.

Mauaji ya Cyprian Ntayaramirwa na Habyarimana yalionesha namna gani ukiwa Rais wa kiafrika unakuwa unawindwa ili uuliwe kwa nguvu au kwa kutumia akili.

Leo hii Idris Deby Rais wa Chad anauawa akiwa battlefront, jambo ambalo ni mashaka makubwa.

Kwamba Rais wa nchi anakwenda battlfront bila taarifa kamili za kiusalama?

Duh, watanzania tumuombe Mungu.
Wala havina mashaka mkuu,mbona wanaohusika ni mabeberu.Shida ni rasilimali mkuu.Nchi ikishakuwa na rasilimali,kwao hiyo ni laana.Wanataka wachukue bure au kwa bei ya kutupa,wakizuiwa tatizo lina anzia hapo.Na mbona walishasema hawataki Marais wazalendo wanaopenda wananchi wao?

Fuata link ifuatayo mkuu utapata jibu.

Hiyo tathimini ya usalama ndo inazuia mtu asife.aliyekwanbia kifo kinazuiwa hivyo ni nani.Ukitoa cheo chake cha kisiasa huyo ni binadamu kama binadamu wengine na ilikua lazima afe kama wanavyokufa wengine hiyo ya kwenda uko ni sababu tu ya kifo chake na ilikua lazima aende ili akafe.
Kwa nini usikae kimya?
 
Kuna Mgogoro na mpasuko mkubwa ndani ya Jeshi na ndio inasemekana walifanya usaliti akiwa eneo la mapambano

Tusubiri report kamili

Back
Top Bottom