Vifo vingi vya wanajeshi wa Israeli chanzo chake ni nini?

Vifo vingi vya wanajeshi wa Israeli chanzo chake ni nini?

Hakuna vita ngumu kama kupigana na mwanajeshi asiye na sare
 
Hivi hizi habari unatoaga wapi make israel inachapika afu dunia nzima inandamana kuionea huruma palestina hii ni ajabu. Nikiangalia aljazira na maongezi yako naona vituko tu
Hata Russia kwenye TV alikuwa anachapika kwelikweeli..... Sijui kinachoendelea hawatoe Tena zile taarifa zao za vifurushi na vikoba mara sanctions... Viliishia wapi...!??
 
Wanakumbi.

VIFO VINGI VYA WANAJESHI WA ISRAELI, CHANZO CHAKE NI NINI? 🇮🇱🇵🇸

Watu wengi wanajiuliza kwamba tangu Jeshi la Israel litangaze kuanza kufanya operesheni ya nchi kavu “Ground Operation” wamefikia wapi wapi na uwezo wao wa kijeshi na misaada kutoka Marekani na mataifa mengine.

Wiki kadhaa zimepita tangu kurejea kwa mapigano mapya pale Gaza mara baada ya makubaliano ya kusitisha kwa muda mapigano hayo kumalizika.

Tangu kurejea kwa mapigano mapya,

Ni takribani wiki kadhaa Jeshi la Israeli halijafanikiwa malengo yake Gaza pamoja na kubana vyombo vya habari kuifahamisha dunia wameishia kuwauwa waandishi hawa habari hapa Gaza kama wanavyouwa watoto na raia wasiokuwa na hatia yetote.

Kinyume na matarajio yao, awamu hii wamepata madhara makubwa kuliko kawaida ndiyi maana hadi Uongozi wa Jeshi lao umetangaza vifo pamoja na majeruhi wengi waliopatikana hivi karibuni uwa ni ngumu kutangaza mpaka wameamua kutangaza hesabu za kisiasa basi hali ni tete Gaza.

Taarifa hizi wala siyo propaganda, hatuandiki kuwafurahisha watu bali tunaleta uhalisia uliopo ambao ni ngumu kuupata mbele ya media zinazotawala dunia kama CNN, BBC, FOX NEWS na media zingine za magharibi.

Kwa nini Jeshi la Israeli linapata sana madhara kwenye operesheni ya nchi kavu pale Gaza?

Hamas wametawala na kutawanyika kila kona ya Gaza, kwa lugha rahisi unaweza kusema rada zao zinawachora tu wanajeshi wa taifa teule.

Kila hatua ambayo wanajeshi wa Israeli wanadiriki kuipiga kwa kuingia Gaza, ni kama vile wanakuwa wameingia kwenye tanuri la moto.

Kubwa zaidi ni mbinu hatari inayotumiwa na Hamas katika kupambana na wanajeshi wa Israeli.

Jamaa wameweka Wadunguaji (Snipers) kwenye maeneo mbalimbali ya Gaza, kila hatua moja ambayo wanajeshi wa Israeli wanaipiga, wanapoteza wanajeshi wengi sana na wengi wamebaki vilema vya maisha.

Ndiyo maana hivi karibuni idadi ya vifo vyao imeongezeka kuliko kawaida.

Ogopa sana kwenda kufanya vurugu kwenye uwanja wa nyumbani wa adui yako, wenzako wanayajua machaka ambayo wakijificha wewe huwezi kuyajua, ndicho kinachowakuta wanajeshi wa Israeli kwa sasa.

Wadunguaji wa Hamas wamejificha na Mashine zao, jamaa wakitoka tu kwenye vifaru vyao, wanachapwa za vichwa kisha Hamas wanapotea kama mizimu.

Huo ndo uhalisia uliopo pale Gaza, nadhani sasa utakuwa umepata picha kamili.

Wanachofanya sasa hivi ni hasira kufanya mashambulizi holela hawajui malengo ya vita ni yapi.

Hii leo ….

View: https://x.com/warintel4u/status/1738853337477300353?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw

Unadanganyka na Aljazeera.

God Bless Israel
 
Hakuna vita ngumu kama kupigana na mwanajeshi asiye na sare
Hamas hawa hapa wanajulikana wewe unameza propaganda za Israel dalili za kushindwa hizo kwani hao watoto 9000 waliowauwa walikuwa na sare???
 

Attachments

  • IMG_8459.jpeg
    IMG_8459.jpeg
    54.8 KB · Views: 2
  • IMG_8456.jpeg
    IMG_8456.jpeg
    79.7 KB · Views: 2
Ona ulivyo haujielewi.
Unatuletea chanzo Cha habari Cha mossad.
UN wenyewe wamefanya uchunguzi na wanatoa ripoti kuwa wanaofariki wengi Ni wanawake na watoto.
Inamaana wewe unaekaa mchambawima una akili kuliko UN staff members?!
Huwa nacheka sana jamaa yeye yupo JF kwa ajili ya kubishana UN kuongea ukweli wamenyimwa viza za kuingia Israel, pia wanashambulia magari ya kubebea wagonjwa na ofisi.
 
Ona ulivyo haujielewi.
Unatuletea chanzo Cha habari Cha mossad.
UN wenyewe wamefanya uchunguzi na wanatoa ripoti kuwa wanaofariki wengi Ni wanawake na watoto.
Inamaana wewe unaekaa mchambawima una akili kuliko UN staff members?!
Hujajibu swali
 
Back
Top Bottom