Vifo vya vigogo vyaacha Simanzi

Vifo vya vigogo vyaacha Simanzi

Hapo Mwananchi wanatuma ujumbe fulani kwa wasomaji ....we huelewi?!

Kabisa maana sie watanzania hatuelewei bora wananchi walivyoweka picha ili tuchanganye na zetu halafu chini wakaweka rais kavaa barakoa.
 
Viongozi wetu walitoa maneno ya dhihaka sana kuhusu gonjwa hili, hawakuacha maneno ya akiba, na licha ya gonjwa kurudi kwa kasi ya 4G ila bado wanaongea maneno ya uongo kwamba halipo (Wamelibatiza jina jipya Pnemonia).

Taifa lipo njia panda, wananchi wanataharuki wakisubiri tamko la serikali, ila serikali ipo kimya ikisisitiza hakuna Covid-19 kuhofia kuaibika mbele ya walimwengu.

Mpaka lije kuondoka na kigogo mmoja wa juu ndio akili zitawasogea. Na litaondoka tu na mtu wa juu hivi karibuni.
Maamuzi ya busara ni kuwa kimya , Mana wakitangaza tu manyanyaso na unyanyapaa unashamiri kweli. Tanzania hakuna korona over
 
Author wa hilo gazeti ameona ni sifa kuchapicha gazeti namna hiyo au ?
Waandishi wa siku duh ! E Mungu tuepushe kwenye hili janga.
Ulitaka hiyo habari isomekaje mkuu?
Wananchi wa kawaida wakifa hawatangazwi, kwanini ujumbe usifikishwe kupitia kupukutika kwa watu mashuhuri nchini?
Au Kama hujaelewa dhima kuu ya hiyo habari bhasi uitafakari kwa mara nyingine. Kaitendea haki taaruma yake na kiapo chake
 
Mkuu angetoa elimu ingependeza zaidi, sio kutumia vifo. Kwani hili jukumu la kujikinga na huu ugonjwa ni lazima litolewe na kiongozi tu ?
 
Kachapisha uongo????
Sio sawa kabisa kutumia vifo, ili jukumu ni la kila mmoja sio lazima maamuzi ayatoe kiongozi.
Tujiulize kwanza ss tumechukua hatua gani kujikinga na hili janga linaloendelea kuitesa dunia. Ndipo tuanze kukosoa.
Imeisha hiyo
 
Wananchi kielimu hatupo sawa, kuna watu Kiongozi wao Mkuu akisema kitu huwaambii kitu, zaidi ukiendelea kuwaambia unaweza chezea kichapo, hao tunawasaidiaje?
 
Corona si mjinga kama wewe ufikiri ya kuwa ana siasa,yeye kazi yake ni kuua tu!
Ni kweli kabisa corona si mjinga,huwezi kujazana kama vile kwenye mikutano ya kampeni bila kuachiana nafasi hata kidogo wala kuvaa barakoa huku mkishindana nyomi et corona ilipungua,aisee! hapo corona lazima ifanye kazi yake ya kuuwa tu.

Kipindi chote cha uchaguzi hatujahimizana kuchukua tahadhari kwa sababu ila baada ya uchaguzi kuisha ndio tunarudi kuambiana kuchukua tahadhari kana kwamba corona ilituachia tufanye uchaguzi,hizi kama sio siasa ni nini?
 
Mkuu angetoa elimu ingependeza zaidi, sio kutumia vifo. Kwani hili jukumu la kujikinga na huu ugonjwa ni lazima litolewe na kiongozi tu ?
Mkuu kumbuka mpaka numbers zimetolewa mitandaoni na TCRA kwamba ukiona mtu anazungumzia uwepo wa huu ugonjwa nchini screenshot sms zake na number then utume katika hizo number alokezi. Je kwa mustakabali huo ulitaka auongelee huo ugonjwa wakati serikali haitambui uwepo wa Covid-19?
That's a clear and precise massage kuwa atakayeelewa na aelewe.
 
Jana TANZIA zilikuwa nyingi aisee, leo Mwenyezi Mungu tunakuomba utusaidie tupite salama, wenye kuvaa barakoa msiache kuvaa.
Unamuomba Mungu gani akusaidie kwenye hili janga?Mungu huyu huyu aliyemuomba Magufuli kuondoa corona?
 
Wananchi kielimu hatupo sawa, kuna watu Kiongozi wao Mkuu akisema kitu huwaambii kitu, zaidi ukiendelea kuwaambia unaweza chezea kichapo, hao tunawasaidiaje?
Waache wapambane na hali zao, siku watakapoelimika ndipo wataelewa hawakuwa sahihi kwa 7bu binadamu tunajifunza kulingana na makosa.
 
P

Ni suala la muda tu
Sidhani.. at least elements za kugomea yale yaliyofanyika kwenye uchaguzi uliopita zingejionesha ningesema labda au ni swala la muda. Kuna watu wanaendelea kunenepa na kujitunisha kwa ukondoo wa watanzania😆😭
 
Viongozi wetu walitoa maneno ya dhihaka sana kuhusu gonjwa hili, hawakuacha maneno ya akiba, na licha ya gonjwa kurudi kwa kasi ya 4G ila bado wanaongea maneno ya uongo kwamba halipo (Wamelibatiza jina jipya Pnemonia).

Taifa lipo njia panda, wananchi wanataharuki wakisubiri tamko la serikali, ila serikali ipo kimya ikisisitiza hakuna Covid-19 kuhofia kuaibika mbele ya walimwengu.

Mpaka lije kuondoka na kigogo mmoja wa juu ndio akili zitawasogea. Na litaondoka tu na mtu wa juu hivi karibuni.

Nasema uongo ndugu zanguuu?
Amina!
 
20210124_145819.jpg
 
Back
Top Bottom