uzi safi sana.
Niliingia Dar kwa nguvu zangu. Nikaenda Ulaya kwa juhudi zangu. Lakini hainifanyi nichukie waliobahatika kuishi maisha mazuri ambayo mpaka leo wapo nostalgic. Ndo dunia ilivo……jamii ina matabaka.
kama hukuishi ushuani the best you can do, tengeneza mazingira wanao wayaishi hayo maisha. Otherwise hatuwezi kuwa Sawa.
Mkuu una roho safi sana.
Ukiwa na kijiba cha roho unajiumiza mwenyewe tu.
Kitu muhimu ni kufanya kazi kuboresha hali yako, kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto na wanaokufuatia, na ukishindwa kabisa ukubali hali yako kwa roho safi bila kujisikia unyonge, maisha ni zaidi ya nafasi katika jamii na utajiri.
Shaaban Robert hakuwa mtoto wa Oysterbay lakini kuna watoto wa Oysterbay kibao wamesoma katika shule iliyopewa jina lake.
Kwa nini? Alikuwa na mchango mkubwa katika literature ya Kiswahili kwa namna ambayo hakuna mtoto wa Oysterbay aliyefikia.
Labda unaweza kusema huyo wa zamani sana.
Diamond Platnumz hajasoma sana, hata Kiingereza hajui vizuri, lakini hakujisikia unyonge, kajikubali, kajiongeza, leo hakuna mtoto wa Oysterbay anayejulikana dunia nzima kama Diamond Platnumz, mtoto wa Tandale sijui Mbagala huko LeMutuz alikuwa anapaita maswekeni.
Rapper Rakim aliwahi kusema "It's not where you're from, it's where you're at".
Hapa tunapiga stories tu kukumbushana tulivyokua, majirani, kukumbuka waliotangulia mbele kwa kifo, mpaka majirani walioishi next door wanajuana, hatuna nia ya kumfanya mtu mwingine ajisikie mdogo na sisi tuliokulia Oysterbay kuwa zaidi.
Kwa kiasi kikubwa nafasi za kukulia huko zimekuja na bahati fulani, ambayo mtu yeyote angeweza kuipata, na wengine baba zetu wamezipata, ingawa na wao walipozipata hizo bahati wengi wao hawakuzilazia damu, hawakuogopa umande.
Mfano huyo Malecela aliyekuwa Waziri Mkuu wakoloni walikuja kwa Chifu Mazengo kutaka kuwasomesha watoto wa Chifu Mazengo, Chifu Mazengo akakataa watoto wake kusomeshwa na wakoloni.
Wakoloni wakaenda pembeni kwa baba yake Malecela kumuomba wasomeshe watoto wake, ndiyo John Malecela na Job Lusinde wakapata nafasi kusoma.
Ina maana yule Chief Mazengo angekubali watoto wake wasomeshwe na wakoloni, leo labda huyo Malecela tusingemjua.
Na huko ndiko Watanzania karibu wote tumetoka, ukichunguza hata kama familia ina wasomi sana utakuta kuna sehemu huko nyuma kulikuwa na pure chance event imewapa the edge.
So, mara nyingine ni vijimambo vya maisha tu vinatoa nafasi, si kwamba watu wanatamba kwamba wana uwezo zaidi.