Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Nani anakumbuka siku Nigga One alivyofariki kwenye ajali ya gari?

Kwanza wangapi humu wanajua Nigga One ni nani?
Dah,

Adili Kumbuka Nigger One.

Nilikuwepo kwenye msiba, nilikwenda mpaka kwao Ilala kule kwenye mazishi.

Nigger One alikuwa ana chill sana Masaki IST lakini alikuwa na family Ilala nafikiri.

Ulikuwa msiba mkubwa, alikuwa very popular member wa Kwanza Unit.
 
Nadhani baba yake alikua na akaa Ilala , ila mama yake na dhani alihamia Obay , kitu kama Mama yao alikua hapo IST ,ila sina uhakika ilikuaje waka pata nyumba Oysterbay kama hakuwa mfanyakzi wa serikali au shirika , lada mama yao alikua kwnye shirika fulani , ila nadhani yule sister wake alika hapo jirani na kina Mwingira .
 
Oi mambo ya roho inakuwaje? [emoji23][emoji23]
 
Chief
Mbona kama umechufukwa? Vidole vinapishana, tuishi man.
 
That was very tragic!

At the time I thought he was the most lyrical member of the group.
 
 
Kuna Binti mmoja Celline... ubini nahifadhi.. mtoto aliishi Zambia & Bongoyo road.. alinielewA sana.. she was the only one in the family.. alifanya Medicine, Muhimbili baadae akaenda Antlanta, Georgia.. nilikua nikifika obey.. ananitambulisha kwa Mama ake... my Boy..
Raha sanA....
 
Nani anaikumbuka Mambo Club?

Kipindi hicho ilikuwa inamilikiwa na mdogo wake na Le Mutuz, marehemu Ippy.

Siku hizi kuna klabu ingine hapo ambayo ni dada poa central.

Kuna siku nilienda just out of curiosity…..sijarudi tena maana nilikuwa kama samaki kwenye nchi kavu.
 
Seriously? Dah…..hiyo nilikuwa sijui aisee.
Mimi siku hizi nikiongea na watu kuulizia watu ambao sijawaona siku nyingi nakuwa naulizia ki magutu magutu, halafu najitayarisha kwa jibu lolote kabisa.

Unaweza kuulizia mtu, ukapata kilio.

Kuna siku nilikwenda Sinza kwa mshkaji mmoja, bahati nzuri pale nje kwao nikakuta watoto, kwanza ile nyumba nikawa kama sijaijua kwa sababu walivunja ya chini wakajenga ghorofa, nikauliza hapa ndipo kwa kina George?

Wale watoto wakajibu ndiyo, lakini George alishafariki, yupo mama yake tu.

Basi nikagonga hodi, nikamsalimia yule mama, nikaulizia namba za mdogo wake George naye alikuwa mshkaji.

Sasa nikaona bahati sana kuongea na kupata habari kutoka kwa wale watoto kwanza.

Najiuliza ingekuwa vipi ningegonga mlango halafu namuuliza yule mama George, George yuko wapi, halafu George kafariki.

Ingekuwa kama narudisha msiba upya.
 
Dah,

Mambo Club ndiyo hii ya hapa Karibu Hotel siyo?

Mambo Club nimeruka sana nyoka hapo na mchizi wangu Mikola Mahiga (RIP).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…