Hahaaa,
Mkuu wewe unamjua. Hilo jina la maskani kabisa wewe unazijua code.
Jamaa alikuwa anakuja maskani na Benzi la Ikulu.
Kiaro yuko wapi sijui siku hizi. Mara ya mwisho niliongea naye alikuwa Nairobi kwenye deal zake.
Kuna siku mshkaji wetu mmoja alikuwa na daladala lake, basi likakamatwa na Polisi. Likawekwa Oysterbay pale.Polisi walikuwa wanamzingua tu mshkaji wanataka hela.
Basi mshkaji akamwambia Kiaro, Kiaro ee, kuna Wamwera wananizingua huku, njoo useme nao.
Basi daah, Kiaro akanunua ile kesi mara moja.
Basi Kiaro akaenda na Benzi la Ikulu akapaki mlangoni pale Oysterbay Polisi.
Sasa si unajua mwana alivyopanda hewani, Kiaro hapo kipande cha mtu anapiga vyuma kama hana akili nzuri, halafu kapiga upara wake ule ameupaka mafuta unag'aa kama kioo, ana miwani ya jua ya kijasusi ile, juu kapiga T Shirt, chini ana Jeans kali, halafu kapiga buti la jeshi jeusiiii linang'ara.
Kaingia Oysterbay Polisi tu akaanza kuwaamrisha wale askari anawaambia "nataka mliachie hili daladala mara moja" yani hakuna majadiliano wala nini.
Wale Polisi kumuangalia tu wakawa wanaogopa, wanajiuliza huyu kiumbe ni nani, usalama wa taifa? Hii Benzi mbona kama ya Ikulu? Huyu jamaa kajiamini vipi kuingia kituo cha Polisi Oysterbay na buti za kijeshi? Huyu ni mwanajeshi au vipi?
Basi akaitwa mkuu wa kituo pale, yule mkuu wa kituo alikuwa anamjua Kiaro, akaanza kujichekesha chekesha lile daladala likatokewa mara moja.
Kiaro mtu poa sana, hana shobo wala mashauzi na mtu, mnakaa naye maskani mnapiga stories, jioni huyo anarudi Sea View anaenda kumnyoa nywele rais Benjamin Mkapa.