Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Luhqngas sasa wakina a.luhanga na dada yk r.luhangas rip
Nlikuwa naendaga sana kwao
R.luhanga alifariki naye msiba wake uliniumaa sana alirudi masomoni toka Ireland
Unajua wakati bomb la ubalozi unatokea mm ilikuwa kama siku 2 hv niingie kwenda kuomba viza ndy balaa likatokea

Ova
Dah, noma sana.

Kwa Luhanga nilikuwa nakwenda kwa I. Kibonge.

Jamaa muhuni muhuni sana, maneno meengi, wakati huo primary anakula fegi mpaka ndumu. Halafu akila ndumu anataka anyonge mwenyewe, ukimnyongea tu lazima anakumind "wewe umejifunza wapi kunyonga vibaya hivi?" Aanakuzodoa.

Kibonge tulipewa makaratasi ya kuchangisha hela za madawati charity walk.

Watu wakazembea hawakuweza kuchangisha.

Kibonge kaipitisha ile karatasi kwa rafiki za baba yake, wadosi wote, kakusanya hela nyingi mpaka karatasi imeisha kaomba karatasi ya pili.

Mwalimu mkuu akamfanya mfano, anasema kuna watu hawajafikisha hata majina matatu, mtazameni mwenzenu Kibonge kachangisha mpaka karatasi imeisha kaja kuomba ya pili.

Tukamuona huyu kibonge noma sana anatufanya tuonekane wazembe.

Mzee Mwinyi alikuwa akikaa kwake pale Oysterbay, akiwa kapumzika, alikuwa anawaita jirani zake mzee Luhanga na Mzee Janguo wanapiga story na kunywa kahawa.

Wazee wamefurahia maisha, yani rais jirani yako, halafu mtu pooa.
 
Dah, noma sana.

Kwa Luhanga nilikuwa nakwenda kwa I. Kibonge.

Jamaa muhuni muhuni sana, maneno meengi, wakati huo primary anakula fegi mpaka ndumu. Halafu akila ndumu anataka anyonge mwenyewe, ukimnyongea tu lazima anakumind "wewe umejifunza wapi kunyonga vibaya hivi?" Aanakuzodoa.

Kibonge tulipewa makaratasi ya kuchangisha hela za madawati charity walk.

Watu wakazembea hawakuweza kuchangisha.

Kibonge kaipitisha ile karatasi kwa rafiki za baba yake, wadosi wote, kakusanya hela nyingi mpaka karatasi imeisha kaomba karatasi ya pili.

Mwalimu mkuu akamfanya mfano, anasema kuna watu hawajafikisha hata majina matatu, mtazameni mwenzenu Kibonge kachangisha mpaka karatasi imeisha kaja kuomba ya pili.

Tukamuona huyu kibonge noma sana anatufanya tuonekane wazembe.

Mzee Mwinyi alikuwa akikaa kwake pale Oysterbay, akiwa kapumzika, alikuwa anawaita jirani zake mzee Luhanga na Mzee Janguo wanapiga story na kunywa kahawa.

Wazee wamefurahia maisha, yani rais jirani yako, halafu mtu pooa.

Sent from my SM-S908U1 using JamiiForums mobile app
[emoji1]

Ova
 
Duh, wewe ,unataja wau hapo nime watambua ni Warioba ,Malocho , kwa malocho sikuwahi kwenda kwnye party ila Miriam alisha wahi fanya party ya vijana yani ya Ki brazamen na masista doo, ilifanyika kwa kina Manyeng'a yani ili combintiona ya watu wawili ilikuwa yani Sophia na Miriam, enzi hizo tunaiga mambo ya Kimarekani ya House Pary the movie kama zile zilizo fanyika kwa kina Eddy Sapi.

Komanya ni wepi yule Waziri ? nakumbuka aliamia mwisho mwisho kabisa huku Oysterbay ya sisi wa Kongwe na sikumbuki kama klikuaga na zile party.

Mahiga ( balozi) sikujua alikaa Obay, kuna Mahiga kaka yake alikaa Oysterbay Mtaa wa Hill road , Mahga balozi alikaa Obay zamani sana miaka ya late 70.s kabla ya kwenda Canada , sikujua kama alikaa Obay.
Bakilana, sikujua kulikua na Bakilana wengine wa huko Mzinga way, kuna Bakilana wale aliokaa huku kama Kenytatta drive au Kaunda dr na kuna hawa walio kaa Msasani road pembeni ya Oysterbay Primary school ,hao wa Mzinga way siwakumbuki .Mtei ni yupi huyo? nlidhani Obay na kumbuka or najua kila mtu.
Party za Warioba zipi hizo , zile akiwa Waziri mkuu? nakumbuka nilienda paty kama Mbili au tatu , moja sijui ilikua ni birthday ya JUne ,kitu kama hicho , wakiwa wamehamia hapo kwa JUmba la Waziri mkuu ,nili attend hizo ila hazikua nyingi na huyo friend wako wa Geneva ni nani ni ,Simon ? maana Smon alikuwa anakuwepo kwenye party hizo.

Mengi akiishi Msasani Road hiyo longtime sana aisee, hata niko primary school ,hapo Obay , tukikaa kwnye mbuyu pale akipita na Mercedez ndio wana sema wadau huyo mzee ni tajiri Oysterbay Nzima, kumbe uhalisia ni Tajiri Tanzania nzima.

TZA na toyota stoud dah, wachana karibu wote walikua na hizo pick ups ,sijui waliambizana , ilafika wakati , kila familai wana pickup huko obay, matokeo yake wachache tuu ndio wakaw na magari ya ukweli ya vijana kutanulia coco beach ( enzi hizococo beach Jumapili wana jaa watoto wa kishua tuu na kutanuliana mavazi na magari) naw alio tesa na mabari ya ukweli Merrcedez Audi,BMW na kumbuka ni kina Janguoz, Abebez,Yuyu,Mandaraz, Yule jma wa Masaki , walimuuaga Manzese wakidhani ni jambazi, ( nime msahau kina alikua wa Ki Mix wa kiarabu) na wengine wachache nime wasahau kwa hapa.

Ajabu Motie sikumjua kabisa , wala sikuw ahi muona kwnye party zozote za vijana wala coco beach, Motie nime kuja mjua ( Kumuona kwnye kuparty) baada ya kuanza date huyu Seko , tena niliza kumuona Bar One, nilikua na msikia tuu ila kwnye party scenes nilikua simuoni ,s ijui ilikua tuna pishana vipi mpaka nilikua simjui hata ana fananaje, sikumbuki nani nilikua na anz amuona zaidi ni Mdogo wake or Motie .
Abbad Mwinyi hapo nilikua nadhani nilisha Ondoko Bongo , sikumbuki matanuzi yake ila nakumbuka matanuzi ya Abdul Msomali na Albert pia.

Party za kina Eddy Sapi, zilkua kiboko , tulikua tunajiona tuko America kabisa ,kwa jinsi tulivyo kua tuna jidanganya kwa kuiga umarekani kupitia hizo Movies za House Prty .
Wazee wetu Oyesterbay, walikua wana mkosoa sana Mzee Adam Sapi kwa kuruhusu party hizo kufanyika nyumbani kwake, kuruhusu vijana kufanya party bila usimamizi wa wazee.

Kuna siku ilifanyika party hapo the Green,Osyterbay ( Mabembeani) , watu tumesha jiandaa ana kufika hapo , tunakuka mapolice wamejaa na party ime fungwa, kumbe wazee wa Oysterbay wali gundua sijui mnoko gani aliwatonya , basi wazee waka contact Mzee mmoja alikua sijui na cheo gani cha Police anaitwa Mwaitenda (Marehemu) basi akaamuru police wakaja hapo kuzuia party, watu tumesha pigilia Reebok zetu ( High Tops) enzi hizo ndio balaa tena baba kaleta toka UK , tumesha amua wakomesha mabishoo filani ambao walikua wanajiona wanajua sana kupigilia vitu vya Ukweli, ila wao wamevaa FILA sisi tuna Reebok na jensz na Tshirts za Ukweli toka majuu , ilikua tukiingia lazima ugeuke maana enzi hizo viu vya nje ni vichache sana na mpaka mtu Uletewe toka nje ,lasivyo utavaa yuliita "Dar Combined" , yani kila mtu anacho , sasa ujania ilikua ukiingia sehemu unapiga kitu tofauti , uliwakomesha mabishoo fulani fulani, ( Mnajijua kama mna soma hapa ) basi tukatangaziwa hapo kwamba Party hakuna na wote watawanyike kurudi majumbani ,duh, sijui MaDJ ndio walikua kina Abel Siwale (Marehemu) na organizers walikuona Mmoja wapo Franco Mtui (Marehemu), ikawa tafrani tuu , kilammoja hajui nini kifanyike.

Basi watu tukawa so dissapinted , ila kabla hatujaaza kurudi tukasikia wana sema kwamba Eddy Sapi kaenda muomb baba yake tufanyie party kwao, na baba yake kakubali, acha bOnge la shangwe lifanyike ,wote tuka ahamia huko kwa Sapi ( Ilikua party kama ya pili kufanyika hapo) ,ila huw ana shindwa elewa watu ulikua tunapataje taarifa na kulikua hakuna cellphone?, basi Wababa zetu , waka kasirika sana waka kemea vikali Mzee Sapi kuruhusu hizo party kufanyika hapo , lakini wapi tupa piga shangwe mpaka late night.

Beach parties, hizo zilikua za kishua hapo coco beach, hakuna wahuni, ,sijui nani alikuja wa tonya watoto wa Manzese, ikaja kuwa balaa, beach parties zikaja vamiwa na wahuni toka Manzense ( enzi hizo Manzege ni ina wahuni hata Mbagara wanasubiri na Mbagara enzi hizo hata hatuijui na sijui kama ilikuwa na watuw anaishi huko nadhani ilikua pori ) unakuta usiku ziadi ya hata 500 wahuni wakitembea kwa miguu kuja beach Usiku kwnye beach party na ndiopo zikaja acha kufanyika , bila kusaghau zile Pickniks za kibisho , ezi hizo tuna shobo na totoz za Zanaki na Shaban robert.

Miaka ile tumekula maraha sana , wengine tulidhani labda kukulia America tungekuwa na fun zaidi, ila baada ya kwenda US na kuona teenagers wanavyo enjoy life kinamna yao, nikasema Bongo nilikuwa na enjoy zaidi kushinda hawa wa huku maana age ina walimit kwenye mambo mengi sana, Bongo ilikuwa tunajiachia kwa raha zote.
Tuko na majamaa yakishua hatari humu rumba limewapitia mbali tangu uchangani labda wajitakie uzeeni
 
Kwa habari za kuaminika ni kwamba kwenye ile tano MAKONGORO alikuwemo lakini me smile akawalalamikia wazee eti yeye no mwenyekiti ila hana meno akapewa karatasi afanye atakalo !akakata jinai la MAKONGORO akatia la mwezi wa kwanza!!!!

HADI kipipa alishangaa na wazee wengine wa chama!!
😁😁😁😁 Kipipa
 
"Ipi Malecela straight from London" 🤣🤣🤣🤣

"Lemutuz super brand with American spirit '

Daha hizi damu za mzee Malecela dah wapumzike kwa amani.
🤣🤣🤣Mzee nae labda alikuwa hivo hivo ujanani, nasikia alikuwa na mapenzi ya kihindi😂
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mzee nae labda alikuwa hivo hivo ujanani, nasikia alikuwa na mapenzi ya kihindi[emoji23]
Mzee Malecela mwenyewe alikuwa full shobo.

Kwanza mshua anapiga bonge la chain la gold.

Halafu, siku nyingine Jumapili jioni unaweza kuwa unatembea mtaani, mara eeh, unakutana na Waziri Mkuu anaendesha Benz yuko peke yake anazunguka mitaa tu Oysterbay.

Siku moja nimemuona hivyo nikashangaa sana, Mzee Malecela, Prime Minister, anajiendesha mwenyewe mitaa ya Oysterbay karibu na kwake.
 
Kuna mtangazaji maarufu sana wa clous FM alikua anaitwa Vivian alikufa kwa ajali na mchumba wake wakiwa njiani kuelekea kutambulishana huko Arusha.Kuna mtu anakumbuka hii issue?
 
Screenshot_20230704-023802.jpg
 
Complex alikua maarufu miaka hiyo ila sijui huko Dar aliishi ushuani au uswazi
 
Mzee Malecela mwenyewe alikuwa full shobo.

Kwanza mshua anapiga bonge la chain la gold.

Halafu, siku nyingine Jumapili jioni unaweza kuwa unatembea mtaani, mara eeh, unakutana na Waziri Mkuu anaendesha Benz yuko peke yake anazunguka mitaa tu Oysterbay.

Siku moja nimemuona hivyo nikashangaa sana, Mzee Malecela, Prime Minister, anajiendesha mwenyewe mitaa ya Oysterbay karibu na kwake.
Hata Magu alikua anatoka Ikulu na unmarked car kisiri anapiga misere sana tuu , hata Uncle Ben ,JK sitashangaa kama naye alikua anatoka , hahahahaahahahah
 
Hata Magu alikua anatoka Ikulu na unmarked car kisiri anapiga misere sana tuu , hata Uncle Ben ,JK sitashangaa kama naye alikua anatoka , hahahahaahahahah
Dah,

Wazee wali own nchi. Yani hata hawakuogopa .

Yani nimemuona Mzee Malecela anajiendesha mwenyewe kwenye bonge la Mercedes Benz yuko peke yake roundabout ya Mbuyuni ya Karume Road kwenda kwa Mzee Mwandoro huku!
 
Back
Top Bottom