Hatari.
Let me remember all the girls. The streets, the homies, the stories. From my times.
Kuna dada mmoja alikuwa anakaa karibu na lighthouse kule Toure Drive, kwa Jaji Nyalali, alisumbua sana.
Tulikuwa tunakwenda karibu na club ya Wamarekani walikuwa wanakwenda sana kuangalia movies.
Kuna siku nyumba yao ilipigwa na radi, I wonder if it was because of the lighthouse.
I think it was Lulu.
Nilikuwa naenda na mshua nilikuwa mdogo sana. Mshua alikuwa anakaa na Judge Bomani, Judge Nyalali na washua wengine wanakata issues ambazo mimi hata sizielewi wakati huo.
Halafu kulikuwa na Mary Mosha hapa karibu na ubalozi wa Marekani wa Laibon. Alikuwa anasoma Forodhani. Baba yake alikuwa DG wa TANESCO, Mzee Mosha akaamua kuhama pale kwa sababu alisema ubalozi wa Marekani ulikuwa unawaangalia mpaka ndani.
Halafu kulikuwa na the Abebe sisters, Salaita na yule mwingine mdogo wake nafikiri yupo Las Vegas siku hizi. Anaitwa Maisara.
Halafu down the road Laibon kulikuwa na Arthur Lema na mdogo wake Brenda, baba yao likuwa DG breweries. Brenda was hot, but she was like a little sister to me.
Baba yao alivyotoka Breweries alienda kufanya kazi Nairobi for six month akarudi na a flashy red car. Akaenda kuwa DG wa Tanganyika Packers.
Arthur alipelekwa shule Ireland akanywa school fees zote, baba yake akampeleka Los Angeles California. Akasoma akarudi Tanzania kuendeleza mashamba yao.
Ule mtaa wa Laibon kulikuwa kuna nyumba ya Mwinyi, basi siku nyingine tukitoka shule tunakaa kuna kijiwe kona ya Kaunda, tunauona msafara wa Mwinyi anarudi nyumbani, anatupungia mkono.Mwinyi was cool to the kids on the corner.
Siku nyingine Mzee Mwinyi anaalika jirani kwenda kucheza naye bao, kuna mzee mmoja alikuwa anakaa nyuma ya nyumba yake alikuwa CEO wa NBC, karibu na kwa Speaker Adam Sapi Mkwawa, mtoto wake alikuwa rafiki yangu, walikuwa wanaitwa sana kwa Mwinyi kula kashata na kunywa kahawa.
Kuna siku Salama Mwinyi alikuwa ananiringishia sarafu mpya ina picha ya baba yake, nikapiga kofi, a message kwamba I don't care that your father is the president. Akataka kwenda kunisemea, lakini rafiki yake akamwambia huyo Kiranga ni kichaa, ukimsemea ndiyo utazidisha ugomvi. That is how I got away with slapping the president's daughter in the face. I am not proud of that, especially since my philosophy of not hitting women now.
Siku moja nikaamua kuwachemsha tu ubalozi wa Marekani. Nilitaka tu kuingia ubalozi wa Marekani na kuwauliza maswali.
Nikaingia. Kufika getini, yule Marine akaniomba ID, nilikuwa na wallet ina picha ya paka. Akaiangalia, akasema huyu ni paka wako? Nikasema ndiyo. Akafurahi sana. Apparently he was a cat person. Huyo paka hata hakuwa paka wangu, it was a stock photo.
Nilikuwa na documebts za watu wa kampuni za Marekani wanataka watu kutoka nchi za nje waende kufanya kazi Marekani. Nikawa nawaluliza wale watu wa Ubalozi, hawa Wamarekani tutawajuaje kama ni watu genuine au matapeli? Yule Consular wa Ublozi wa Marekani hakuwa na jibu. Kwanza aliniangalia kama haamini nauliza swali lile, inaonekana alikuw ahajapata kuulizwa swali lile na hakuelewa kama nimetumwa na serikali au vipi. Akaniambia atanipa mtu wa kunisaidia. Yule mtu alinizungusha ule ubalozi wa Marekani Laibon mpaka nikajua huyu ananizungusha makusudi nisijue ramani ya jengo. Mwisho wakanifikisha kwa mtu aliyeniambia kwamba Ubalozi wa Marekani Tanzania ni mdogo sana na hauna labor attache, kwa maswali yangu walihitaji nipate majibu kutoka kwa labor attache wa ubalozi wa Marekani Nairobi Kenya, nikapata mambo mengine nikaacha kufuatilia.
Mtaa huo pia walikuwa wanakaa kina Said, Idi, na wakina Janguo wengine.
Idi alikuwa na shobo sana, lakini siku moja alinionesha a very human side of him. Deereva wetu alikuja kunichukua shule, Muhimbili Primary (nilianza Muhimbili kwa sababu ya kukaa Upanga) halafu darasani mwalimu alikuwa katuchelewesha kutoka, yule derava hakujua la kufanya, Idi akajipa jukumu la kuja darasani na kumwambia mwalimu kwamba kuna dereva ananisubiri ameshangaa hatujaachiwa kuondoka darasani, mwalimu akaturuhusu kutoka, kutoka siku hiyo Idi Janguo akawa rafiki yangu.
Mtaa huo wa Laibon nakumbuka kina Chambi Chachage, kina Humphrey Mbise, Salama Mwinyi alikuwa anakuja kwenye nyumba yao ya Laibon siku moja moja, lakini mara nyingi akikaa Ikulu.
Siku moja natoka shule nikakutana na Salim Ahmed Salim akitembea kufanya mazoezi, alikuwa na bodyguars wake wachache tu, akatupa hi kawaida tu..
Kuna binti mmoja wa Adel, I forgot her first name, alikuwa anasoma Jangwani, baba yake alikuwa Permanent Secretary kwenye one of the key ministries, nilikuwa naongea naye sana kwenye simu halafu hanijui mimi ni nani.
Kuna siku tumeenda Ubalozi wa Indonesia kwenye party, kule Coco Beach, nikatokea naongea na mtoto wa balozi anataka sana kujua Kiswahili, alikuwa anasema anataka sana kujifunza Kiswahili, kinafanana sana na lugha yao, kilichofuata hapo sitaki kuhadithia.
Those were the days.