Kifo ni kifo lakini vifo vya wahanga wa ajali hii, looh! Mtu usemeje?
Watu wazima waliokuwa kwenye gari lile waliotoka salama, wanacho nini cha kumwambia nani leo?
"Kwa hakika mtu mzima aliyekufa na watoto wale akipambana kuwakoa alifanya yote yaliyokuwa sahihi."
Hawa watu ilikuwa muhimu kuwaweka katika kumbukumbu zetu kama taifa na kuhakikisha matukio kama haya yanaepukika.
Ni wazi kuwa wengi wenye akili timamu tungekuwa tayari kufa badala ya malaika hawa. Yawezekana ilikuwa ni alfajiri mno na watu wa kuweza kutoa msaada hawakuwa barabarani bado.
Huu uchukuliwaji watoto mapema alfajiri ulikuwa wa kupigwa marufuku. Kama ilivyo kwa magari ya zimamoto, wagonjwa au ya viongozi; magari ya watoto wa shule yangepewa vipaumbele barabarani. Waanze kuchukua watoto angalau 07:00 kukiwa kumepambazuka kabisa.
Barababara za mwendokasi nazo ziwepo kwa matumizi ya magari haya, njiani kwenda mashuleni. Yapo mangapi magari haya, yatatuathiri nini?
Kama taifa kwa kufanya hivi tutakuwa tumejitahidi tulivyoweza japo kuwatendea haki wahanga hawa wakiwa katika mauti.
Wapumzike kwa amani wahanga wa shule ya msingi Ghati Memorial.