Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Mi TTCL washanifungia, nina zote Fiber na Copper, sema haikua kazi rahisi,
Nimewaandikia malalamiko nikatuma kwenye page zao zote za social media pamoja na email yao.

Kama account zao wamezi link na viongozi wa juu ambao taarifa hizi wao hawazijui basi shauri yao.

Wame respond kwenye twitter na email.

Hivi saizi wameniambia survey wanakuja ndio nawasubiri hapa.

Wakizingua na hapa kweli nitawaona wabishi
 
Hahahaha hatari na nusu
 
Hahaha ulitumia njia gani kuwapata hao ttcl? Polee mkuu.
Unawapitia ofisini na kumpigia simu fundi mara kwa mara, tatizo process yao ipo fragmented sana, Survey wanafanya wa marketing, anaeleta waya mwengine, anaeleta router mwengine etc. Nililetewa waya nimekaa nao home mwezi mzima jamaa wa router hajakuja.

Sema jambo moja zuri aisee jamaa wana router kali, nimecheki online bei $300, unaweza kutengeneza wifi zote 2 kwa mpigo 2.4ghz na 5Ghz na zikafanya kazi kwa pamoja, 5Ghz naitumia kustream Wireless Dex kwenye simu perfomance nimeridhika. Hata hizo za 2.4ghz unaweza tengeneza wifi hata 4 tofauti, mtu kama wewe ingekufaa sana hii, unatengeneza wifi yako ya 5Ghz main ya nyumbani speed kubwa na wifi nyengine za wale waooomba omba kila siku password.
 
Akija jamaa wa survey omba namba ya fundi wa waya uwe unamsumbua yeye.
 
Akija jamaa wa survey omba namba ya fundi wa waya uwe unamsumbua yeye.
Mkuu itabidi nifaye hivyo ila nilichokihisi ni kwamba huwenda kuna watu wamefokewa kuhusiana na swala langu

Na ndio maana limejibiwa na wahudumu zaidi ya wawili na utekelezaji nimeanza kuuona muda huo huo

Hivi napigiwa simu kuwa wamefika nikawapokee nitarudi kuweka mrejesho hapa.
 
Enjoy express service mkuu, sometime wanadeserve kufokewa na wao waamke.
 
Enjoy express service mkuu, sometime wanadeserve kufokewa na wao waamke.
Tayari wamekuja na saizi ndo wanasepa.

Niliomba namba ya fundi lakini walichoniambia ni kwamba kuna mfumo ambao ni randomly katika kumteua fundi wakuja kufanya installation

Ipo idara inayojitegemea kwa ajili ya kuteua mafundi hivyo wamedai hata wakinipa namba hawana uhakika kama huyo fundi ndio atayekuja siku ya kufanya installation

Kaniambia kuwa survey wamefanya na wanaeda kuiwasilisha ikafanyiwe tathmini za mahitaji ya vifaa

Akanitajia na jina la ajabu sijui O.B.P.U kuwa ni miongoni mwa vitu vinavyohitajika kwa ajili ya kufunga fiber.

Ila kuna kitu amenichanganya aliponiuliza mimi nimuambie wapi zimeishia nyaya zao za fiber.

Yani yeye muhusika wa kampuni hajui wapi nyaya zimeishia anataka kufahamu kupitia mimi? Nimeshangaa

Ikabidi na mimi nimpe majibu kuwa imeishia mita 200 kutoka hapo japo sina hakika na hayo majibu.

Akaniambia ooh hili eneo lako lipo mbali na waya za fiber kwa hiyo kutakuwa na ugumu kidogo.

Ugumu unatoka wapi wakati serikali ilitangaza kuwa imeingia makubaliano na TANESCO kuwa wapitishe nyaya zao kwenye nguzo zao?

Sasa hapo ugumu unakujaje?

Akasema tutaangalia.

Nikamuuliza kuhusu uhakika wa siku ambayo huyo fundi atakuja kwa ajili ya kufanya installation.

Akasema itategemea na foleni jinsi livyo, kwasababu kuna watu tangu wiki iliyopita tuliwafanyia survey kwa hiyo vifaa vikiwasili lazima waanze wao kupatiwa huduma.

Nikamuambia kama ndio hivyo basi mimi ndio nayetakiwa kuanza kuhudumiwa kwasababu nimeanza kujaza fomu tangu mwaka juzi, so hao watu kivyovyote vile watakuwa wamenikuta.

Akasema poa.

Nikamuambia kesho majira ya saa 8 mchana nitakuoigia simu kukuulizia mrejesho. Akasema sawa.
 
Hiii ipo pia kwa hawa netsolution..waliniambia waziunganishe zote mbili..yaani ulivyoongea ww kama yule fundi aliyekuja nifungia sema nilimkatalia..hii ina option ya 2.4gh na 5g..so akacombine kwa pamojaa ila choice ni yako..basi nitafanya hivi kwa ushauri wako.
 
Pasua kichwa, fundi alienifungia aliniambia hadi mita 300 wanaunga, mimi nimeungwa mita 150, kitachotokea ni speed tu kupungua, mfano kwangu inacheza 16-18mbps
 
Kama unacheza games, unastream vitu toka simu kwenda tv, umefunga home network na server kama za plex etc hio 5ghz muhimu sana.
 
Pasua kichwa, fundi alienifungia aliniambia hadi mita 300 wanaunga, mimi nimeungwa mita 150, kitachotokea ni speed tu kupungua, mfano kwangu inacheza 16-18mbps
Mi hata ije 12Mbps fresh tu

Ila ngoja tu kwanza nikomae nao maana wasije kufanya uhuni wa kukamilisha ratiba waonekane walikuja tu.

Hapo ndio tutafika hadi kwa Chalamila
 
Mkuu shukran, Huyu Dada kaniletea leo. Eneo nilipo lina 4G. Ila inapiga kazi vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…