Enjoy express service mkuu, sometime wanadeserve kufokewa na wao waamke.
Tayari wamekuja na saizi ndo wanasepa.
Niliomba namba ya fundi lakini walichoniambia ni kwamba kuna mfumo ambao ni randomly katika kumteua fundi wakuja kufanya installation
Ipo idara inayojitegemea kwa ajili ya kuteua mafundi hivyo wamedai hata wakinipa namba hawana uhakika kama huyo fundi ndio atayekuja siku ya kufanya installation
Kaniambia kuwa survey wamefanya na wanaeda kuiwasilisha ikafanyiwe tathmini za mahitaji ya vifaa
Akanitajia na jina la ajabu sijui O.B.P.U kuwa ni miongoni mwa vitu vinavyohitajika kwa ajili ya kufunga fiber.
Ila kuna kitu amenichanganya aliponiuliza mimi nimuambie wapi zimeishia nyaya zao za fiber.
Yani yeye muhusika wa kampuni hajui wapi nyaya zimeishia anataka kufahamu kupitia mimi? Nimeshangaa
Ikabidi na mimi nimpe majibu kuwa imeishia mita 200 kutoka hapo japo sina hakika na hayo majibu.
Akaniambia ooh hili eneo lako lipo mbali na waya za fiber kwa hiyo kutakuwa na ugumu kidogo.
Ugumu unatoka wapi wakati serikali ilitangaza kuwa imeingia makubaliano na TANESCO kuwa wapitishe nyaya zao kwenye nguzo zao?
Sasa hapo ugumu unakujaje?
Akasema tutaangalia.
Nikamuuliza kuhusu uhakika wa siku ambayo huyo fundi atakuja kwa ajili ya kufanya installation.
Akasema itategemea na foleni jinsi livyo, kwasababu kuna watu tangu wiki iliyopita tuliwafanyia survey kwa hiyo vifaa vikiwasili lazima waanze wao kupatiwa huduma.
Nikamuambia kama ndio hivyo basi mimi ndio nayetakiwa kuanza kuhudumiwa kwasababu nimeanza kujaza fomu tangu mwaka juzi, so hao watu kivyovyote vile watakuwa wamenikuta.
Akasema poa.
Nikamuambia kesho majira ya saa 8 mchana nitakuoigia simu kukuulizia mrejesho. Akasema sawa.