Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Tunaomba model no ya router waliyokupa, au hata picha yake.
 
Kutokana na speed kupungua leo imenibidi niibuke Morroco HQ kufatilia swala langu na hivi ndio walivyonijibu.

Ni kwamba serikali imekuja na new policy inayowataka makampuni ya simu kuweka limit ya speed kwa wateja wake pindi wanapofikisha idadi fulani ya matumizi.

Kwakua mimi kifurushi changu ni cha 110,000 basi kwa mujibu wa masharti ya serikali ni kwamba matumizi yangu yatapofika 1TB basi speed ita drop kutoka 30Mbps hadi 2-3Mbps

Na kama ningekuwa natumia kifurushi cha 150,000 basi limitation yake ingekuwa extended hadi kwenye 1.5TB baada ya hapo speed ingepungua ila kutokana na ukubwa wa kifurushi chake basi bata speed ingepungua isingekuwa sawa na kifurushi cha 110K

Nimeambiwa ingekuwa 5-7Mbps. Na hivyo hivyo kama utanunua kifurushi kikubwa zaidi utaongezewa idadi ya matumizi na pia speed utayopunguziwa itakuwa ni ya juu kidogo.

Kaniambia kuwa wale wenye vifurushi vya 70K wa 10Mbps ukomo wao naskia ni 500GB na speed yao ikipungua ni chini ya 1Mbps
 
Sasa faida ya hizo backbone za materabyte ni nini? Jisogeze Fiber tu mkuu kama matumizi yako yapo eneo moja.
 
Halotel pia wamezingua?
Halotel ya fiber? Kama fiber ya Halotel bado sijafuatilia.

Ila kama ni ile Router yao basi

Halotel ndio kabisa at least Airtel speed inapungua baada ya 1TB.

Halotel speed yao ni complete mbovu na kwa jinsi nilivyosikia malalamiko ya watu, wengi wanadai baada ya zile 24GB za mwanzo kukata basi hapo ndio speed inapokuwa mbovu.

Lakini pamoja na hayo kifurushi chao hakieleweki kina speed ya kiasi gani kwa hiyo hata kutoa malalamiko inakuwa ngumu.
 
Fiber mkuu, wote voda, Tigo na Halotel wana fiber sasa hivi na naona wamegawana maeneo mengi.

Sema nako pia ulizia usije kuta kuna limit pia.
 
tigo hawana hii huduma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…