Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Hilo nalitambua mkuu.

Ila hiyo majuzi speed ilishuka regardless ya nimewasha vpn au sijawasha.

Toka jana ndo speed imerudi kawaida, ila nikiwasha vpn tu inashuka tena mpaka 2Mbps.

Hiyo inamaanisha wamefusa nyaya mahali.
 
Mkuu ulipoenda HQ uliulizia why speed ilishuka?
Maana hapa nipo nafikiria kununua router kati ya hizi option mbili Vodacom na Airtel, Vodacom niliwahi kutumia sina shida nayo kabisa japo ilikuwa ya ofisini sasa kulingana na usumbufu wa hapa na pale nahitaji kununua ya kwangu na nimeona bei ya Airtel ni nzuri ukilinganisha na Vocadom kwenye upande wa vifurushi.

Je speed yake huwa inabadilika mara nyingi au ndo hiyo mara moja uliyopata 2Mbps maana Vodacom nlikuwa naenjoy sana haijawahi nisumbua speed kwa mazingira ya Kigamboni.
 
Nunua ya Voda .. Airtel Hamna kitu
 
Toka 2023 naitumia hii ya Airtel, na naweza kusema kwa mahali nilipo haijawahi kunisumbua mpaka nikafikiria kuhama.

Kasoro hiyo juzi nilikuwa nimefikia kikomo cha DATA CAP, ambayo nayo nahisi kuna mtu alibonyeza kitufe cha limit ya 500GB kwa bahati mbaya maana inapaswa iwe 1TB.

Ila toka niende hq naona kwa sasa imekaa poa.
 
Wataalamu swali kuhusu hizi Airtel router, hivi eneo ambalo huwa inasoma 5G ila zile bars zinakuwaga mbili na kile kitaa kinavary mda mwengine red mara orange kijani nadra na eneo ambalo inasoma 4G+ na full bars na green colour wapi tunategemea connectivity itakuwa zaidi
 
Komaa kwenye 5G, tafuta eneo ndani ya nyumba ambalo network ipo stable,

Pia unaweza ukafanya majaribio mwenyewe weka 5G pima speed halafu weka 4G nayo pima speed compare download speed na ping.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…