Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

sawasawa, maana natumia halotel(na watu kadhaa) ya 70k kwa 30Mbps ila limit 600GB
 
Fiber yao nzuri mkuu, usisite kufunga kama unaweza.. labda waje wabadilike huko mbeleni si unajua tena hizi kampuni hapa bongo ni unreliable wakati mwingine πŸ˜… zikiwa pressurized tu na mifumo au mamlaka basi zinaanza mauza uza...
TTCL wamepita mtaani kufunga nyaya zao ngoja nitaona niwachukue wao au halotel
 
Nakaa mtaa fulani hivi wa kishua, ni ngumu kumuulza mtu kuhusu TTCL pia sijaona hata mmoja ambae ameifunga, binafsi huwa sijui nyaya ya fiber ipoje.

Halotel niliongea na huyo wakala wao, akasema nimtumie location, nilipotuma hadi sasa yupo kimya. Nafikiria kwenda kabisa ofisini kwao.

Pia mimi internet ni sehemu ya maisha yangu, so ni kulipia walau three months and above, tena kwa hiyo elfu 50 naweza lipia hata minne ikiwa tu hakuna extra charges.

Matumizi yangu ni madogo, na devices ni chache, TV mbili, moja Room na nyingine seblen. Simu mbili na laptop tu basi. Nikitumia simu, basi laptop inakaa pembeni. Nikiangalia TV basi naunganisha TV na simu basi. Ila hiyo speed ya TTCL ya 60mbps ni unyama sana lakini changamoto zao ndio hizo.
 
Unanishawishi ninunue router ya 5G then nisajili hiyo line unlimited ya Voda. Voda nilipo wako poa kuliko mitandao yote. Kwenye simu tu natumia 4G ila mwendo wake ni mzuri sana.
 
Cheif, hivi kuna mafundi wa kurekebisha hizi router? yakwangu zlt x25 imepiga shoti pamoja power bank yake
Kama uchumi wako una ruhusu nunua tu used zimejaa mno mtaani au check FB kule Market Place bei 30k - 40k hapo unapata box ingine...hizo huwa zikiungua zinaunguza motherboard kabisa sio rahisi kuua componet moja let's say capacitor au diode moja moja πŸ˜„ probably hapo power supply lazima iwe imekula mkasi....
 
Nasikia Savanna ni kama voda vile, ni mwendo haswaaaa
Kama kuna fiber imepita kwako mzee we funga tu hata hao Savannah ni wazuri mbona tena 49k unapata 20mbps, ila TTCL Fiber waweke mwishoni ni wasumbufu sana (wawe last option ukiwa huna namna ingine).. Fiber upande wa bando na speed ina nafuu kuliko hayo mabox ya 5G ya Airtel na Halotel
 
Kwa sasa natumia Airtel ya 5G, kwa speed ya 5g sio haba, naweza kustream mechi online bila shida kabisa nikitumia simu. TV yangu haiisomi 5G, so nikistream kwa TV ni changamoto na kwa TV naona ni bora zaidi kuliko kustream kwa simu.

So hapo ndo limeanza kufikiriwa wazo la kupata solution nje ya 5G ya Airtel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…