Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

Hii ni thread ya vifurushi ambavyo sio rasmi kama vya chuo au vifurushi maalum ambavyo vinatoa kiasi kikubwa cha internet, nitalist vifurushi ninavyovifahamu kama kuna wanaojua vyengine watasaidia

Tigo
Kwa Tigo bonyeza *147*00# kisha chagua size yako, unaweza kupata vifurushi vizuri, Ila njia hii sio reliable kwani vifurushi hivyo hubadilika kila Mara.

Vodacom
Vodacom angalia kwenye ya kwako tu, piga *149*03# kuangalia ofa.

Airtel
-Vifurushi vya chuo
Hawa jamaa wana vifurushi vizuri zaidi vya chuo hasa cha usiku ambacho unapata 10gb kwa sh 600, pia kipo cha kawaida unapata 2gb kwa 1000 na 1.2gb kwa sh600. Kuvipata unahitaji kununua vocha za chuo zinazopatikana vyuoni au kutumia airtel money *150*60# kisha uchague ofa kabambe nafkiri option ya 6.

Halotel
-Royal bundles pengine kifurushi kizuri zaidi kwa Sasa kinakupa dakika takriban 200 na Internet unlimited kwa 0.5mbps kwa mwezi mzima. Ni vyema kwenda ofisi za Halotel na kununua line ya Royal bundle, pia unaweza kukuunga kwa kubonyeza menu yao ya *148*66#

-Mega bundle kwa shilingi 10,000 Unapata GB 15 ambazo unatumia mb 500 kila siku kwa mwezi, kujiunga ni *150*88#, unakiunga na salio la halopesa.

-Kifurushi Cha usiku kwa 1000 unapata Internet unlimited, kizuri kwa ajili ya kudownload files kubwa Kama games na movies. Kujiunga *148*66# kisha vifurushi maalum (ya kwako tu)

vifurushi vya 4G kuendana na line zao mpya za 4G,
1000 unapata GB 1 kwa siku
5000 unapata GB 7 kwa wiki
10,000 unapata GB 10 kwa mwezi.

TTCL
-bandika bandua ni vifurushi vizuri kwa matumizi makubwa Kama kuangalia Netflix, zipo option Kama
-1000 GB 4 kwa siku (Mb 500 mchana 3.5GB usiku)
-2500 GB 10 kwa siku
-5000 GB 8 kwa wiki (3gb mchana na 5GB usiku)
Uzuri wake ni kwamba GB za usiku zinaanza saa 2 usiku muda mzuri ambao watu wanaangalia movies baada ya kutoka makazini.

-Toboa Night navyo ni vifurushi vizuri vya usiku in case Halotel kwako inasumbua ama Haina speed, kwa 500 unapata GB 2 na 1000 unapata GB 10.

Vyote toboa na bandika bandua unajiunga kwa kubonyeza *148*30# kisha TTCL bundles.

-Ofa maalum, pia TTCL Wana ofa mbalimbali Kama vile za sabasaba, nanenane etc ambazo wanazieka kwenye option ya vifurushi maalum,
Ntarud hapa
 
Yes nimetest mkuu imesukumaa.msaada nata hii wifi iende mbali kifaa gani kinahitajika mkuu?nishachukua pesa za watu kule wanapata bar moja tu[emoji16][emoji16]
Njia ya bei rahisi tafuta repeater mkuu.

Ama nenda pale Uhuru na msimbazi kkoo kuna mq router ya mtumba kibao, kakusanye kuanzia 5000-30,000 unazipata, Tumia hizo router kusambaza, ukitumia Ethernet baina ya Router na router itasaidia.
 
Hapa mi pia nataka maelekezo ukiwa na router mbili unaweza kukonect kwa pamoja ?
 
Njia ya bei rahisi tafuta repeater mkuu.

Ama nenda pale Uhuru na msimbazi kkoo kuna mq router ya mtumba kibao, kakusanye kuanzia 5000-30,000 unazipata, Tumia hizo router kusambaza, ukitumia Ethernet baina ya Router na router itasaidia.
Shukrani mkuu..mie siye mtaalam wa hizi mambo nisije enda kichwa kichwa nikapigwa labda uniambie pale nikifika nichukue ya namna ipi
 
Shukrani mkuu..mie siye mtaalam wa hizi mambo nisije enda kichwa kichwa nikapigwa labda uniambie pale nikifika nichukue ya namna ipi
Router yoyote yenye wan
images.jpeg-50.jpg

Ukichomeka ethernet wan na wan automatic router inapata internet ni njia rahisi ambayo haina longo longo.

Hata hizo repeater pia.

Sijajua tu bei za ethernet cable kwa mita. Eneo lina urefu gani?
 
Router yoyote yenye wan
View attachment 2741265
Ukichomeka ethernet wan na wan automatic router inapata internet ni njia rahisi ambayo haina longo longo.

Hata hizo repeater pia.

Sijajua tu bei za ethernet cable kwa mita. Eneo lina urefu gani?
Umenichanganya kidogo kaka..ina maana ninunue wire wa ethenet mrefu mpaka kwa jirani au ni umbali kati ya router na router kaka.samahani kwa maswali kaka.
 
Back
Top Bottom