Imebidi nirudi kuangalia USSD menu ya TTCL kwa makini. Hawana lolote, nao ni walewale, lao moja na mitandao mingine kukandamiza wananchi.
Rates zao ni kama mitandao mingine (245MB = sh. 500, na 1GB = sh. 2,100).
Wafanye basi angalau rate iwe 300MB kwa sh. 500. Rate hii angalau itawapa nafuu wananchi. Wananchi wengi hawamudu kununua pocket Wi-Fi na 5G router kwa ajili ya vifurushi vya mwezi kutokana na hali halisi ya Tanzania.
TTCL ilitakiwa iwe mfano mzuri kwa mitandao mingine kama kampuni ya serikali yenye mamlaka ya kiuchumi na mtaji mkubwa. Lakini baadala yake imekuwa mfano wa hovyo. Vocha zake kupatikana shida, network signal inakatakata, comissions kwa mawakala hazieleweki n.k. Kifupi wafanyakazi wa serikali wanafanya kazi kwa mazoea na kutegeana. Wanajua wafanye kazi au wasifanye, mshahara mwisho wa mwezi unaingia.
Baadhi ya kampuni za serikali zimeoza.