Nyalumana originally
JF-Expert Member
- Apr 24, 2019
- 421
- 1,367
Hiyo ni kweli,mwaka 2007 nilikwenda hotel moja jijini Arusha nikiwa na mdogo wangu mimi nikiwa ajirani tena ajira ilikiwa ya maana inayolipa kwa kipindi hicho, dogo langu ambae nae alikuwa amesoma elimu kama ya kwangu akitokea likizo ila alikuwa ameajiriwa kwenye taasisi yenye hali tete.So wakati tunagonga beer tukajikuta tunajumuika na watu mezani kwetu na wakati tunapiga story kumbe kati ya wale kulikiwa na HR wa shirika kubwa fulani Tanzania, kwenye stori ndo akatujulisha kuwa kuna nafasi za kazi shirikani kwao,kucheck vigezo dogo anavyo vyote.Duu akaambiwa kesho aende ofisini akafanye usahili atamsaidia endapo kutakuwa na shida.Hadi wa leo naongea dogo yupo job maisha fresh.Kwa ufupi unakuta kijana kasoma chuo, kakaaa mtaani zaidi ya miaka tano (5) hana ajira, kijana huyuhuyu unamkuta kwa mangi ama kwenye baa za kawaida anafakamia kongagi ama K- vant kupunguza stress.
Sasa ngoja niwape siri ukitaka kufanikiwa mara moja moja tembeleeni hotel kubwa kubwa mfano ( sea cliff ama capetown) kule ukifika nunua bia yako hata moja (Heinekein ama Windhoek) zugazuga baadae jichanganye na wazee wanaofika maeneo hayo.
Trust me! Ukihudhuria maeneo hayo kwa wiki na ikatokea hujapata connection ya maana basi jua una mkosi mkubwa sana.
Nimemsaidia kijana miaka kadhaa ya nyuma na anahudumu katika serikali ya Mama Samia.
Sababu ya kuleta kisa hiki ni kwamba leo kanitumia milioni tano Cash kama shukrani.
So kila nikipitaga maeneo ya Ile hotel naiona ajira ya dogo.
Sehemu kubwa ina mambo makubwa hakika
Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app