Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Duuuh kumbe wanawaibia madoni wa Kariakoo ebwana hio ni hatari zaidi Mkuu, kwa hio Pesa wanapeleka wapi sasa wakibanwa si watoe kwani mpaka wafe?
Una maswali ya kijinga sana,yaani mtu America,uanze kufuatilia na pesa alizoiba kapeleka wapi?
Pesa si kila mtu ana matumizi yake?
Rejea maswali uliyokua unauliza juu,yaani ya kipumbavupumbavu,au we ni litoto liningalijinga?
Unaboa sana.
 
Hio sijaona mkuu sasa wakibanwa si warudishe Pesa za watu kwani ni mpaka wafe hivyo Mkuu Wewe umeiba Pesa ya mtu mwenyewe kashtuka basi akusamehe mrudishie yaishe kwani mpaka akuue Mkuu?
Ahahahahah daah mkuu utakua una tabia za kulea lea sana wewe......

Wanasema usicheke na mtu anaependa ufe njaa au uwe maskini..

Kingine sisi wenye kipato kidogo ndo huwa wazembe sana kwenye kulinda pesa zetu
Ila madoni huko hapana chezea pesa zao...
Mpaka mtu anakutwa na hatia jua kashaanza kula cha mtu hivo kufidia kile alichokula ni lazima akamuliwe utumbo mpana
 
Una maswali ya kijinga sana,yaani mtu America,uanze kufuatilia na pesa alizoiba kapeleka wapi?
Pesa si kila mtu ana matumizi yake?
Rejea maswali uliyokua unauliza juu,yaani ya kipumbavupumbavu,au we ni litoto liningalijinga?
Unaboa sana.
Mkuu Mimi nipo tayari niwe Mjinga ili niwe mwelevu sijui ABC zozote za Kariakoo unaweza niita mbumbumbu wa Kariakoo pamoja na kwamba naishi Dar na nimeishi Dar zaidi ya miaka 35+ Ila mishenitauni za Kariakoo zinazochukua Uhai wa hao wanaopotea sizijui zaidi zaidi labda za wale madogo wauza Simu ndio kidoogo nazijua tena kwa mbali sana
 
Ahahahahah daah mkuu utakua una tabia za kulea lea sana wewe......

Wanasema usicheke na mtu anaependa ufe njaa au uwe maskini..

Kingine sisi wenye kipato kidogo ndo huwa wazembe sana kwenye kulinda pesa zetu
Ila madoni huko hapana chezea pesa zao...
Mpaka mtu anakutwa na hatia jua kashaanza kula cha mtu hivo kufidia kile alichokula ni lazima akamuliwe utumbo mpana
Yaan kashakula Pesa ya watu anaanza kubanduliwa Kucha tena Mkuu? Sasa Pesa inarudi vipi na yeye unamkamua utumbo mpana Mkuu?
 
Unabowa sana, siyo lazima uchangie kila uzi hata usivyovijuwa.

Kariakoo kuna kijana anaitwa tajiri wa wiki mbili, aliaminika dukani watu wakamrubuni akaiba million 200.

Hizi pesa zote alizipata tajiri mwenye mali, kosa lake alifanya mawasiliano na mke wake wakamdaka, kwahiyo jamaa alimiliki million 200 za wizi kwa wiki mbili tu.

Jamaa amemsamehe na amempa million 5 za kuanzia maisha mapya nje yake tajiri yake.

Usiwe unakurupuka tu chai wakati hujui lolote.
Ndio maana tumemwambia huko. Atulie watu washushe madini..
 
Kuna jamaa humu JF aliwahi sema kuwa kuna Warundii walikuwa wanamwagiza mizigo anawatumia kwenye mabasi,walikuwa wanawasiliana nae kwa njia ya WhatsApp sasa jamaa akaingia tamaa akala pesa za Warudi,kumbe jamaa wakawapigia madalali na kuwapa taarifa.Wakamdaka na kumpeleka mafichoni humohumo sokoni,tena anasema yaani pako kama selo vile.
Alichezea kichapo hadi kuna jamaa akamsaidia...
 
Still Kuna maelfu ya vijana waaminifu kariakoo na viunga vyake..

Mfano Mimi leo nimemfuata bodaboda hatufahamiani ndio tumeonana first time nikampa mzigo kimfuko kina thamani ya 500k

Nikamuuliza ana charge Bei gani kuipeleka akasema 3000 Mimi nikampa. 5000

Tukabadilishana namba pia nikampa namba za anae pokea after few minutes ananipigia amepeleka tayar nikampigia jamaa anae pokea akasema amesha pokea..

Kariakoo licha ya kuwepo wizi,ujanja ujanja na utapeli Ila pia Kuna watu waaminifu SANAA
 
Mkuu story yako ni very interesting yaan umefunguka vizuri sana kuna mengine wengi tulikua hatuyajui kwa hio Jamaa wote waliokua wanaiba spea za Magari sasa hivi hawapo tena wamepotezwa wote?
Zaidi ya hao jamaa waliokuwa wananunua mizigo mikubwa ya wizi (sometimes gari hadi tano kwa usiku mmoja) sasa hawapo au waliokuwepo baada ya kuona yaliyowapata wenzao wameogopa kujulikana walichofanya wameji-orginize wanasafiri Dubai wanafunga container la used wakishusha bongo wanagawana.

Sasa wamebaki wanaonunua vitu vidogo vidogo vinavyochomolewa kwenye magari ya watu na mateja na watoto chokoraa kama glasses za side mirror na bumper lamp cover za nyuma za side mirror etc ambao hawana madhara makubwa kiasi hiko,haya mambo yana enzi na enzi mkuu early 90s wakati mimi naingia kwenye fani japo nilikuta ndiyo inaishia ishia kulikuwa na wizi wa vioo vya magari (windscreen) ambapo wewe mmiliki kioo cha gari yako unakinunua huku ukiona kabisa kimeandikwa namba za usajili za gari yako ukileta biashara za polisi kinadondoshwa chini kinapasuka watu wanakimbia halafu sasa ukaagize kioo Nairobi na gari yako unataka uitembelee.

Hii biashara iliisha na kuogopwa baada ya kuibiwa kioo cha gari ya judge sasa wakati wa kufanya biashara na wale wezi mwenye mali akajitambulisha kwa cheo huku amewapanga polisi jamaa wakakimwaga chini kikapasuka mmoja akakamatwa sikumbuki alifungwa miaka mingapi lakini aligeuka kuwa mfano toka siku ile deal likaisha wakahamia kuvunja vunja vioo na kuiba spare mchezo ambao umedumu mno mpaka miaka hii ndiyo kidogo kumekuwa na afadhali.
 
Still Kuna maelfu ya vijana waaminifu kariakoo na viunga vyake..

Mfano Mimi leo nimemfuata bodaboda hatufahamiani ndio tumeonana first time nikampa mzigo kimfuko kina thamani ya 500k

Nikamuuliza ana charge Bei gani kuipeleka akasema 3000 Mimi nikampa. 5000

Tukabadilishana namba pia nikampa namba za anae pokea after few minutes ananipigia amepeleka tayar nikampigia jamaa anae pokea akasema amesha pokea..

Kariakoo licha ya kuwepo wizi,ujanja ujanja na utapeli Ila pia Kuna watu waaminifu SANAA
Kwenye 1000 mwizi ni mmoja au wawili tu kkoo. Na mwizi hachukui round.
 
Zaidi ya hao jamaa waliokuwa wananunua mizigo mikubwa ya wizi (sometimes gari hadi tano kwa usiku mmoja) sasa hawapo au waliokuwepo baada ya kuona yaliyowapata wenzao wameogopa kujulikana walichofanya wameji-orginize wanasafiri Dubai wanafunga container la used wakishusha bongo wanagawana.

Sasa wamebaki wanaonunua vitu vidogo vidogo vinavyochomolewa kwenye magari ya watu na mateja na watoto chokoraa kama glasses za side mirror na bumper lamp cover za nyuma za side mirror etc ambao hawana madhara makubwa kiasi hiko,haya mambo yana enzi na enzi mkuu early 90s wakati mimi naingia kwenye fani japo nilikuta ndiyo inaishia ishia kulikuwa na wizi wa vioo vya magari (windscreen) ambapo wewe mmiliki kioo cha gari yako unakinunua huku ukiona kabisa kimeandikwa namba za usajili za gari yako ukileta biashara za polisi kinadondoshwa chini watu wanakimbia halafu sasa ukaagize kioo Nairobi na gari yako unataka uitembelee.

Hii biashara iliisha na kuogopwa baada ya kuibiwa kioo cha gari ya judge sasa wakati wa kufanya biashara na wale wezi mwenye mali akajitambulisha kwa cheo huku amewapanga polisi jamaa wakakimwaga chini kikapasuka mmoja akakamatwa sikumbuki alifungwa miaka mingapi lakini aligeuka kuwa mfano toka siku ile deal likaisha wakahamia kuvunja vunja vioo na kuiba spare mchezo ambao umedumu mno mpaka miaka hii ndiyo kidogo kumekuwa na afadhali.
Mkuu hii ni very interesting story sijawahi kusimuliwa popote kuhusu habari km hizi kwa kweli umenilisha UBONGO, kwa hio sasa hivi wamebakiza Wizi wa kupasua vioo Ila hapa Juzi Juzi kuna Dogo alifungua uzi humu humu analalamika kaibiwa IST yake na hii inakuaje mkuu emu funguka kidogo ni wa Kariakoo ndio wanapiga hizo deal za kuiba mpaka Magari ya watu au ni wa sehemu zingine?
 
Alafu sio kuokotwa. Wengi wako mahabusu. Tena za mikoa ya mbali. Maana biashara za mikoa ndio wengi huleta ujanja. Achana kabisa na kesi ya upepelezi ya wizi haswa simu au pesa. Ni kesi ngumu sana kwenye maisha ya vijana wa kkoo.
Hapo biashara za mikoa ndio umenifungia komeo Mkuu sijaelewa vizuri unamaanisha deal za mikoa wakipiga wanaleta ujanja mwingi kumbe wanajimaliza wenyewe?
 
Yaan kashakula Pesa ya watu anaanza kubanduliwa Kucha tena Mkuu? Sasa Pesa inarudi vipi na yeye unamkamua utumbo mpana Mkuu?
Yaani ule cha watu alafu ukikamatwa utegemee wakuache ety kisa ukisharudisha cha watu...

Au mkuu upo kukusanya data hapa..
Skiza mi naongea tuu sio kama nina experience ila tuu logically ipo hvo
 
Back
Top Bottom