Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Mkuu hii ni very interesting story sijawahi kusimuliwa popote kuhusu habari km hizi kwa kweli umenilisha UBONGO, kwa hio sasa hivi wamebakiza Wizi wa kupasua vioo Ila hapa Juzi Juzi kuna Dogo alifungua uzi humu humu analalamika kaibiwa IST yake na hii inakuaje mkuu emu funguka kidogo ni wa Kariakoo ndio wanapiga hizo deal za kuiba mpaka Magari ya watu au ni wa sehemu zingine?
Nachelea kusema ni watu wa Kariakoo kwa maana kwamba wezi wa magari mazima mazima huwa hawaji-specify kutokana na maeneo wanakotoka wengi huwa ni madalali yaani anakuuzia gari Dar then anauza ramani kwa wezi wanakuibia kisha wanaenda kuiuza tena Sumbawanga.

Watu huwa wanasema kwa kuhisi (wakati fulani makonda akiwa mkuu wa mkoa hapa Dar) akawa anasema kwamba eti watu wananunua magari ya wizi wanayakata wanauza spare,mfano IST show room currently price ipo juu ya 10+mill so tu-assume mwizi atataka umpe 7mil na wewe uikate kate kibiashara haitakulipa labda uinunue 3mill na hakuna mwizi atakuuzia bei hiyo wakati wapo wakumpa hela nzuri so magari yanayoibiwa tunapishana nayo humu mjini au yapo mikoani huko ila kusema yameuzwa Kariakoo au popote pale ili yakatwe vitu viuzwe kama spare used ni uwongo.
 
Mkuu wala usiogope Wewe funguka tu hakuna ataekwambia umevujisha
Hapana naona kama kuna taarifa unakusanya maana kuna mambo mengine hata kwa hali ya kibinaadamu tu wewe mwenyewe uwezi vumilia.

Mfano watu wanapokamata mwizi mtaani huwa wanamfanya nini...

Haijalishi karudisha hiko kitu au laa ila adhabu/ kipigo pale pale
.

Hivo mambo mengine ni wewe kufikilia tu kama watu juu huko walivyo comment
 
Wengi wanaochangia wamemung'unya sana maneno kiasi asiyejua kinachoendelea hapati clue ya yanayotokea,vijana wanaopotea Kariakoo ni upande wa vitu kama simu laptop na tv na vitu mfanano wa hivyo pamoja na spare za magari.

Mimi nafanya biashara ya spare za magari,nyuma miaka saba nikiuza used kwanza Kariakoo kisha Ilala kule Lindi St so nikizungumza kwa upande huo nawajua vijana pamoja na watu wazima 11 wamepotea toka 2022 hadi leo hawajulikani walipo wa mwisho kwa upande huu walipotea wawili kwa pamoja mwaka jana mwezi wa tano na wote miaka ya nyuma wakati nafanya used walikuwa wanajihusisha sana na kununua vitu vilovyokuwa vikiibiwa kwenye magari ya watu wenyewe wakiita ”full",yaani gari inavunjwa kioo wanatoa lock wanachukua kuanzia dashboard show p/window switch radio side mirrors headrest nje wanang’oa taa zote bumpers nyuma na mbele kama mmiliki alisahau chochote cha thamani wanabeba so hawa jamaa walikuwa wanakaa pale mnada wa spare ulioungua moto nyuma ya Big Born p/station.

Jamaa walikuwa wanakula na askari wa Msimbazi na Central wakati fulani Mambosasa akiwa mkuu wa police Dar akalivalia njuga kwa kuwapa kitu kama offer (maana walikuwa wanajulikana kote police Msimbazi Stakishari Central Mabatini kwamba ndiyo wanaodhamini biashara hiyo hata picha zao zilibandikwa kutani) kwamba kuanzia pale hawana kesi ila wakiri kuacha mara moja mchezo huo kwani option iliyokuwa ifanyike baada ya kudhihirika wanaendelea na kazi hiyo ni kupotezwa moja kwa moja na kwamba jeshi la polisi halitakuwa na muda wa kwenda kutoa maelezo mahakamani,kilichoendelea wanakijua wenyewe baadae walipovunja hicho kiapo ndiyo wakapotea.

Baada ya hii ambush ndiyo matokeo tunayoyaona sasa wizi ule umepungua kama siyo kuisha kabisa nadhani hata Agrey baada ya wale watano kupotezwa kuna mabadiliko.
Ndivyo ilivyo. Askari wanajua issue nyingi, ukipewa onyo ukakaidi utapata tamu yako.
 
Una maswali ya kijinga sana,yaani mtu America,uanze kufuatilia na pesa alizoiba kapeleka wapi?
Pesa si kila mtu ana matumizi yake?
Rejea maswali uliyokua unauliza juu,yaani ya kipumbavupumbavu,au we ni litoto liningalijinga?
Unaboa sana.
😃😃😃😃😃😃
Mkuu mvumilie tu huku tupo watu tofauti tofauti
 
Kama inakuja inakata, kuna dogo kijijini kwetu alikuja huko Dsm nahisi kuuza hiyo mizigo ya matajiri, mwaka mmoja akarudi home na ukwasi, akajenga nyumba chap ndani ya week akaezeka. Week ya tatu akaanza kuumwa na kufa haraka haraka.

Tukazika tukasahau
 
Huyo Lethergo sijui hiyo miaka 35+ kakaa dar ipi..
Ana maswali ambayo hata mtu ambae haijui dar kabisa hawezi uliza ..
Mkuu tulia kuna namna ya kuuliza maswali ili upewe full story sio nyinyi mnauliza maswali mnamix na matusi au hujaona Jamaa ananielewa na ananisimulia A to Z au hamtaki nijue nyie Jamaa ni watu wa ajabu sana, kila mtu ana namna yake ya kuuliza maswali sio lazima tufanane hujapenda namna yangu ya kuuliza maswali acha kusoma ninachokiandika
 
Back
Top Bottom