Uchaguzi 2020 Vijana kuweni makini kwa ahadi za uongo kutoka Vyama vya Upinzani

1.ewe ni nani hata utufokee vijana?

2. Mageuzi ndani ya chama yanatuhusu nini sisi?

3. Mambo ya Misri usituambie kabisa

4. Hakuna anayesema kutakuwa na ajira 100%, mmefanya mambo ya ovyo yaliyopelekea kupungua kwa ajira

#USITUFOKEE
Kabla ya uhuru tanganyika ilikuwa imeendelea kuliko japan mavijana hayahaya yakadanganywa yakachagua tanu miaka mitano badae tulikuwa masikini wa pili duniani nyuma ya bangladesh, leo tumefika uchumi wa Kati yameanza tena kudanganywa,

Mwaka 1954 chama Cha Nationalist ndio kilikuwa na sera nzuri hawahawa vijana wakadanganywa na mwalimu wa form two.
 
magufuli ni bonge la rais kuwahi tokea tanzania bt kinachomponza zaidi ni ile team maslahi ndani ya ccm, hawa mabwana maslahi yao yalipominywa wamekua na chuki za wazi wazi na ndo watukanaji wakubwa wa magufuli mitandaoni, hawa ndo wanachagiza kuupa nguvu upinzani ulojifia.
 
Vijana wawemakini na ahadi za uongo za wagombea ,sikilizeni na chambueni,huwezi tafuta ufafanuzi was kilichozungumzwa
 
Tatizo wakishajiona wao wapo kwenye mifumo rasmi basi wanasahau kilakitu juu ya wengine hilo ndio tatizo kubwa
 
Pamoja sana Mkuu! Umesema vema.
 
Acha kudanganya wewe. Uko zama gani wewe? Viwanda vya zama hizi siyo labour intensive kwasabb ya kukua kwa teknolojia.

Wewe unapuyanga, I have all, the knowledge, skills and expertise in the field.

Kama huelewewi kaulize kuanzia ground at gin stands to a finished product ......what it takes forgetting about cotton farming, sells, transporting seed cotton, loading etc.
 
Wakubwa huwa hawadanganyi,sasa inakuwaje wewe ni mkubwa halafu unadanganya?
 
Tatizo wakishajiona wao wapo kwenye mifumo rasmi basi wanasahau kilakitu juu ya wengine hilo ndio tatizo kubwa
Hapo ndipo kwenye matatizo zaidi has hizi siasa za kusifiasifia zinamfanya kiongozi kutokuona kuna mahali penye shida.
Hili la ajira sio la kubeza kabisa kwani tulishughudia yaliyowapata Tunisia na ukifuatilia kwa umakini tatizo lilikuwa ni ajira.
 
UZWAZWA nao ni KIPAJI. Eti huyo anayejiita kichaa kaleta mageuzi makubwa. UPUMBAVU Nchini unazidi kushamiri kwa kasi ya kutisha. Mxiewwwwwwwwww!


 
Milioni 50 kwa kila Kijiji ahadi hiyo ni nani ALIYETUTAPELI, ili tusimpe nafasi hiyo tena?
 
Naona Umeandika Upuuzi mtupu. Hivi unadhani ukidanganywa kwamba Madaraja na ununuzi wa ndege hauna manufaa kwa watanzania kwa sababu watanzania hawana uwezo wa kupanda ndege unaacha kuwaza nje ya box kwamba kazi ya ndege ni kutuingizia fedha za kigeni zitakazopelekea wewe na watoto Wako kuhudumiwa na Serikali yako hata hilo hujui?


Barabara na madaraja visipojengwa nani Atakubali kupeleka. Chombo chake kubeba mazao kwa gharama nafuu?

Je!unajua kwa kukosa miundombinu bora ndiko kunakochangia Mfumuko wa bei? Hivi hata kama ungekua na fedha mfukoni kwa kutokuwekeza kwenye miundombinu hata hiyo PESA hisingekua na thamani kwako.

Sidhani kama wewe ulikuwepo wakati nchi hii imetoka kwenye utawala wa mkoloni. Tuulize sisi tuliokuwepo ndugu ndio tutakusimulia shida na Hadha tuliokua tunaipata.

Nyie mmezaliwa juzi mmekuta CCM imefanya kazi kubwa kuboresha nchi hii Leo unatumia Smartphone kutukana serikali? Hujui CCM ilipoitoa nchi hii KIJANA.

Leo unapanda gari unaenda kila maali kwa wakati sisi tulikua tunakesha kutoka mkoa 1 kwenda mwingine nyie mmekuta Neema mmevimbiwa na kutukana.

Ni mjinga tena lofa Atakae sema Serikali ya chama cha mapinduzi haijafanya kitu kwenye nchi hii.
 
Ccm imefanya kazi kubwa ipi?

Unasema ulikuwepo enzi za wakoloni, je hao wakoloni hawakua na ndege, wahakujenga barabara, hawakujenga reli? Leo hii miaka 60 bado tunakuja kuambiwa eti reli ni maendeleo, basi wakolni walishayaleta zaidi ya miaka 60 iliyopita kama hayo ndio maendeleo.

Miaka 60 ya uhuru bado serikali inazungumzia ndege, barabara, reli huku watu hawana huduma za afya, hakuna maji, hakuna madawa, hakuna wauguzi, hakuna madawati, hakuna madarasa, eti ndege na barabara.

Ccm kwa miaka 60 ilichokifanya kwa Tanzania ni sawa na kijana wa miaka 25 kufanya matendo au mambo ya mtoto wa miaka 3, kuchezea kinyesi chake, kuchezea mkojo, kula matope. Huwezi kusema huyo kijana wa miaka 25 anaefanya mambo ya mtoto wa miaka 3 kua amekua.

Mimi kutokuwepo huko nyuma bado hakuondoi ukweli kua hakuna kitu ccm imefanya kwa nchi hii zaidi ya kuwafanya raia waendelee kua fukara wa kutupwa.

Wazee kama nyie wenye mawazo ya hovyo ndio bado mnasababisha hii nchi kuendelea kua masikini.

Wazungu huwema age comes with experience and wisdom but sometimes age comes alone, wewe age came alone.(kwa kiswahili hata wajinga huzeeka).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…