Naona Umeandika Upuuzi mtupu. Hivi unadhani ukidanganywa kwamba Madaraja na ununuzi wa ndege hauna manufaa kwa watanzania kwa sababu watanzania hawana uwezo wa kupanda ndege unaacha kuwaza nje ya box kwamba kazi ya ndege ni kutuingizia fedha za kigeni zitakazopelekea wewe na watoto Wako kuhudumiwa na Serikali yako hata hilo hujui?
Barabara na madaraja visipojengwa nani Atakubali kupeleka. Chombo chake kubeba mazao kwa gharama nafuu?
Je!unajua kwa kukosa miundombinu bora ndiko kunakochangia Mfumuko wa bei? Hivi hata kama ungekua na fedha mfukoni kwa kutokuwekeza kwenye miundombinu hata hiyo PESA hisingekua na thamani kwako.
Sidhani kama wewe ulikuwepo wakati nchi hii imetoka kwenye utawala wa mkoloni. Tuulize sisi tuliokuwepo ndugu ndio tutakusimulia shida na Hadha tuliokua tunaipata.
Nyie mmezaliwa juzi mmekuta CCM imefanya kazi kubwa kuboresha nchi hii Leo unatumia Smartphone kutukana serikali? Hujui CCM ilipoitoa nchi hii KIJANA.
Leo unapanda gari unaenda kila maali kwa wakati sisi tulikua tunakesha kutoka mkoa 1 kwenda mwingine nyie mmekuta Neema mmevimbiwa na kutukana.
Ni mjinga tena lofa Atakae sema Serikali ya chama cha mapinduzi haijafanya kitu kwenye nchi hii.
Ccm imefanya kazi kubwa ipi?
Unasema ulikuwepo enzi za wakoloni, je hao wakoloni hawakua na ndege, wahakujenga barabara, hawakujenga reli? Leo hii miaka 60 bado tunakuja kuambiwa eti reli ni maendeleo, basi wakolni walishayaleta zaidi ya miaka 60 iliyopita kama hayo ndio maendeleo.
Miaka 60 ya uhuru bado serikali inazungumzia ndege, barabara, reli huku watu hawana huduma za afya, hakuna maji, hakuna madawa, hakuna wauguzi, hakuna madawati, hakuna madarasa, eti ndege na barabara.
Ccm kwa miaka 60 ilichokifanya kwa Tanzania ni sawa na kijana wa miaka 25 kufanya matendo au mambo ya mtoto wa miaka 3, kuchezea kinyesi chake, kuchezea mkojo, kula matope. Huwezi kusema huyo kijana wa miaka 25 anaefanya mambo ya mtoto wa miaka 3 kua amekua.
Mimi kutokuwepo huko nyuma bado hakuondoi ukweli kua hakuna kitu ccm imefanya kwa nchi hii zaidi ya kuwafanya raia waendelee kua fukara wa kutupwa.
Wazee kama nyie wenye mawazo ya hovyo ndio bado mnasababisha hii nchi kuendelea kua masikini.
Wazungu huwema age comes with experience and wisdom but sometimes age comes alone, wewe age came alone.(kwa kiswahili hata wajinga huzeeka).