Vijana Kuweni na Busara hata Kidogo

Vijana Kuweni na Busara hata Kidogo

Jana jioni nilikuwa nafanya mazoezi(jogging) nikapita barabara moja kuna ghorofa linajengwa.

Nikasikia kijana mmoja (27-30yr) anafoka na kutukana kwenye simu.
'WEWE MZEE SIKU YA PILI LEO NAFIKA HAPA UMEACHA LINDO. HUO UZEE WAKO MIAKA 70 ISIWE KIGEZO KUTUSUMBUA. KAMA ULITUMIA HELA ZAKO VIBAYA UJANANI USITULETEE... Duh nilishtuka sana nikaishia zangu.

Aisee inawezekana kweli mzee kakosea ila kuna njia nzuri ya kuongea na mtu mzima au mfanyakazi wako na sio lugha kama hizo. Kijana mdogo namna ile kumtukana mzee ambae anaweza kuwa baba au babu yake si sawa. Kuna laana nyingine za kujitakia. Vijana kuweni na busara.
Shida unataka busara kwenye pesa za watu.Nahisi kama busara zingetumika kwenye teknolojia leo usingekuwa kwenye JF wala internet na gari ya passo.
 
Jana jioni nilikuwa nafanya mazoezi(jogging) nikapita barabara moja kuna ghorofa linajengwa.

Nikasikia kijana mmoja (27-30yr) anafoka na kutukana kwenye simu.
'WEWE MZEE SIKU YA PILI LEO NAFIKA HAPA UMEACHA LINDO. HUO UZEE WAKO MIAKA 70 ISIWE KIGEZO KUTUSUMBUA. KAMA ULITUMIA HELA ZAKO VIBAYA UJANANI USITULETEE... Duh nilishtuka sana nikaishia zangu.

Aisee inawezekana kweli mzee kakosea ila kuna njia nzuri ya kuongea na mtu mzima au mfanyakazi wako na sio lugha kama hizo. Kijana mdogo namna ile kumtukana mzee ambae anaweza kuwa baba au babu yake si sawa. Kuna laana nyingine za kujitakia. Vijana kuweni na busara.
Nikweli kabisa familiar, laana zingine ni za kujitakia, ukicheki kwa maisha yetu ya Kitanzania Mzee wa kimaskini kufika umri wa miaka 70 au 80 akiwa na afya ningumu sana usikute Mzee wawatu alikuwa anaumwa daaah.
 
Hamna laana,ingekuwa hivyo kila mahali kungekuwa balaa maana hakuna mtu ambae hajawai kukorofishwa.
 
Back
Top Bottom