Vijana mliomaliza vyuo kwanini mnavuta bangi?

Vijana mliomaliza vyuo kwanini mnavuta bangi?

Mkuu; Hapo ndo patamu. Hivi unathubutuje kujipa jukumu la kumkanya kijana asijiingize huko? Unapenda utukanwe na vijana mchana kweupe? e.g hebu soma comment #2,3,5 n.k.
Halafu ingefaa ulione hili tatizo kwa mapana yake. Halipo specific kwenye bangi, madawa ya kulevya au vijana tuu. Ni multi-sectoral issue. Wazee, ambao ndo ilitegemewa wawe ndo watoa miongozo na wadhibiti wa Nidhamu cku hizi wamejivua jukumu hilo na wanasema "Acha wafu wazike wafu wao...... Haliwahusu" Serikali ambayo ndo # 1 kuhakikisha mustakabali wa Ustawi wa Jamii ndani ya nchi, yenyewe imejitoa ufahamu na kuachia mambo yaende kama yanavyoenda - Hakuna uwajibikaji hata ule wa saizi ya punje ya haradali.
Wananchi kwa ujumla wao (watoto, watu wazima na wazee) wanakula vitu fake mitaani hadi mafuta ya Transfoma, wanapata madawa substandard / fake huko hospitali, pharmacies vipimo fake maabara n.k. Serikali imejikita kwenye kukusanya(Maokoto) bila kumjali huyo anayetozwa, Uwepo wa nishati e.g. umeme ili kuwezesha utendaji n.k.n.k. ... yupo mwandishi mmoja alishindwa kuendelea kufikiri zaidi akaishia kusema tazama kila kitu "ni Ubatili mtupu...." Biblia, Mhu. 1:2.
Kwahiyo unasubiri hadi mwanao awe kijana mkubwa ndo uanze kumkanya?
 
Back
Top Bottom