Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Kuna jamaa tulikuwa naye PCM aisee balaa; tangu form five sikuwahi kuona anaandika notice; yeye alikuwa na makaratasi tu anaandika mambo yake mwingine huelewi kitu. Hasomi kazi yake ni kuzunguka kwa room za wenzake kupiga soga. Ukishidwa swali nenda kwake anaku solvia fastaa ka machine; jamaa aliondoka na point tatu.

Akili inatokana na genetic ya ukoo; hizi zetu za kuungaungaa aisee unahangaika sana.
 
Ndo maana nikiona mtu anaandika mambo ya hovyo humu nachukulia poa kua ni lifestyle yake aliyochagua.
Huyo mzee kanikumbusha yule bibi tuliokua tunachat nae kule Kapuku forum huku tukimwita bebi/mrembo/mchumba etc..
Jf ni Imaginary world
yaani huko nako ni balaa, bibi mwenye wajukuu wake but alikuwa na nidhamu sana
 
Last week nilikua napitia matokeo ya madogo wa form six kwa Special Schools (Mzumbe, Tabora Boys, Kibaha na Ilboru) lengo ni kuhesabu One za Tatu yaani ni za kutafuta kwa tochi... Nimeambulia kuona moja tu ya dogo wa Mzumbe alokua T.O (dogo mwenyewe PCB, sijui PCM siku hizi wamerogwa na nani).

Huu ni ushauri kwa madogo ambao mpo Advance na mna munkari wa kupiga One Kali tatizo hamjui strategies zipi mtumie. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma sana na kufaulu. Kusoma sana sio kufaulu, bali kusoma kwa technique.

Mbinu nilizotumia kupiga One ya 3 bila kukesha darasani:

Target Audience:
Wanafunzi waliopo Advance (five na six) hasa PCM (shule za Private hawahusiki sababu wana walimu na miundombinu ya kutosha)

Malengo:
Weka malengo ya kupiga One Kali. Yaani kila somo lisome ukiwa na mind za kupata A. Ukijiwekea malengo ya kupiga A lazima utakua unasoma kwa focus.
Mie wakati naingia form five nikaweka malengo kuwa lazima nipige one ya 3 na niingie Top 3 kitaifa. Na ikawa hivo mwisho wa siku.

Timetable:
Sikua na fixed (defined) ratiba kama wenzangu walivokua wamebandika ndani ya matranka yao au ukutani pembeni ya kitanda. Mie nilikua nasoma kwa mood.
Nilikua na alternate kati ya Physics na Chemia. Napiga maswali ya Gravitation nikichoka nafunga kesho napitia Inorganic Chemistry.

Hesabu nilikua napitia kila siku nikitaka kulala (somo la kulalia). Mfano nikitoka class kupiga maswali ya Electronics narudi Dom nafungua pure II napiga maswali yangu 20 ya Complex Number then nalala.

Kuna wakati najikuta nasoma Physics hata week nzima (mfano napoamua kupitia Mechanics), yaani kifupi sikua na ratiba fixed, nasoma kutokana na nataka nikave topic zipi kwenye somo husika.

Achana na tabia ya kusoma kwa ratiba, soma kulingana na somo lipi topic ipi upo nyuma sana. Topic ipi hujapitia maswali mengi, topic ipi umeanza kusahau. Lazima upige One ya 3.

Kabla sijasahau: Mie usiku mwisho wangu kusoma ilikua saa nne. Mchana ndio muda wangu wa kupiga kitabu, giza likiingia tu basi nakua zoba. Usually ikifika saa tatu usiku kama sijaenda prepo basi siendi tena, napitia hesabu kitandani nalala.
But mchana hunikuti nafanya upuuzi (labda jioni kwenye jogging uwanjani).
Lazima upige One ya 3.

Twende kwenye masomo husika sasa:

Physics:
Vitabu nilivosoma mpaka napiga pepa: (Chandy, Nelkon na Roger Muncaster).
Katika somo unalotakiwa upitie vitabu vingi ni Physics. Lakini mie nilikua mjanja. Nilipitia vitabu ambavyo NECTA wanapenda kutoa maswali basi. Vingine nikaachana navyo.

Nilianza na Chandy, then nilipo kimaliza nikaja Nelkon (hiki hata sikusoma, bali nilifanya maswali yote ya mle sababu hakina maelezo mengi). Then form six mwishoni nikamalizia Roger (japo kina maswali magumu, nilijitahidi kufanya, yaliyonishinda nikaachana nayo)

Ukitaka kuelewa Physics basi soma Chandy (wahindi wanaeleza mpaka una enjoy), but ukitaka kufaulu Physics NECTA piga maswali karibu yote ya Nelkon na Roger Muncaster. NECTA wanapenda kutoa maswali kutoka kwenye Nelkon na Roger.

Practical za Physics zote nilifoji wakati wa pepa. Ukijifanya kupiga practical real hutomaliza muda hautoshi. Ukikaribia NECTA jifunze namna ya kufoji practical za Mechanics, Heat na Umeme.

Lazima upige One ya 3.

Chemistry:
Katika masomo yaliokua mteremko kwangu basi ni Chemistry. Kwanza kabisa ndio somo ambalo sikuwahi kabisa kusoma Vitabu. Niliishia kusoma Notes tu pamoja na kupitia Past Papers za NECTA.
Yaani nilikua nashangaa watu wanakomaa kusoma Ramsden usiku wa manane wakati Chemia ni mwendo wa notes tu unapiga banda. Practical zake ndio chai kabisa.

Kifupi ni kuwa ukitaka kupiga banda la Chemia with minimum efforts fanya hivi:
Soma notice za topic husika (mfano Electrochemistry), ukishaelewa chukua Review ya NECTA, pitia pepa moja baada ya nyingine kwa topic (achana na tabia ya kupitia pepa zima matopic yote utaloose concentration, nenda topic by topic).
Ukimaliza rudi tena kwenye notice, soma topic nyingine (mfano Organic) then njoo tena kwenye Review, fanya hivo hivo. Hadi umalize topic zote.

Practical za Chemia zote nilifanya real, sikufoji hata moja. Sababu praki za Chemia ni simple, sinafanyika ukifata procedure. Kifupi Chemia hutakiwi kukosa A au B+. Mie nilipiga A kali nikaongoza Chemia kitaifa form six yetu. Watu wamekomaa na mavitabu nikawakimbiza kama kawa.
Lazima upige One ya 3.
View attachment 818007



Advanced Mathematics:
Katika somo ambalo nilikua nasomea kitandani ni hesabu. Kwanza kabisa sikua na ratiba maalum ya kusoma hesabu. By the way hesabu hatusomi, bali huwa tuna solve.
Nilianzaga kukomaa na Tranter kubabake kikanishinda. Nikaachana nacho.
Nikakomaa na Pure I na II nikakomaa nazo na sikuwahi kusoma kitabu kingine chochote zaidi ya hivi viwili.
Style yangu ile ile, nasoma topic (mfano Integration) then nazama kwenye NECTA Review napiga maswali yote ya Integration mpaka yaishe. Nikimaliza natafuta another topic hivo hivo.
Lazima upige One ya 3.

Mwisho Kabisa:
Watu wanaamini kuwa ili ufaulu masomo ya sayansi kwa One kali lazima uende ukapige mapindi kwa tuition center za Dar (Mgote, Moody, Mtiga, Mbuga etc).
Hilo sio kweli, sio kweli, ni uongo.

Mie sikuwahi kusoma tuition yoyote Dar. Nilipiga mapindi ya vichochoroni tu.
Mengine tulifundishana na wenzangu shule. Na topic zingine niliamua kusoma mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kunifundisha (mfano Modern Physics, Static Electricity, Complex Numbers, Statistics).

Vijana acheni kulala, wekeni malengo ya kupiga One kali ili inapofika stage ya kuomba vyuo unak ua na wide selection ya kwenda chuo na course unayotaka.
Lazima upige One ya 3.

View attachment 818008
Dogo, thid is one of the best advice i ever come across, huu ushauri wako madogo wakiufuata watafika mbali sana,

Achana na hao wanaopenda kukosoa kila kitu, by the way, naamini uko mbali sana zaidi yao kiakili, so stop arguing na hao watu for no reason, you are just wasting your precious time.

Mimi ningepata this kinda advice wakati nasoma A -Level, nadhani ningepata 1 point 3, ingawa nilifaulu vizuri sana PCM ingawa nilitumia guvu zaidi na kupata scholaship ya kusoma nje na kupata Degree yangu ya kwanza ya Engineering.

Hayo uliyoandika yanadhihirisha how brilliant you are, na ndio una demonstrate wewe kuwa asset, kwamba unatumika kuongeza value kwa wadogo zako waweze kufaulu vizuri.
 
hata chuo sijafika.. ila maisha nayoishi ni wachache sana wameyafikia.. mimi hata a level sijasoma.. niliishia o level tu then college ya kizushi kisha nikazama mtaani.. karibu sana tupambane kitaa.. huku hakuhitaji A za physics bali ni kujua kuusoma mtaa

I can feel your pain.. Pole mkuu ndio maisha.
 
What an inspiring, motivational thread! I am sure this will be of use to those "A level students" who are serious with their education. Good job CCNP Engineer !

Kindly ignore those losers who attacks you with their cheap comments simply because they didn't make it to the top. What they have written reveals their jealous and hatred towards the learned! Don't argue with them, let them spew their venom of ignorance and stupidity.
 
Halafu nimegundua waliofeli wengi wako inferior, always wanakuja kuwatafuta waliofaulu shule huko mbele ya safari ili tu wajikompee. Ila huyu jamaa sijui malengo yake yalikua nini lakini kwa ufaulu wake angepata mwongozo akaomba scholarship USA au EUROPE angezamia huko huko kwa kukimbiza. Anyway kila mtu na maamuzi yake.
 
sijaponda wasomi nimekuponda wewe mpuuzi uliyeshindwa kutumia ma AAA yako kujikomboa na ukaishia kuajiriwa na serikali kwa TGSE..

mwisho wa siku umetapeliwa na dogo ontario.. huwezi ku reason pamoja na ma AAA yako yote..

mtu aliyefaulu kama wewe kushindwa kujitambua mpaka unafikiria kukopa bank milion 5 na ukimbie nazo bila kulipa ni mpuuzi..

Ushauri: Mimi mwajiriwa Serikalini, nataka nichukue mkopo (kwa kutumia ajira yangu) kisha niache kazi

wenzako wajanja waliopata hayo ma A yako walijua ku reason .. wakaachana na coet wakaenda udbs na Baf mzumbe.. wakamaliza wakaingia big 4 proffessional firms... then wakaingia kwenye ma bank vitengo nyeti wanakula salary hela zaidi ya ulizotaka kukopa na kuzulumu bank..

wengine wakalamba ma scholarship ya ukweli na kusepa bongo na kazi wanafanya majuu..

wewe ni mpuuzi ndio maana unapata tabu sana... jifunze kuusoma mtaaaa
[emoji23]hapo kwenye kutapeliwa unanichekesha sana
Kweli jamaa alizingua

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Yaani watu waliofeli shule wanajifanyaga wote wamefanikiwa maisha mtaani na kuona waliopiga shule wamepoteza muda hawana mbele wala nyuma.

Wakati nina rafiki zangu kibao tu nilosoma nao walifeli na maisha yao mpaka leo hii magumu tu, lazima afanye kazi kila siku masaa 16 apate mkate wake.

Ukweli ni kuwa, wanaponda tuliofaulu ili kupunguza maumivu ya KUFELI na kujiweka sawa na sisi.
Kama hukutaka shule usingeenda kabisa, ungesubiri ukue tu uingie kitaa tuone.

Ha ha ha ha,,, Jamaa punguza kusema ukweli basi
 
Kwa hili utakuwa umemchoma kwa kiasi fulani wajanja wengi walienda kusoma course za biashara nje ya nchi tena vyuo vikubwa kubwa tu......

Labda bwana Engineer hapa aliona kusoma UDSM ndio atakuwa ameyamaliza maisha but all in all huwezi mlaumu labda ana malengo yake binafsi ila kwa performance yake atakuwa anakula pesa nzuri......
Nna jamaa yangu alikuwa TO ila yuko kitaa magomeni kapanga chumba kimoja akipiga mapindi. Kusoma na kupata maksi kubwa bila kuwa na akili za kitaa utaishia kunung'unika moyoni ... AAA zisizokusaidia ni kazi Bure
 
Sijui kwa nini umeamua kubisha na watu wenye akili ndogo mkuu, Sisi wengine ni member wa professional site kama stackoverflow kule kuna criteria za mtu kuchangia sio kile mtu anakua na iyo priviledge so huwezi kukuta upumbavu kwenye vitu positive. Kudos lakini naona umefuata njia ya mengi kureveal the thruth japo mara nyingi hua sio kweli kwa uzoefu wangu.
Kwaio kabla ya kuchangia wanakuuliza umepata A ngapi A level na O level au chuo una GPA ya ngapi au?
 
Daah umenikumbushana mbali sana aisee, ile Organic chemistry nilikua kila nikisoma haikai kichwani, Advanced mathematics ilikua rahisi tuu kwangu, Chemistry daah
All in all nashukuru mungu leo hii ni Civil Engineer ingawa necta ilikua tofauti na mock, mock nilipiga 1 point 7 , necta sasa [emoji28]
 
Uzi huu umenizibitishia ambavyo hekima bila noti, uishia kuzalauliana.

Mleta mada, kwa namna yoyote ile ni kijana smart upstairs.

Kwa nchi za wenzetu vipaji Kama hivi ni lulu na ni asset kubwa na utazamawa kwa jicho la hekima hata kama hana hela.

Ubora wa mtu hauko kwenye uwezo wa kuwa na gari kali au kuishi kwenye mjengo wa maaana

Context za maisha yetu hutofautiana, likewise hata destiny za maisha yetu

Siku za hivi karibuni kuna watu wanaojiita wana elimu ya kitaa na wana make bingo ya maana, hali inayopelekea hata just discourage wasomi.

Kwa bahati nzuri kundi hili ukiri wao ni watu wa mishe, frankly speaking wengi ni watu wasio heshimu maadili, kila aina ya dili regardless itamtaka kuiba, kuua, na hata kufanya ushenzi wowote kisa atapata fedha, yeye ajali kitu. Kinachoangaliwa ni pesa


Vijana smart, wengi walijikuta kwenye mfumo rasmi huu wa kibongo, wamejikuta trapped na mfumo usiojari vipaji na uwezo wa watu katika utumishi na kujikuta ujira wao unapangwa kwa ngazi za mishahara na pengine pasipo kuzingatia ufanisi wao. Ndo maana haishangazi TO anaefanya kazi katika almashauri X kuzidiwa maisha na kilaza mmoja aliajiriwa kwa mchongo wa mjomba BOT Kama afsa manunuzi, lakini ana opportunity kibao za 10 percent kwenye denda za wizara.

Huyu kilaza mtaani ataheshimika sana kuliko smart mind aliyeko almashauri akipigika kusubiri fedha ya OC ili alipwe overtime.

Issues kama hizi zinanilazimisha kuamini tunahitaji kutathimini value of our life. Lazima tuheshimiane kwa kile tunavyoweza ongeza value kwenye maisha ya watu.

Haijalishi kwa kuwa ni mwalimu na mfumo wa kiutumishi ujanipa kipaumbele, unizalau coz siendeshi gari ya maana.
 
kwenye miti hakuna wajenzi.. yaani na ma AAA yako yote umeishia kuajiriwa serikalini kwa mshahara wa hazina... ma scholarship yote yaliyojaa duniani umeyaacha unahangaika na forex na mwisho wa siku unatapeliwa na wadogo zako kina ontario...

wahuni wana div 3 za mwisho tena za HKL ila ajira za maana kwenye mabalozi.. au wanajiajiri wenyewe wanagombania tenda na kupiga hela..

nashangaaga sana best students kuwaona udsm... ukikomaa kweli kweli na ukawa na washauri sahihi unatembea mapema sana.. bongo nyoso
Haki ya nani, nilipoona maelezo yako haya imebidi nirudie kumsoma tena Engineer ili nione mahali aliposema "kaajiriwa na serikali"; Walahi sijapaona, eti ni wapi!?
 
Wabongo tuache uchawi, Tajiri unamchukia, Aliyefaulu unamchukia Aliye na nyazfa unamchukia, hv tumerogwa na nani, Weng humu wanapenda wapiga nyeto, Maskin wenzao, Vilaza wenzao, wavuta bangi. Huu ni upuuzi kwaio mnataka wote tufeli maisha? shenz kbsaa bichwa kubwa kumbe limejaa bisi na mabunda, mnakera sana.
 
kumbe mie kichwa sana!mie mambo yote nilikuwa namalizia pale darasani.nilikuwa sisomi tena wala ku solve chochote baada ya muda wa darasani.
 
Back
Top Bottom