Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Dah nilichokiona katika huu Uzi kuna watu mna historia na upinzani wa chini kwa chini kumbe ambao sie wengine tulikuwa hatuujui kumbe mnafahamiana kutoka huko FOREX sasa sie tuliodandia mmetuingiza chaka na kutafuta upande wa kulaumu kuwa hauthamini upande mwingine.

Ushauri wangu tupambane tu na maisha mliosoma na ambao pia hatukusoma maana hiyo ndo dhamira ya kila binadamu.

nashangaa watu mliovamia kumbe vita yetu ya simba na yanga.. na jioni usikute tunakunywa bia pamoja.. sijui mtajificha wapi... huyu kitambo sana mpinzani
 
hata chuo sijafika.. ila maisha nayoishi ni wachache sana wameyafikia.. mimi hata a level sijasoma.. niliishia o level tu then college ya kizushi kisha nikazama mtaani.. karibu sana tupambane kitaa.. huku hakuhitaji A za physics bali ni kujua kuusoma mtaa
Damn!!!!!!!AAA kawekee Necta na onesha wajuku zako baadae.Haiwezekani kabisa wote tunafanana na Ronaldo kiumri na Messi na wengine tumepitwa Mbape sijui Ngolo Kante...halfu tuna salary slip ya makato asilimia 45 ya mshahara wako.Na ukute hata ujibane paso kwa mwaka hununui....Naishia hapaa
 
nashangaa watu mliovamia kumbe vita yetu ya simba na yanga.. na jioni usikute tunakunywa bia pamoja.. sijui mtajificha wapi... huyu kitambo sana mpinzani
Hongereni simba na yanga sie mahabiki wa Faru Jeuri ngoja tupite tu.
 
anafikiri AAA za physics ukienda nazo dukani unapewa unga,,, au unanunua gari kwa cheti cha AAA huku ni maujanja ujanja tu.. mwisho wa siku dogo ontario kamtapeli hela zake pamoja na AAA zake.. huo ndio mtaaa sasa
Hahaha!dah hapa kweli mjini
 
hongera sana mkuu,mimi nilisoma kwa kila namna lakini ilifika kipindi akili inaniambia ili somo uwezo wako nikupata F au D yaani kwa kifupi Mungu ametuumba kiakili uwezo tofautitofauti.
Yaani unasoma mpaka inafikia kipindi unaona somo halieleweki sawa na kusukuma mlima kilimanjaro

Wee ulitakiwa ubebe hivyk hivyo tuu...ishu sii kupita tuu
 
Hizi mbwembwe acheni nyie...happy duniani kinachomata ni hiki "Bora uzaliwe mwenye babati kuliko mwenye kipani"
Mliokosa akili za darasani huwa mnajifariji, hamkubali kushindwa.
Mwenye akili habahatishi, wewe mwenye bahati japo una bahati ila unabahatisha.
 
Kusoma ama Maisha hayana formula maalum!! Kinachohitajika ni kufocus kwenye kitu unachohitaji na kuweka nguvu zaidi!

NB; USISAHAU KUMWOMBA MUNGU AKUPE MWANGA WA KUKUONGOZA UENDAPO
 
Mliokosa akili za darasani huwa mnajifariji, hamkubali kushindwa.
Mwenye akili habahatishi, wewe mwenye bahati japo una bahati ila unabahatisha.

Acha zako unaakili za kurudia Mambo ya wenye akili....sio tunajifariji Hui ndio ukweli ukitaka uthibitisho muulize benzima
 
Kuna watu mnamponda jamaa, kisa nyinyi hamja soma sana ila mna maisha mazuri, lkn cha ajabu watoto wenu wa kuwazaa mmewapeleka shule za gharama. Sasa si mngewaacha watoto zenu wakae nyumbani ili wasimamie hizo biashara zenu kwani mkiwapeleka shule watachelewa kushika hela. Hongera mwana kwa kupiga kijiti cha 3.
 
Unawaambia waache kulala huku kichwa kina eleza wafaulu bila kukesha.
Jinga sn ww
 
Hongeren kwa nafas zenu.
Cha msingi tutimize majukum yetu.


Kama haujasoma na umefanikiwa sawa-SAIDIA JAMII

kama umesoma na umefanikiwa -JITAHID UFAIDISHE NA WENGNE ELIMU YAKO.

NB:
ILA KWA MANENO HAYO@CCNP ENGINEER....UNAONEKANA HUJAFAIDIKA VYAKUTOSHA
Hii point makini sana
 
Last week nilikua napitia matokeo ya madogo wa form six kwa Special Schools (Mzumbe, Tabora Boys, Kibaha na Ilboru) lengo ni kuhesabu One za Tatu yaani ni za kutafuta kwa tochi... Nimeambulia kuona moja tu ya dogo wa Mzumbe alokua T.O (dogo mwenyewe PCB, sijui PCM siku hizi wamerogwa na nani).

Huu ni ushauri kwa madogo ambao mpo Advance na mna munkari wa kupiga One Kali tatizo hamjui strategies zipi mtumie. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma sana na kufaulu. Kusoma sana sio kufaulu, bali kusoma kwa technique.

Mbinu nilizotumia kupiga One ya 3 bila kukesha darasani:

Target Audience:
Wanafunzi waliopo Advance (five na six) hasa PCM (shule za Private hawahusiki sababu wana walimu na miundombinu ya kutosha)

Malengo:
Weka malengo ya kupiga One Kali. Yaani kila somo lisome ukiwa na mind za kupata A. Ukijiwekea malengo ya kupiga A lazima utakua unasoma kwa focus.
Mie wakati naingia form five nikaweka malengo kuwa lazima nipige one ya 3 na niingie Top 3 kitaifa. Na ikawa hivo mwisho wa siku.

Timetable:
Sikua na fixed (defined) ratiba kama wenzangu walivokua wamebandika ndani ya matranka yao au ukutani pembeni ya kitanda. Mie nilikua nasoma kwa mood.
Nilikua na alternate kati ya Physics na Chemia. Napiga maswali ya Gravitation nikichoka nafunga kesho napitia Inorganic Chemistry.

Hesabu nilikua napitia kila siku nikitaka kulala (somo la kulalia). Mfano nikitoka class kupiga maswali ya Electronics narudi Dom nafungua pure II napiga maswali yangu 20 ya Complex Number then nalala.

Kuna wakati najikuta nasoma Physics hata week nzima (mfano napoamua kupitia Mechanics), yaani kifupi sikua na ratiba fixed, nasoma kutokana na nataka nikave topic zipi kwenye somo husika.

Achana na tabia ya kusoma kwa ratiba, soma kulingana na somo lipi topic ipi upo nyuma sana. Topic ipi hujapitia maswali mengi, topic ipi umeanza kusahau. Lazima upige One ya 3.

Kabla sijasahau: Mie usiku mwisho wangu kusoma ilikua saa nne. Mchana ndio muda wangu wa kupiga kitabu, giza likiingia tu basi nakua zoba. Usually ikifika saa tatu usiku kama sijaenda prepo basi siendi tena, napitia hesabu kitandani nalala.
But mchana hunikuti nafanya upuuzi (labda jioni kwenye jogging uwanjani).
Lazima upige One ya 3.

Twende kwenye masomo husika sasa:

Physics:
Vitabu nilivosoma mpaka napiga pepa: (Chandy, Nelkon na Roger Muncaster).
Katika somo unalotakiwa upitie vitabu vingi ni Physics. Lakini mie nilikua mjanja. Nilipitia vitabu ambavyo NECTA wanapenda kutoa maswali basi. Vingine nikaachana navyo.

Nilianza na Chandy, then nilipo kimaliza nikaja Nelkon (hiki hata sikusoma, bali nilifanya maswali yote ya mle sababu hakina maelezo mengi). Then form six mwishoni nikamalizia Roger (japo kina maswali magumu, nilijitahidi kufanya, yaliyonishinda nikaachana nayo)

Ukitaka kuelewa Physics basi soma Chandy (wahindi wanaeleza mpaka una enjoy), but ukitaka kufaulu Physics NECTA piga maswali karibu yote ya Nelkon na Roger Muncaster. NECTA wanapenda kutoa maswali kutoka kwenye Nelkon na Roger.

Practical za Physics zote nilifoji wakati wa pepa. Ukijifanya kupiga practical real hutomaliza muda hautoshi. Ukikaribia NECTA jifunze namna ya kufoji practical za Mechanics, Heat na Umeme.

Lazima upige One ya 3.

Chemistry:
Katika masomo yaliokua mteremko kwangu basi ni Chemistry. Kwanza kabisa ndio somo ambalo sikuwahi kabisa kusoma Vitabu. Niliishia kusoma Notes tu pamoja na kupitia Past Papers za NECTA.
Yaani nilikua nashangaa watu wanakomaa kusoma Ramsden usiku wa manane wakati Chemia ni mwendo wa notes tu unapiga banda. Practical zake ndio chai kabisa.

Kifupi ni kuwa ukitaka kupiga banda la Chemia with minimum efforts fanya hivi:
Soma notice za topic husika (mfano Electrochemistry), ukishaelewa chukua Review ya NECTA, pitia pepa moja baada ya nyingine kwa topic (achana na tabia ya kupitia pepa zima matopic yote utaloose concentration, nenda topic by topic).
Ukimaliza rudi tena kwenye notice, soma topic nyingine (mfano Organic) then njoo tena kwenye Review, fanya hivo hivo. Hadi umalize topic zote.

Practical za Chemia zote nilifanya real, sikufoji hata moja. Sababu praki za Chemia ni simple, sinafanyika ukifata procedure. Kifupi Chemia hutakiwi kukosa A au B+. Mie nilipiga A kali nikaongoza Chemia kitaifa form six yetu. Watu wamekomaa na mavitabu nikawakimbiza kama kawa.
Lazima upige One ya 3.
View attachment 818007



Advanced Mathematics:
Katika somo ambalo nilikua nasomea kitandani ni hesabu. Kwanza kabisa sikua na ratiba maalum ya kusoma hesabu. By the way hesabu hatusomi, bali huwa tuna solve.
Nilianzaga kukomaa na Tranter kubabake kikanishinda. Nikaachana nacho.
Nikakomaa na Pure I na II nikakomaa nazo na sikuwahi kusoma kitabu kingine chochote zaidi ya hivi viwili.
Style yangu ile ile, nasoma topic (mfano Integration) then nazama kwenye NECTA Review napiga maswali yote ya Integration mpaka yaishe. Nikimaliza natafuta another topic hivo hivo.
Lazima upige One ya 3.

Mwisho Kabisa:
Watu wanaamini kuwa ili ufaulu masomo ya sayansi kwa One kali lazima uende ukapige mapindi kwa tuition center za Dar (Mgote, Moody, Mtiga, Mbuga etc).
Hilo sio kweli, sio kweli, ni uongo.

Mie sikuwahi kusoma tuition yoyote Dar. Nilipiga mapindi ya vichochoroni tu.
Mengine tulifundishana na wenzangu shule. Na topic zingine niliamua kusoma mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kunifundisha (mfano Modern Physics, Static Electricity, Complex Numbers, Statistics).

Vijana acheni kulala, wekeni malengo ya kupiga One kali ili inapofika stage ya kuomba vyuo unak ua na wide selection ya kwenda chuo na course unayotaka.
Lazima upige One ya 3.

View attachment 818008
Unaweza kua na points nzur lakin taarifa yako imetawaliwa na ujivuni mwingi na sina hakika km inaweza kua na msaada kwa wanafunzi wengi zaidi watapotea kama watafata ushauri wako as ulivyoupresent.

Kumshauri mtu asome apate one ya 3 ni lazima awe mtu unaefahamu uwezo wake na speed yake ya kuelewa na kukumbuka vitu, mtu aliepata C ya Maths or Chemistry akifata njia yako atatoka na S advanced.

So its a good thing na hongera kwako but ushauri wako ni mbovu sana, umetawaliwa na majivuno na sifa nyingi.
 
Nimejifunza kitu ila sina nafasi tena mimi umri ushapita but naitamani sana ya 3 mimi nilipata ya 6 mkuu but still nawaza kwann sikumake wonders?
 
Yaan tuna wivu wa kijinga jamaa kaonyesha jinsi Gani alifaulu vizur leo ametoa mbinu watoto wazitumie tunishia mponga na HKL zetu za div 3 jamani,Bro nahis we Ni Elias Kihombo,ambae yupo Geita Nini? Ila mkuu nikupe hongera Sana kuonyesha njia kwa watoto wetu ,Mungu akubariki
 
Nilipata sifa sana, kwangu na kwa shule yangu nilosoma.
Mama yangu alikua proud of his son (you know, unless you dont have plans to have kids)
Nikaitwa Bungeni na kupewa zawadi na Prime minister, Mkemia mkuu wa serikali.

Nika apply chuo nachokitaka kwa Course nayoitaka (bila kuhofia competition).
Nikapata scholarship ya TCRA 100%.

Mwisho wa majibu ya swali lako
Mkuu o level ulipata ngapi?
 
  • Thanks
Reactions: apk
Back
Top Bottom