Uzi huu umenizibitishia ambavyo hekima bila noti, uishia kuzalauliana.
Mleta mada, kwa namna yoyote ile ni kijana smart upstairs.
Kwa nchi za wenzetu vipaji Kama hivi ni lulu na ni asset kubwa na utazamawa kwa jicho la hekima hata kama hana hela.
Ubora wa mtu hauko kwenye uwezo wa kuwa na gari kali au kuishi kwenye mjengo wa maaana
Context za maisha yetu hutofautiana, likewise hata destiny za maisha yetu
Siku za hivi karibuni kuna watu wanaojiita wana elimu ya kitaa na wana make bingo ya maana, hali inayopelekea hata just discourage wasomi.
Kwa bahati nzuri kundi hili ukiri wao ni watu wa mishe, frankly speaking wengi ni watu wasio heshimu maadili, kila aina ya dili regardless itamtaka kuiba, kuua, na hata kufanya ushenzi wowote kisa atapata fedha, yeye ajali kitu. Kinachoangaliwa ni pesa
Vijana smart, wengi walijikuta kwenye mfumo rasmi huu wa kibongo, wamejikuta trapped na mfumo usiojari vipaji na uwezo wa watu katika utumishi na kujikuta ujira wao unapangwa kwa ngazi za mishahara na pengine pasipo kuzingatia ufanisi wao. Ndo maana haishangazi TO anaefanya kazi katika almashauri X kuzidiwa maisha na kilaza mmoja aliajiriwa kwa mchongo wa mjomba BOT Kama afsa manunuzi, lakini ana opportunity kibao za 10 percent kwenye denda za wizara.
Huyu kilaza mtaani ataheshimika sana kuliko smart mind aliyeko almashauri akipigika kusubiri fedha ya OC ili alipwe overtime.
Issues kama hizi zinanilazimisha kuamini tunahitaji kutathimini value of our life. Lazima tuheshimiane kwa kile tunavyoweza ongeza value kwenye maisha ya watu.
Haijalishi kwa kuwa ni mwalimu na mfumo wa kiutumishi ujanipa kipaumbele, unizalau coz siendeshi gari ya maana.