Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

Wapi nimeweka majivuno??? Kusema kuwa nilikua nasoma kwa ujanja nikafaulu ndio majivuno??
By the way kama mtu amefaulu malengo alokua amejiwekea kwanini asijivunie???
Mnaionwea wivu ama... Wewe mtoto wako akifaulu form four akapiga ONE YA 7 hautajivunia??

Ballagh-Shatwain
Dogo unazingua, acha misifa ya kijinga. Kaa utulizane jinsi ya kuwasilisha mambo.

Pitia jamii forum mwanzo mwisho uone Kama kuna mwanaume amejisifia kupata point 3.

Wanaume hatujazoea hii kitu. Aidha unajipa moyo kwa sababu hujafanikiwa ulivyotaka hivyo unataka watu wakurecognise.

Shwain mwenyewe. Eti my mum was happy. Te he te he. Tutakupa heshima kwa jinsi ulivyo, sio kututisha na AAA.
 
Ujivuni na kujiona zaidi vinaweza kumfanya mwerevu akawa mjinga.
Mpongeze dogo alikunja 1.3(PCM) , 4.6GPA (First class)

Mimi ,nawafatilia tu hawa vijana kwenye mjadala wao ,maana kuna vingine vinanichekesha tu na vingine vinafurahisha
 
hongera sana mkuu,mimi nilisoma kwa kila namna lakini ilifika kipindi akili inaniambia ili somo uwezo wako nikupata F au D yaani kwa kifupi Mungu ametuumba kiakili uwezo tofautitofauti.
Yaani unasoma mpaka inafikia kipindi unaona somo halieleweki sawa na kusukuma mlima kilimanjaro
Unavyosema ni sahihi. Kitu kimoja nitofautiane nae ni hili la kuwashauri kusoma bila kuwa na ratiba. Mimi naona, watu tunatofautiana kwenye uwezo wa kuzingatia mambo. Usipokuwa na ratiba unaweza ukakosa focus. Ratiba ni muhimu sana ni kama plan of action. Plan of action isipokuwepo huwezi kujua kama umefanikiwa katika kukamilisha jambo fulani. Isipokuwa nakubaliana naye kwamba kama ratiba yako kusoma somo fulani, uhakikishe unadeal na topics ambazo you are not conversant.! Kitu kingine nachokubaliana naye ni swala la muda. Vijana wengi wanapoteza muda sana mchana kwa kufanya vitu visivyo muhimu, na matokeo yake wanaona wacompasate muda wa usiku. Hii ni mbaya sana, kwani ni muhimu kutumia muda wako ipasavyo kwa kutimiza majukumu yako ya kiuanafunzi, yaani kujifunza.
 
Endeleeni kubishana na mtu km huyu
Screenshot_20180726-125630.jpg
 
Waafrika wana roho ya kwanini sana. Hawapendi kuona mwenzao ana kitu kizuri.

Kila mtu asifiwe kutokana na jema alilonalo. Ninyi wenye hela mtasifiwa kwa hela zenu, na wenzenu wenye akili watasifiwa kwa akili zao. Ninyi mna hela, na wenzenu wana akili.

Japo mimi nilifeli form four, ila ninawathamini sana wenye akili, na ninafurahi sana ninapoona mtu kapata one kali.

Hizo gari zenu zimetokana na wenye akili, zimetengenezwa kutokana na elimu. Bila ya hawa wenye akili, vitu vingi mnavyomiliki msingekuwa navyo.

Wenye akili wanaitengeneza dunia.
PUMBAVU NYIE.

Ungekua ulipata angalau division three usingetukana. Pambana na hali yako
 
Kusoma nikitu kingine mkuu watu wamesoma hadi wanatoboa ozone lakini matokeo madogo,habari ya kusoma inahusisha na IQ ya MTU na mtu
 
Mm mwenyew nimesoma advance PCB naelewa Masomo yalivokuwa magumu hongera Kwa ufaulu wako Kama Kweli uliyofanya n Kweli
 
Last week nilikua napitia matokeo ya madogo wa form six kwa Special Schools (Mzumbe, Tabora Boys, Kibaha na Ilboru) lengo ni kuhesabu One za Tatu yaani ni za kutafuta kwa tochi... Nimeambulia kuona moja tu ya dogo wa Mzumbe alokua T.O (dogo mwenyewe PCB, sijui PCM siku hizi wamerogwa na nani).

Huu ni ushauri kwa madogo ambao mpo Advance na mna munkari wa kupiga One Kali tatizo hamjui strategies zipi mtumie. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma sana na kufaulu. Kusoma sana sio kufaulu, bali kusoma kwa technique.

Mbinu nilizotumia kupiga One ya 3 bila kukesha darasani:

Target Audience:
Wanafunzi waliopo Advance (five na six) hasa PCM (shule za Private hawahusiki sababu wana walimu na miundombinu ya kutosha)

Malengo:
Weka malengo ya kupiga One Kali. Yaani kila somo lisome ukiwa na mind za kupata A. Ukijiwekea malengo ya kupiga A lazima utakua unasoma kwa focus.
Mie wakati naingia form five nikaweka malengo kuwa lazima nipige one ya 3 na niingie Top 3 kitaifa. Na ikawa hivo mwisho wa siku.

Timetable:
Sikua na fixed (defined) ratiba kama wenzangu walivokua wamebandika ndani ya matranka yao au ukutani pembeni ya kitanda. Mie nilikua nasoma kwa mood.
Nilikua na alternate kati ya Physics na Chemia. Napiga maswali ya Gravitation nikichoka nafunga kesho napitia Inorganic Chemistry.

Hesabu nilikua napitia kila siku nikitaka kulala (somo la kulalia). Mfano nikitoka class kupiga maswali ya Electronics narudi Dom nafungua pure II napiga maswali yangu 20 ya Complex Number then nalala.

Kuna wakati najikuta nasoma Physics hata week nzima (mfano napoamua kupitia Mechanics), yaani kifupi sikua na ratiba fixed, nasoma kutokana na nataka nikave topic zipi kwenye somo husika.

Achana na tabia ya kusoma kwa ratiba, soma kulingana na somo lipi topic ipi upo nyuma sana. Topic ipi hujapitia maswali mengi, topic ipi umeanza kusahau. Lazima upige One ya 3.

Kabla sijasahau: Mie usiku mwisho wangu kusoma ilikua saa nne. Mchana ndio muda wangu wa kupiga kitabu, giza likiingia tu basi nakua zoba. Usually ikifika saa tatu usiku kama sijaenda prepo basi siendi tena, napitia hesabu kitandani nalala.
But mchana hunikuti nafanya upuuzi (labda jioni kwenye jogging uwanjani).
Lazima upige One ya 3.

Twende kwenye masomo husika sasa:

Physics:
Vitabu nilivosoma mpaka napiga pepa: (Chandy, Nelkon na Roger Muncaster).
Katika somo unalotakiwa upitie vitabu vingi ni Physics. Lakini mie nilikua mjanja. Nilipitia vitabu ambavyo NECTA wanapenda kutoa maswali basi. Vingine nikaachana navyo.

Nilianza na Chandy, then nilipo kimaliza nikaja Nelkon (hiki hata sikusoma, bali nilifanya maswali yote ya mle sababu hakina maelezo mengi). Then form six mwishoni nikamalizia Roger (japo kina maswali magumu, nilijitahidi kufanya, yaliyonishinda nikaachana nayo)

Ukitaka kuelewa Physics basi soma Chandy (wahindi wanaeleza mpaka una enjoy), but ukitaka kufaulu Physics NECTA piga maswali karibu yote ya Nelkon na Roger Muncaster. NECTA wanapenda kutoa maswali kutoka kwenye Nelkon na Roger.

Practical za Physics zote nilifoji wakati wa pepa. Ukijifanya kupiga practical real hutomaliza muda hautoshi. Ukikaribia NECTA jifunze namna ya kufoji practical za Mechanics, Heat na Umeme.

Lazima upige One ya 3.

Chemistry:
Katika masomo yaliokua mteremko kwangu basi ni Chemistry. Kwanza kabisa ndio somo ambalo sikuwahi kabisa kusoma Vitabu. Niliishia kusoma Notes tu pamoja na kupitia Past Papers za NECTA.
Yaani nilikua nashangaa watu wanakomaa kusoma Ramsden usiku wa manane wakati Chemia ni mwendo wa notes tu unapiga banda. Practical zake ndio chai kabisa.

Kifupi ni kuwa ukitaka kupiga banda la Chemia with minimum efforts fanya hivi:
Soma notice za topic husika (mfano Electrochemistry), ukishaelewa chukua Review ya NECTA, pitia pepa moja baada ya nyingine kwa topic (achana na tabia ya kupitia pepa zima matopic yote utaloose concentration, nenda topic by topic).
Ukimaliza rudi tena kwenye notice, soma topic nyingine (mfano Organic) then njoo tena kwenye Review, fanya hivo hivo. Hadi umalize topic zote.

Practical za Chemia zote nilifanya real, sikufoji hata moja. Sababu praki za Chemia ni simple, sinafanyika ukifata procedure. Kifupi Chemia hutakiwi kukosa A au B+. Mie nilipiga A kali nikaongoza Chemia kitaifa form six yetu. Watu wamekomaa na mavitabu nikawakimbiza kama kawa.
Lazima upige One ya 3.
View attachment 818007



Advanced Mathematics:
Katika somo ambalo nilikua nasomea kitandani ni hesabu. Kwanza kabisa sikua na ratiba maalum ya kusoma hesabu. By the way hesabu hatusomi, bali huwa tuna solve.
Nilianzaga kukomaa na Tranter kubabake kikanishinda. Nikaachana nacho.
Nikakomaa na Pure I na II nikakomaa nazo na sikuwahi kusoma kitabu kingine chochote zaidi ya hivi viwili.
Style yangu ile ile, nasoma topic (mfano Integration) then nazama kwenye NECTA Review napiga maswali yote ya Integration mpaka yaishe. Nikimaliza natafuta another topic hivo hivo.
Lazima upige One ya 3.

Mwisho Kabisa:
Watu wanaamini kuwa ili ufaulu masomo ya sayansi kwa One kali lazima uende ukapige mapindi kwa tuition center za Dar (Mgote, Moody, Mtiga, Mbuga etc).
Hilo sio kweli, sio kweli, ni uongo.

Mie sikuwahi kusoma tuition yoyote Dar. Nilipiga mapindi ya vichochoroni tu.
Mengine tulifundishana na wenzangu shule. Na topic zingine niliamua kusoma mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kunifundisha (mfano Modern Physics, Static Electricity, Complex Numbers, Statistics).

Vijana acheni kulala, wekeni malengo ya kupiga One kali ili inapofika stage ya kuomba vyuo unak ua na wide selection ya kwenda chuo na course unayotaka.
Lazima upige One ya 3.

View attachment 818008
real nimekukubali
 
Back
Top Bottom